Maharage Chande aondolewa TANESCO, apelekwa TTCL. Gerson Msigwa awa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo
Wizara ya nishati ilifanya kazi vizuri chini ya Mhongo na kakemani, hawa wengine ni viazi tu.
 
Ni miongoni mwa akina mama ninaowakubali sana hapa jukwaani kwa michango unayotoa na kuchangia ila kwa hili naona kabisa kuwa unaelekezwa na nafsi kuliko ukweli ulivyo japo haijabadili muono wangu kwako

Wengi inawezekana ni kwa kuangalia nasaba za kiimani kwa jina lake bila kuangalia utendaji wake kuanzia mwanzo mpaka hapo pa kupewa ttcl na hata alipotokea pale tanesco wabaya wanaangalia ukatikaji wa umeme ktk msimu huu(kuna sbb nyingi ambazo zipo nje ya uwezo wake)ila pale kafanya makubwa ya kukumbukwa na kusifiwa kama alivyofanya kwenye mashirika na taasisi nyingine za kiserikali na binafsi alizopitia ktk safari yake ya kitendaji
Mkuu naona kila anaehoji utendaji wa Maharage unamuona kama hajafikiria vizuri. Okay, tuchukulie kwamba sisi tunaosema hajaifanyia kitu cha maana TANESCO, wewe unaweza kutueleza ni lipi la maana alilofanya hapo TANESCO..?

Ama unasukumwa na hisia tu.
 
Afadhali kirusi kimetoka TANESCO!
Hakuna Kirusi chochote Pale Tanesco zaidi ya wana ccM wenye nguvu,na walafi waliokita mizizi yako.Hapo kutakaa sawa siku Ccm ikitoka Madarakani.Mafisadi Makubwa ya Ccm ya enzi na enzi huwa yamejificha kwenye Taasisi nyeti kama hii ya Umeme mana wanajua huko kuna ulaji wa Maishaa.
 
𝐒𝐞𝐦𝐚 𝐭𝐮𝐮 𝐤𝐮𝐧𝐚 𝐛𝐚𝐚𝐝𝐡𝐢 𝐲𝐚 𝐯𝐢𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐢 𝐮𝐭𝐞𝐧𝐝𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐚𝐳𝐢 𝐰𝐚𝐨 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐡𝐚𝐭𝐚 𝐰𝐚𝐤𝐢𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐯𝐢𝐬𝐢𝐯𝐲𝐨 𝐤𝐰𝐚𝐨 𝐧𝐢 𝐬𝐚𝐰𝐚 𝐭𝐮𝐮. 𝐋𝐚𝐛𝐝𝐚🤫🤔 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐛𝐚𝐝𝐢𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐡𝐚𝐲𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐞𝐮𝐥𝐢𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐚𝐳𝐢𝐟𝐚𝐧𝐲𝐢𝐚 𝐯𝐲𝐞𝐦𝐚 𝐧𝐚𝐟𝐚𝐬𝐢 𝐳𝐚𝐨
Tatizo la Tanesco linajulikana mkuu, issue siyo watendaji.. issue ni vyanzo vya kueleweka vya kuzalisha umeme.
 
Mkuu naona kila anaehoji utendaji wa Maharage unamuona kama hajafikiria vizuri. Okay, tuchukulie kwamba sisi tunaosema hajaifanyia kitu cha maana TANESCO, wewe unaweza kutueleza ni lipi la maana alilofanya hapo TANESCO..?

Ama unasukumwa na hisia tu.
Bila kusigana nawe nakubali ndo mazoea yetu kuwa tukiulizwa swali badala ya kujibu nasi huwa tunauliza .......mimi nimeomba tutajiwe hujuma,ubadhirifu na alichoshindwa Maharage ili kukazia tuhuma zetu kwake
Pia ieleweke hakuna aliehoji hata mmoja kuhusu utendaji wake ila wengi wanatoa shutuma bila kueleza tuhuma kiasi nikiongozwa na hizo
ulizosema hisia zangu naona si sawa
 
Naona ziara ya mtwara kwa mama ilikuwa na lengo la kufyeka watu
 
Biteko kapewa jumba bovu litamuangukia tu na kumchafua. Ukweli ni kwamba bongo haizalishi umeme wa kutosha kukidhi mahitaji, hata waziri akiwa malaika toka mbinguni kama vyanzo ni vile vile mgao utaendelea tu.
 
Naona sasa rasmi Salim Kikeke anaingia kwenye nafasi ya Gerson Msigwa
 
Tulisema ni vigumu shamba boy (Dotto) Naibu Waziri Mkuu akae na Mtoto wa Mjini (Maharage). Ilikuwa lazima mmoja apishe na Kwa mazingira ya Sasa , Mtoto wa Mjini alikuwa lazimaa aende. TAIFA linapangwa upya
Ni kweli. Huwezi kuweka divai mpya ndani ya kasiki lililochakaa. Ikianza kuumuka kasiki litapasuka.
 
Ukizoea kushinda na njaa, siku ukipata mlo mmoja unashukuru.
 
Back
Top Bottom