Walau sasa Nishati kutatakata kidogo..

January na Maharage walikuwa virusi na wahujumu wa taifa..

Naona ziara ya Mtwara imefyeka watumishi wengi sana. Madudu yalikuwa mengi bila shaka.
Naona kwenda kuhujumu TTCL
 
Nafikiri kazi kubwa ya Rais wa Tanzania ni kutua. No wonder JPM alidai alikuwa analalamikia saa 8 usiku akipitia majina ya wateule.
 
Mhh wahenga walisema mtu mzima ukifumaniwa chutama.....

Huu
 
Hii nchi mafisadi na wasio na elimu wala vipaji vyovyote ambao wamepata kazi kwenye system huwa hawana wasiwasi kabisa, kwasababu wanajua hata wakiharibu kazi au kuiba kitakachofanyika ni kuwahamishia kwenye sekta nyingine yenye maslahi kama yale au zaidi kabisa.


Mtu kama Maharage atasaidia nini TTCL ikiwa huku kwingine amefeli au ndio maswala ya trying&error system.?
 
Hii imedhihirisha kabisa kwamba viongozi waliowekwa TANESCO baada ya januari kuwa waziri walikuwa mafwafwa mazuzu watupu mpaka kupelekea nchi kuwa gizani sasa samia anahaha naona kamrudisha mhandisi kama ambavyo alikuwa akishauriwa

Mpaka mwenyekiti wa bodi kabadilishwa😁😁😁😁

Washukuriwe wote waliopaza sauti naona samia kapita mulemule.

Rais wa hovyo kuwahi kutokea Tanzania😕
 
Kwa hiyo TTCL ndo imepelekewa mtu incompétent. Yaani mtu kaharibu Tanesco anapelekwa kuwa mkurugenzi shirika lingine.Samia kweli anatuchezea akili.Sema na sisi sijui namna gani vipi.Maana tatizo la umeme tu,lazima tungeandamana.

Amna maharage kule Ndio sector yake uku ni connection tuu alipewa ila sio issue zake
 
Pamoja na Maharage kutolewa Tanesco ninampongeza kwa kazi moja tu nzuri aliyoifanya Tanesco ya kufuta kitengo cha Emergency kila ofisi ya Tanesco nchini na kuanzia Tanesco call center moja japo ninasikia ni mradi
wake basi kisifutwe baki kibaki na kiwe mali ya Tanesco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…