Over act/deed.
Hili nilisalisemaga kwenye Uzi wangu wa
Uchambuzi na Tathmini | Final submission ya Tundu Lissu nilisema kwamba neno "
The Public" ni pana sana na ndicho kinachomtesa katuga now.
Katuga anasema kwamba Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code kimeanza na maneno “
any person or group of persons”, lakini katika hati ya mashitaka Jamhuri imetumia maneno “
the public” kwa sababu, kwa mujibu wa hoja yake, public inaweza kujumuisha watu hao.
Hapa Katuga anarejea pia maana ya “
public” katika Kifungu cha 5 cha Penal Code.
Naomba niseme wazi:
Katuga, hapa unakula kinyesi chako mwenyewe.
Why?
Kwa sababu tunahitaji kurudi kwenye kanuni ya kwanza kabisa ya kutafsiri sheria ya jinai. Hatuanzi na kutafuta kifungu kingine ili tutengeneze kosa; tunaanza na kosa ambalo mshtakiwa ameshtakiwa nalo, kisha tunaangalia kama particulars zilizowekwa kwenye hati ya mashitaka zinaangukia ndani ya maneno ya sheria hiyo.
Kifungu cha 39(2)(d) ndicho kinachounda offence inayojadiliwa hapa.
Kwa hiyo swali la kwanza si,
Neno public linaweza kumaanisha nini katika Penal Code?
Swali la kwanza ni,
Kifungu cha 39(2)(d) kinataka nini hasa, na hati ya mashitaka imefuata maneno na elements za kifungu hicho kwa usahihi gani?
Katuga Pia ametumia Kifungu cha 135 cha CPA Kwenye kuandaa Hati ya mashtaka bila kumpa accused taarifa ya kutosha kuhusu nature ya offence, tatizo hilo linaweza kuathiri validity ya charge kwasababu CPA inataka uandike kila kitu kuhusu Nature ya Offence. Yaani Hati ya mashtaka ilitakiwa iseme wazi kwamba tunakopa tafsiri ya neno "
Any person or
Group of persons" kwenye Kifungu kingine cha sheria tofauti na s.39(2)(d).
Hapa sasa katuga anapaswa kuulizwa,
Je, nani anaethibitisha kuwa huo huma umeshawishika na hayo maneno ya lissu?