Majaribio ya treni ya umeme yafanyika

Majaribio ya treni ya umeme yafanyika

Kinachofanyiwa majaribio ni njia ya reli, mifumo yake (umeme, mawasiliano n.k), namna ya uendeshaji 'operations' n.k

Huitaji kujaribu treni yenyewe, sababu treni yenyewe hujaribiwa na watengenezaji...

Nikuulize tu swali moja, wewe kabla ya kununua gari Japan au kwingineko, huwa unapewa ulijaribu?

cc Ngalikihinja
Basi ungeandika heading inayoashiria kuwa kinachojaribiwa ni infrastructures ambazo zinabeba hicho kinachotembea kwenye hizo infrastructures..!!

By the way, hicho kichwa kinachooneka kinazijaribu hizo infrastructures ndo chenyewe kitakachotumika wakati ukifika?
 
Itapendeza kama umeme hautakuwa wa luku....
Nikija Dar, natumai itakuwa tayari niipande mpaka Kigoma nikumbUKE nostalgia ya reli ya kati miaka ileeeee...una safiri na waranti yaa uanafunzi...
Nipite Morogoro, kutoka Moro mpaka Kilosa ni viunga vya misitu ya Uluguru ya ukijani na ukungu wa kutosha, mara tunaingia Kilosa, hatukai sana tunaitafuta Kongwa, mara Dom hii hapa, nishuke niende Wimpy's nikapate msosi, nirudi na kushushia karanga za kuchemsha, tuitafute Manyoni, sijui yale marashi na sabuni za ulaya walikuwa wanatoa wapi wale wauzaji wa Manyoni, mara Honi ya treni ikilia unaliacha liaanze kuondoka ili ulikimbize na kudandia na ujione VanDamme, hapo tunaitafuta Itigi ni Mandhari ya kutosha huku umechungungulia dirisha maeneo ya mlangoni, na nakumbuka ikifika Tabora, unatakiwa uwe macho juu na mizigo yako maana hapo ni wezi wako juu ya treni inaeenda wananing'inia na kuchomoa mabegi,
aaahh naona hivyo vituo nimechanganya madawa....nitarudi nikiwa sober...
Mnapenda sana kutupaka shombo watu wa Mbokamanyema.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Treni ya umeme kwa nchi za wenzetu mbona zinaenda kasi kwetu kuna nini ebu chekini hii ya wenzetu huko nga'mboView attachment 2279512
Hii chombo inatembea asee acha utani, haiwezi kuwepo hapa kwetu hata kidogo.

Nimeona hapo ime_run 5600+km per hour ni muda mzuri sana, labda chuma kingekuwepo na kuonyeshwa kitu kama hii angetoa tamko moja tu machine inanunuliwa kama bombardier 😁!.
 
Kinachofanyiwa majaribio ni njia ya reli, mifumo yake (umeme, mawasiliano n.k), namna ya uendeshaji 'operations' n.k

Huitaji kujaribu treni yenyewe, sababu treni yenyewe hujaribiwa na watengenezaji...

Nikuulize tu swali moja, wewe kabla ya kununua gari Japan au kwingineko, huwa unapewa ulijaribu?

cc Ngalikihinja
Mbona mnabishana na wakati, wakati ndio msema kweli wacha tuone ikiwa operational vinakuja vichwa vya aina gani.
 
Hii ndio iliyofanyiwa majaribio mbona kama itakuja ya hivyo tumepigwa pakubwa naona kama imepitwa na wakatiView attachment 2279510
Hakuna kupigwa. Hicho kichwa ndicho sahihi kwa speed ya 160km/hr labda waongeze nakshi tu.

Reli yetu ingawa ni SGR (1.435m) ina design capacity hiyo ya 160km/hr sawa na ile ya Afrika ya Kusini (cape gauge: 1.067m) ambayo ni nyembamba zaidi. Bila shaka viwango vya kihandisi kuhusiana na vitu kama kona, msingi, miinuko, nishati, n.k. vitakuwa pungufu katika sgr yetu. Bado tumeendelea; tumetoka mbali, you know.

