Maharage Chande aondolewa TANESCO, apelekwa TTCL. Gerson Msigwa awa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo
Ni UDINI tu. MTU amehalibu sehemu A anapelekwa sehemu B kuendelea kuhalibu tu.
Mm nataka umeme sio kuona kiza tu bandani kwangu.
 
Umeongea jambo la maana mkuu, watanzania tunashindwa kutambua chanzo cha tatizo la umeme kukatika badala yake Tunajikuta tunadili na Maharage..tumekuwa washabiki wa hovyo mnoo.
Aiseee ndugu yangu, naona kweli matatizo mengine Tz sio mtu, ila ni mifumo mibovu tuliyojiwekea na mambo kuendeshwa kisiasa zaidi, kuliko kuendeshwa kiutaalamu na kufuata abc's za kiuchumi..... endeleeni kula mtori, na nyama mtazikuta chini.....
 
Huyo Maharage ndo alisababisha umeme uwe unakatika a?
Nini kilitokea hapo katikati kilichopelekea mabadiliko hasi baada ya Kalemani na wenzake kutolewa wizarani na kwenye shirika la TANESCO respectively?

Kwanini ni baada ya Makamba na Maragwe kuingia ndio mambo yakaanza kwenda kombo tofauti na yalivyokuwa kwa miaka mitano nyuma (awamu ya tano)..?

Jibu ni kwamba, rasilimali watu ndio tatizo hapo TANESCO, hizi nyingine ni mbwembwe tu kutaka kuwatetea.
 
Walimuona chuma JPM chizi sasa wanarudi kwenye ramani zake. Mwenyekiti bodi ya Tanesco kapelekwa Meja Jenerali! Hii nchi ukichekacheka utashtuka hata wewe umeuzwa.
Hii nimeipenda pia, wajeda kidogo wana nidhamu
 
This is the huge Public deceiving ( shame kwa SHH), ivi kweli mtu kama Maharage kaharibu sehemu then anateuliwa tena sehemu kweli? Kweli jameni?

Kwamba kwa watanzania zaidi ya 20million wenye uwezo na sifa hawaonekani mpaka aliyeharibu point A kuhamishiwa point B kweli? Kweli SHH?

This proves the fact kwamba , Maharage alitumwa kukwapua na kahamishiwa TTCL akaharibu then aje na wazo la kubinafsisha, CCM ni zaidi ya ukoo wa Panya.

Huyu mwamba yangefanyika mawili kama angekuwa kwenye nchi zenye viongozi na uongozi, sio hawa wachumia tumbo,

Mosi, astaafishwe for the public interests

Pili, afunguliwe mashtaka maana tuhuma zake zinathibitika vizuri tu.

Haya yote yana mwisho.
Si ametoka kulamba tuzo majuzi hapa ya transformational leadership kwenye mashirika ya umma. Tanzania bana 😁😁😁

IMG-20230922-WA0078(2).jpg
 
This is the huge Public deceiving ( shame kwa SHH), ivi kweli mtu kama Maharage kaharibu sehemu then anateuliwa tena sehemu kweli? Kweli jameni?

Kwamba kwa watanzania zaidi ya 20million wenye uwezo na sifa hawaonekani mpaka aliyeharibu point A kuhamishiwa point B kweli? Kweli SHH?

This proves the fact kwamba , Maharage alitumwa kukwapua na kahamishiwa TTCL akaharibu then aje na wazo la kubinafsisha, CCM ni zaidi ya ukoo wa Panya.

Huyu mwamba yangefanyika mawili kama angekuwa kwenye nchi zenye viongozi na uongozi, sio hawa wachumia tumbo,

Mosi, astaafishwe for the public interests

Pili, afunguliwe mashtaka maana tuhuma zake zinathibitika vizuri tu.

