Mahakamani 29 Septemba 2026: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

unataka wahukumu unavyotaka wewe, tulia hao majaji wanajua wanachofanya mbona mnajiongelesha sana.
 
Final submmision ya Likatuga anathibitisha Lisu si mhaini, bali Mungu aliwanyima maono kesi ya kumbambika.

Hata wanaobambikiwa kesi za murder huwa si lengo wanyongwe bali uhangaike na hiyo kesi miaka isiyopunguwa kumi ukiwa jela, sasa siku hizi kuna kesi zimewekewa muda maalum lazima ziishe.

Huu ndio ushetani anaoufanya pia Museven kwa Kiza Besigye.
 
SEHEMU YA 7.

Waheshimiwa Majaji, kiini hiki hakikupingwa wakati wa hoja za awali zilizofanywa mbele ya Mahakama hii.

Ilikuwa ni moja ya undisputed facts kwenye Preliminary Hearing iliyofanyika tarehe 22 September mwaka jana, ukurasa wa 133.

Mshtakiwa alikubali kwamba yeye ni raia wa Tanzania na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waheshimiwa Majaji, kwa mujibu wa Kifungu cha 198 CPA, Sura ya 20, iliyorekebishwa mwaka 2023, zoezi hili siyo la mapambo.

Jambo lolote ambalo litakuwa undisputed litakuwa limeingia kwenye orodha.

Haya siyo maneno ya Katuga, Waheshimiwa, bali ni Kifungu cha 198(4) kinachosema yale mambo ambayo hayana formal disputes hayana sababu, unless Mahakama ielekeze.

Kwa faida ya Kifungu cha 198, ileweke jukumu la Jamhuri: inatakiwa kuthibitisha kile ambacho kipo katika hati ya mashitaka.

Hoja ambayo imekataliwa kwenye Preliminary Hearing siyo kazi ya Jamhuri kuthibitisha hoja hiyo.

Waheshimiwa Majaji, tuhuma zipo kwenye hati ya mashitaka. Summary of evidence zilizopo katika Preliminary Hearing hazitengenezi tuhuma.

Hata zikiwa zimetengenezwa, ni kumpa Mshtakiwa kuzijibu au kuzikataa.

Kama anakubaliana nazo, linaingia katika Memorandum of Undisputed Facts, Waheshimiwa.

Ni segment ambayo zile summary ambazo ni Memorandum of Agreed Facts.

Summary of evidence haitengenezi tuhuma.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kumaliza hoja ya kwanza, ambayo imethibitika kwa Mshtakiwa kukubali kwake mwenyewe, Mahakama yenu tukufu inabaki na hoja mbili.

Waheshimiwa Majaji, neno Serikali katika Kifungu cha 39(2) limetumika neno Executive.

Hakuna tafsiri mahususi ya neno Executive wala Judiciary.

Tukisema Judiciary, unakuwa umemtishia nani, au Bunge?

The same to Executive, haionyeshi umemtishia nani.

Ukisoma Kifungu cha 39, hakijatumbia Serikali ni nani, ikabaki Serikali ni Serikali.

Ni sawa na hata neno Mahakama, ndiyo halijawa defined.

Waheshimiwa Majaji, ni msimamo wa sheria kwamba inapaswa kutafsiriwa kama ilivyo au kama inavyosema.

Na hii njia ya kutafsiri sheria inaitwa plain meaning.

Kesi ya Nassibu Abubakar Aziega Vs Jamhuri, Criminal Appeal Number 146 ya mwaka 2021, TanzLII July 2024.

Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, ikikaa Mbeya.

Mahakama ya Rufaa ilirejea shauri la jinai la Mwesige Godfrey and Another Vs Jamhuri.
 
Hiyo ilikuwa mbinu ya majaji kuendelea kujipatia per diem zao za kutosha.

Kwa siku unakunja per diem ya 300,000 Tzs hata uwe wewe lazima ungesema kuna kesi ya kujibu.

Kufikia leo wamekunja sio chini ya Milioni 150 each.

Lakini kwa information iliyopo pale hakuna kesi ya kujibu maana ushahidi ulikuwa umepwaya vibaya sana hadi aibu kusema there is a case to answer.
Wakati kesi inaanza mliponda hivi hivi mwisho wa siku mwamba akakutwa na kesi ya kujibu ....ukimsoma Katuga kiufipa kweli utasema anapuyanga lakini ukimsoma kisheria anatumia vifungu kumjibu Lisu kuhusu hati ya mashitaka
 
Yaani anaiachia mahakama badala yeye aliyetumwa na CCM kuthibitisha hayo makosa mbele ya mahakama? Ama kweli hawa majaji wa CCM wanabebeshwa mzigo mzito sana!
Unajua mie nachoka kabisa, bafala wao waliofungua case waweke uthibitisho na ushahidi usio na shaka juu ya shauri lao. Eti wanawapa kazi mahakama iangalie makosa hayo km ni kweli ya kihaini au laah?

Huyu Katuga ni mzima kweli kichwani?
 
Nimeona point za Katuga linaelekea huko, Yule Mzee siku zote Yuko mbele ya muda, Ameshamalizana na hili Alisema hatakubali hukumu ya makosa ambayo hajashtakiwa nayo na aliyapinga kwa hoja na Sheria murua.

Pia Alisema hukumu ya uhaini haina kosa Dogo, ni Aidha uachiwe huru au uhukumiwe kunyonywa, nothing between.
 
Katuga na maCCM wenzake wanajitekenya na kucheka wenyewe
 
Unajua mie nachoka kabisa, bafala wao waliofungua case waweke uthibitisho na ushahidi usio na shaka juu ya shauri lao. Eti wanawapa kazi mahakama iangalie makosa hayo km ni kweli ya kihaini au laah?

Huyu Katuga ni mzima kweli kichwani?
Amechanganyikiwa bula shaka, sio bure!
 
Deed na over act tulishamalizana nazo kwenye dictionary ya Oxford advanced learners na Black Law dictionary
 
Wakati kesi inaanza mliponda hivi hivi mwisho wa siku mwamba akakutwa na kesi ya kujibu ....ukimsoma Katuga kiufipa kweli utasema anapuyanga lakini ukimsoma kisheria anatumia vifungu kumjibu Lisu kuhusu hati ya mashitaka
Alikutwa na kesi ya kujibu sababu jamhuri ndio iliyoamua. Hakuna wa kuipinga.
 
Ni aibu kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…