Maisha Kitendawili: Ni sahihi IGP Mstaafu kuwa Mkuu wa Mkoa, kama ilivyo sasa kwa Sirro?

Maisha Kitendawili: Ni sahihi IGP Mstaafu kuwa Mkuu wa Mkoa, kama ilivyo sasa kwa Sirro?

Jakaya Kikwete anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ?
Anaweza. Na anaweza kukataa kama ataona ni udhalilishaji. Raia yeyote anaweza kuteuliwa katika nafasi yeyote isipokuwa kuna wachache kama CAG ambao hawaruhusiwi kuteuliwa nafasi nyingine ya utumishi mpaka baada ya kupita muda fulani baada ya kutoka kwenye nafasi yake. Na kila raia ana haki ya kukataa uteuzi. Hata Sirro anaweza kukataa uteuzi kama hajaridhika nao.

Amandla...
 
Wambura akienda ziara Kigoma, nani atampigia Salute mwenzake?
 
Kwa Sirro kakosea watu wa protocol watamwambia
Hata hajakosea na nina imani kwa level ile wanajadili na mteule kabla, mara nyingi kutokana na unyeti wa mkoa, mpakani aweza kumuomba amsaidie kwa kazi maalum kupitia uzoefu fulani na akakubali
 
Wambura akienda ziara Kigoma, nani atampigia Salute mwenzake?
Kawaida viongozi wenye cheo fanana wakiwa na uniform wote wanapiga saluti, ikiwa mmoja katika sare, Mwingine (mstaafu) kavaa kiraia atabana mikono tu badala ya salute, hiyo haiondoi hadhi ya cheo chake
 
Kwa Sirro kakosea watu wa protocol watamwambia
Yupo jamaa alikuwa mkuu wa takukuru nchi nzima somebody Mbungo (mtanisaidia kama nimekosea jina) aliwahi kuondolewa na kupewa uRC ama uRAS (wazee wa kumbukumbu mtanisaidia).
 
Hapana IGP sio equivalent ya CDF. Labda kama Major General hata Luten General sidhani. Swali Major General wapo walioteuliwa kuwa wakuu wa mikoa ?
MAJOR General Tumainel Kiwelu, Herman Lupogo, Silas Mayunga, Mathew Luhanga nk, pia hata makanali Nsa Kaisi, Anatory Tarimo nk
 
Ni kweli kwamba Kazi ni Kazi tu ili mradi mkono uende kinywani, lakini Je inawezekanaje aliyekuwa IGP akawe RC?

Soma Pia: UTEUZI: Balozi Simon Sirro ateuliwa kuwa RC wa Kigoma, Kenan Kihongosi kuwa RC wa Arusha. TRC yapata Mkurugenzi Mpya

Katika uteuzi ulifanyika Usiku huu Balozi Simon Sirro kapelekwa Kigoma kuwa Mkuu wa Mkoa.

Toa maoni yako
Vitu vingine vipo nje ya uwezo wako. Wakati mwingine teuzi zina yake kwa maslahi mapana ya nchi au maslahi ya aliyemteua
 
Anaweza. Na anaweza kukataa kama ataona ni udhalilishaji. Raia yeyote anaweza kuteuliwa katika nafasi yeyote isipokuwa kuna wachache kama CAG ambao hawaruhusiwi kuteuliwa nafasi nyingine ya utumishi mpaka baada ya kupita muda fulani baada ya kutoka kwenye nafasi yake. Na kila raia ana haki ya kukataa uteuzi. Hata Sirro anaweza kukataa uteuzi kama hajaridhika nao.

Amandla...
Hata DGIS haruhusiwi kuteuliwa kwenye nafasi yoyote baada ya Kutoka hio Position
 
Mtu kashika nafasi ya juu katika jeshi leo unamleta mkoani aanze kuhamasisha michango za mbio mwenge, serious kamanda silo naye akikubali teuzi atakuwa ajielewi
 
Ni kitendawili haswaaaa lkn osha sahani yako chakula bado kipo
 
Back
Top Bottom