Haya yote yana mwisho.
Huu ndio mfumo wa maccm, kulindana kwa hali na mali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa Viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:
  1. Amemteua Ndugu Said Othman Yakubu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Yakubu alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  2. Amemteua Ndugu Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
    Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Ndugu Msigwa alikuwa Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali. Nafasi
    iliyoachwa wazi ya Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali itatangazwa baadae.
MAKATIBU TAWALA MKOA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Abdallah Mohamed Malela, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Badala yake amemteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huu, Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
  2. Amemteua Ndugu Mohamed Jumanne Gombati kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gombati alikuwa Mkurugenzi Msaidizi
    Sehemu ya Maafisa Waandamizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
WAKUU WA TAASISI
  1. Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais - Tume ya Mipango.
  2. Amemteua Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
    Anachukua nafasi ya Mhandisi Peter R. Ulanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  3. Amemteua Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyamo - Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  4. Amemteua Dkt. Erasmus Fabian Kipesha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).
WAKUU WA WILAYA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Hanafi Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini na badala yake amemteua Bi. Mwanahamisi Mkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mkunda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
  2. Amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Mariam Chaurembo atapangiwa kazi nyingine.
WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI (MA -DED)
  1. Amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo. Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine.
  2. Ametengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Ndugu Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kafunda alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali.
  3. Amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.
KATIBU TAWALA WILAYA
Amemteua Ndugu Francis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya
(DAS) ya Namtumbo. Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki - Kilindi Handeni.

Katibu Mkuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa siku ya Jumanne saa sita mchana Ikulu, Dar es Salaam.
View attachment 2759138
View attachment 2759139
View attachment 2759157
Habari wakuu? Ivi hapo kwenye Uteuzi wa Dr. Stephen Isaac Mwakajumilo imekaaje hii? Maana Dr Stephen ni mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Mbeya! Na Sasa ameteuliwa kuwa DC tena.
 
This is the huge Public deceiving ( shame kwa SHH), ivi kweli mtu kama Maharage kaharibu sehemu then anateuliwa tena sehemu kweli? Kweli jameni?

Kwamba kwa watanzania zaidi ya 20million wenye uwezo na sifa hawaonekani mpaka aliyeharibu point A kuhamishiwa point B kweli? Kweli SHH?

This proves the fact kwamba , Maharage alitumwa kukwapua na kahamishiwa TTCL akaharibu then aje na wazo la kubinafsisha, CCM ni zaidi ya ukoo wa Panya.

Huyu mwamba yangefanyika mawili kama angekuwa kwenye nchi zenye viongozi na uongozi, sio hawa wachumia tumbo,

Mosi, astaafishwe for the public interests

Pili, afunguliwe mashtaka maana tuhuma zake zinathibitika vizuri tu.

Haya yote yana mwisho.
Kazi maalumu!
 
Hii nchi mafisadi na wasio na elimu wala vipaji vyovyote ambao wamepata kazi kwenye system huwa hawana wasiwasi kabisa, kwasababu wanajua hata wakiharibu kazi au kuiba kitakachofanyika ni kuwahamishia kwenye sekta nyingine yenye maslahi kama yale au zaidi kabisa.

Mtu kama Maharage atasaidia nini TTCL ikiwa huku kwingine amefeli au ndio maswala ya trying&error system.?
Awesome mambo ya telecommunication na Ana utaalam huo
Ngoja tuone ata perform vp

Ova
 
Walimuona chuma JPM chizi sasa wanarudi kwenye ramani zake. Mwenyekiti bodi ya Tanesco kapelekwa Meja Jenerali! Hii nchi ukichekacheka utashtuka hata wewe umeuzwa.
Kenyatta aliona mbali..siku ya mazishi alimuonya huyo mama kuwa tembelea njia hii hii aliyochonga jamaa..mother akaanza kuchonga njia yake kwa kiburi na majivuno..imeishia bondeni.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo TTCL ndo imepelekewa mtu incompétent. Yaani mtu kaharibu Tanesco anapelekwa kuwa mkurugenzi shirika lingine.Samia kweli anatuchezea akili.Sema na sisi sijui namna gani vipi.Maana tatizo la umeme tu,lazima tungeandamana.
Ni mtaalam wa mambo ya telecomuication Vicky

Ova
 
Back
Top Bottom