Maisha Kitendawili: Ni sahihi IGP Mstaafu kuwa Mkuu wa Mkoa, kama ilivyo sasa kwa Sirro?

Maisha Kitendawili: Ni sahihi IGP Mstaafu kuwa Mkuu wa Mkoa, kama ilivyo sasa kwa Sirro?

Kutoheshimiwa kwa itifaki na katiba ya nchi kutodhibiti mamlaka ya Urais kunasababisha kufanyika mambo kienyeji tu.Na yeye akiondoka madarakani ateuliwe kuwa DC wa Manyovu.
 
Mmesahau yule mkuu wa mkoa wa songwe? Utoke kuwa wa kitaifa ukawe wa kimkoa hiyo ni demotion badala ya promotion. Kwa mtindo huu Rais mstaafu anaweza kuteuliwa mbunge kisha kulambishwa uwaziri!!
 
Soon tutasikia mpango nae kateuliwa kuwa katibu wa kata
 
Kwa Sirro kakosea watu wa protocol watamwambia
Kakosea kwa Sirro kama Sirro au kwa Sirro kama mstaafu? Lazima ufahamu kuna ngazi fulani za kijeshi ukishafikia basi sheria zinaruhusu kuwa Kiongozi wa umma na ndo maana kuna viongozi mbalimbali wa kijeshi wamepata kuwa wakuu wa mikoa! Na hata yule Wambura leo anaweza kuteuliwa kuwa RC au DC, na protokali zinaruhusu!
 
Aggrey mwanri aliwahi kua naibu waziri wa maji kipindi Cha kikwete na badae akaja kua mkuu wa mkoa wa tabora kipindi Cha magufuli.
Pia amosi makala kabla ya kuwa RC aliwahi kua mbunge Jimbo Moja huko morogoro
Kiitifaki Mkuu wa Mkoa ni mkubwa kwa Naibu Waziri
 
IGP ukimpelela Jeshini ni sawa na Mkuu wa JKt.
Mkuu usipende kuvichukulia poa vyeo vya Polisi ikiwa hata hujui makubwa yaliyofanywa na Jeshi la Polisi katika nchi hii.
Ukifuatilia historia Mkuu wa Kwanza wa JKT alitokea Polisi akiwa na cheo cha Assistant Superintendent of Police (ASP) ambaye ni sawa na Captain wa TPDF, hali kadhalika Idara ya Usalama wa Taifa pia iliwahi kuongozwa na ASP wa Polisi.
 
Kakosea kwa Sirro kama Sirro au kwa Sirro kama mstaafu? Lazima ufahamu kuna ngazi fulani za kijeshi ukishafikia basi sheria zinaruhusu kuwa Kiongozi wa umma na ndo maana kuna viongozi mbalimbali wa kijeshi wamepata kuwa wakuu wa mikoa! Na hata yule Wambura leo anaweza kuteuliwa kuwa RC au DC, na protokali zinaruhusu!
HIlo neno 'kijeshi' unaelewa maana yake? Haluhusiani na polisi hivyo halifai kutumika kumuelezea polisi kwa sababu sio jeshi. Sema 'kipolisi'.
 
Mkuu usipende kuvichukulia poa vyeo vya Polisi ikiwa hata hujui makubwa yaliyofanywa na Jeshi la Polisi katika nchi hii.
Ukifuatilia historia Mkuu wa Kwanza wa JKT alitokea Polisi akiwa na cheo cha Assistant Superintendent of Police (ASP) ambaye ni sawa na Captain wa TPDF, hali kadhalika Idara ya Usalama wa Taifa pia iliwahi kuongozwa na ASP wa Polisi.
JKT ya mwanzo haikuwa sehemu ya Jeshi, unaelewa hilo? Ilikuwa chini ya wizara ya utamaduni. Ilikuwa kama sehemu ya kuwakutanisha vijana wa wakati huo.

Huo mlinganisho wa vyeo wa taasisi zisizofanana umeutoa wapi?
 
Mkuu usipende kuvichukulia poa vyeo vya Polisi ikiwa hata hujui makubwa yaliyofanywa na Jeshi la Polisi katika nchi hii.
Ukifuatilia historia Mkuu wa Kwanza wa JKT alitokea Polisi akiwa na cheo cha Assistant Superintendent of Police (ASP) ambaye ni sawa na Captain wa TPDF, hali kadhalika Idara ya Usalama wa Taifa pia iliwahi kuongozwa na ASP wa Polisi.
Mkuu ndiyo uhalisia huo siyo kuvuchukulia poa, Una jua Jumanne Murilo kwa cheo chake ni mdogo kwa Brigedia General?. IGP ni mdogo ata kwa Luteni General wa JWTZ.
 
Kama hana kazi zake binafsi na alizaliwa kwaajili ya utumishi wa umma tu inakucost nini wewe ,mbona kova ni kiongozi wa bakwata.

Uchochezi kwako imekuwa ni kazi pia hata ujinga kama huu unapita nao.

Leta sera zenu ni vipi mtabadirisha maisha ya WaTz waondookane na umaskini,maradhi na ujinga siyo uchochezi.
 
Ni kweli kwamba Kazi ni Kazi tu ili mradi mkono uende kinywani, lakini Je inawezekanaje aliyekuwa IGP akawe RC?

Soma Pia: UTEUZI: Balozi Simon Sirro ateuliwa kuwa RC wa Kigoma, Kenan Kihongosi kuwa RC wa Arusha. TRC yapata Mkurugenzi Mpya

Katika uteuzi ulifanyika Usiku huu Balozi Simon Sirro kapelekwa Kigoma kuwa Mkuu wa Mkoa.

Toa maoni yako
Ni aibu Sana, huyu jamaa itakuwa financialy hsyupo vzr, akaomba kupitia mlango wa nyuma, apewe kazi asife njaa,nchi hii ina vijana wengi wangeweza kupewa, hii kazi, kwanini apatiwe MTU tayari ana miaka 65,kafsnya utumishi for 40yrs, anakula pensheni, kitu gani kipya anapeleka,
Ndio maana, tunasema hivi vyeo vya RC, DC, ni vya kipuuzi, anaenda pale kuzeekea tu, Hana function maalum!
 
Back
Top Bottom