SEHEMU YA 8.
Mahakama ya Rufaa ilirejea Shauri la Jinai la Mwesige Godfrey and Another Vs Jamhuri.
Rufaa ya Jinai Namba 354 ya 2015, TanzLII, 19 February 2015.
Ambapo Mahakama hii ya Rufaa katika kesi hiyo ilirejea kesi ya Camnetti Vs United States, 242 U.S. 470, 227 (1917).
Mahakama ilisema kwamba sheria inatakiwa mwanzo kabisa itafsiriwe kwa lugha yake ambayo imetengeneza.
Na jukumu la Mahakama kuweza kutumia sheria hivyo ilivyo (Plain Meaning Rule).
Waheshimiwa Majaji, kesi hii iliendelea mbele ku-quote maneno yaliyopo katika kesi Mwesige Godfrey:
Connecticut Nat. Bank v. Germain, 503 U.S. 249 (1992).
Waheshimiwa Majaji, kama tulivyoeleza awali, kazi ya hati ya mashitaka ni kumu-inform Mshtakiwa.
Ni msimamo pamoja kwamba Mshtakiwa anaweza kuwa further informed kutokana na aina ya mashitaka yake kutokana na ushahidi utakaotolewa na upande wa Jamhuri.
Waheshimiwa, zipo kesi nyingi za kumfanya Mshtakiwa aelewe mashitaka yake.
Daniel Ruhele Vs Jamhuri, Criminal Appeal Number 201 of 2007, TanzLII, 1 March 2012, TZCA 269.
Katika ukurasa wa 5, though katika kesi hii walikuwa wanaona element moja haijawa cured na ushahidi.
Mbali na mashauri mengi, lakini ni moja ya kesi inaonyesha hata kama hujawa informed na charge, lakini ushahidi unaweza kukufanya ujiandae na utetezi.
Mahakama yenu itaangalia nature ya ushahidi wa Prosecution na utetezi.
Je, wakati anajitetea alikuwa haelewi au alikuwa anaelewa anachojitetea?
PW1 George Bagyemu katika ushahidi wake anaiambia Mahakama kwamba Mshtakiwa alitoa maneno ya kutishia Serikali.
Serikali ambayo jukumu lake ni kulinda sheria, na uchaguzi unatokana na sheria.
Hivyo kutishia uchaguzi ni kutishia Serikali.
Shahidi wa 6, katika ukurasa wa 445, PW16 anaiambia Mahakama hii kwamba maneno yale yanatishia Serikali ambayo ina jukumu la kulinda nchi.
Na maneno hayo yalilenga amani na utulivu.
Na kwamba wenye jukumu la kulinda amani na utulivu...
Katika ukurasa huohuo, shahidi anasema maneno hayo hayakulenga tu kuvuruga amani.
Kwa hiyo Waheshimiwa Majaji, Shahidi PW16 anaelezea kwamba maneno ya Mshtakiwa yatahamasisha uasi na atavuruga uchaguzi.
Ni vitisho dhidi ya Serikali, ambapo ni jukumu la Serikali kulinda hizo sheria.
Ushahidi wa mashahidi hawa wawili unaungwa mkono na ushahidi wa utetezi DW1, Mshtakiwa mwenyewe, katika ukurasa wa 619.
Wakati akidodoswa maswali.
Lakini pia katika ukurasa wa 622, Waheshimiwa Majaji, Mshtakiwa anasema jukumu la maintain order ni la Polisi, na mbele anasema Polisi wanafanya kazi chini ya Serikali.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi huu unaonyesha hati ya mashitaka imeeleweka na kumfanya aandae ushahidi wake.
Kwa hiyo ikitokea Mahakama inapenda kujiuliza Executive iliyotumika katika hati ya mashitaka ni wapi, maana ibakie kuwa ni Plain Meaning.
Point muhimu ya Mahakama yenu ambayo tunaomba to consider inaweza kuwa ni kiini cha Kifungu cha 39(2)(d).
Umetumia for the purpose of intimidating the Executive.
Neno lililotumika hapo linamaanisha kama Serikali ilitishika is immaterial.
Waheshimiwa, samahani tunatumia muda mwingi kufafanua hiki kifungu kwa sababu hiki kifungu hakijawahi kutumika.