Hiyo emu inayowavutia wadau ni ya speed kuanzia 200 hadi 250km/hr (kiwango cha kimataifa. Tusikate tamaa. Tutafikia hata ile ya 450km/hr kama China na Japan. Polepole ndio mwendo. We’re on the right track.
 
Kichwa ndiyo nini? Sema*engine"
Mambo mengine mnalazimisha bure
Engine kama engine uwezi kuiweka kwenye reli ikavuta mabehewa ya abiria au mizigo, engine inawekwa kwenye super structure ya Locomotive hicho ndicho kinaitwa kichwa cha Train -hivyo alive sema ni kichwa cha Train yuko sahihi kabisa. Kitu kingine,kwenye vichwa vya train za umeme havina engine, kuna traction motors na speed control systems, basi.
 
Itapendeza kama umeme hautakuwa wa luku....
Nikija Dar, natumai itakuwa tayari niipande mpaka Kigoma nikumbUKE nostalgia ya reli ya kati miaka ileeeee...una safiri na waranti yaa uanafunzi...
Nipite Morogoro, kutoka Moro mpaka Kilosa ni viunga vya misitu ya Uluguru ya ukijani na ukungu wa kutosha, mara tunaingia Kilosa, hatukai sana tunaitafuta Kongwa, mara Dom hii hapa, nishuke niende Wimpy's nikapate msosi, nirudi na kushushia karanga za kuchemsha, tuitafute Manyoni, sijui yale marashi na sabuni za ulaya walikuwa wanatoa wapi wale wauzaji wa Manyoni, mara Honi ya treni ikilia unaliacha liaanze kuondoka ili ulikimbize na kudandia na ujione VanDamme, hapo tunaitafuta Itigi ni Mandhari ya kutosha huku umechungungulia dirisha maeneo ya mlangoni, na nakumbuka ikifika Tabora, unatakiwa uwe macho juu na mizigo yako maana hapo ni wezi wako juu ya treni inaeenda wananing'inia na kuchomoa mabegi,
aaah naona nimechanganya madawa kwenye vituo nitarudi nikiwa sober....
 
By the way, hicho kichwa kinachooneka kinazijaribu hizo infrastructures ndo chenyewe kitakachotumika wakati ukifika?

Hicho kichwa kimezalishwa Austria...

Vichwa na treni(mabehewa) vitavyotumika baadaye vitatoka Korea Kusini, China...

Taarifa zipo mitandaoni hata ukigoogle utapata, na hapa JF zipo pia

Thread 'Ununuzi wa injini na behewa za abiria na mizigo kwa matumizi ya reli ya kisasa - SGR' Ununuzi wa injini na behewa za abiria na mizigo kwa matumizi ya reli ya kisasa - SGR
 
Kinachofanyiwa majaribio ni njia ya reli, mifumo yake (umeme, mawasiliano n.k), namna ya uendeshaji 'operations' n.k

Huitaji kujaribu treni yenyewe, sababu treni yenyewe hujaribiwa na watengenezaji...

Nikuulize tu swali moja, wewe kabla ya kununua gari Japan au kwingineko, huwa unapewa ulijaribu?

cc Ngalikihinja
Nimependa jibu lako huko juu katika mistari miwili ya mwanzo; lakini swali ulilouliza kwenye huo mstari wa tatu hauhusiani kabisa na kinachojadiliwa hapa.
 
Chukulia wew ndio dereva wa hiyo treni na ndio mara ta kwanza unafanya majaribio, ungetembea speed ngap
Spidi inayoendana na viwango vinavyotarajiwa kwa treni hiyo; kwani hili nalo ni gumu kueleweka?
 
Train ya SGR Tanzania ni ndoto kwani wenye malori mengi ndio wameshika serikali.
Lakini wangekua na huruma kidogo angalau ile ICD ya vigwaza ikakamilika ili kupunguza congestion barabara ya Kibaha/chalinze.
Sasa hivi ukitoka Mbezi Hadi chalinze utapishana na malori zaidi ya elfu mbili.
 
Back
Top Bottom