DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Unafahamu mazingira ambayo samaki kanda ya ziwa huwa wanauzwa? Sijaona samaki wakiuzwa sehemu iliyofungwa, labda kwenye viwanda vya samaki. Maeneo yote samaki huuzwa maeneo ya wazi, na mara nyingi ni kwenye fukwe za ziwa.
Samaki anayenunuliwa fresh kwa ajili ya kwenda kuliwa, unamwekea dawa ya kuhifadhi ili iweje........bei ya hao samaki ni kiasi gani hadi ugharamike kununua kemikali inayouzwa pesa nyingi na ambayo huwezi kuipata kirahisi.
 
Zebaki migodini ndo Chanzo.

Pwani hutumia barafu hizo hizo, na maji hayo hayo, dawa hizo hizo.

Kumbuka pia samaki wa ziwa Victoria hutumika Nchi nzima, hujiulizi why tatzo kubwa libaki Kanda ya ziwa?

SERIKALI=SIRI KALI.

Ameeen
 
Aisee! Sasa imagine marehemu kafariki na magonjwa ya kuambukiza, hayo maji ya kumuoshea yanakuwa salama kweli hata tukiachilia mbali saratani.
 
Hatuna Wanasayansi na Watafiti? Hivi mercury migodini na maji taka ya mortuary kipi kinasababisha cansa zaidi. Mawakala wa hazadous waste ndio wanauza hayo maji? NEMC na Mkemia Mkuu mpo?

 
Kwanza napenda ku declare interest, mie ni mtu wa mwanza tena pembezoni mwa ziwa victoria, kasumba yetu huwa hatuli samaki wa kuhifadhiwa kwenye majokofu, huwa tunapenda samaki fresh tena mzuri zaidi yule anayefiki sokoni akiwa bado yupo hai.
 
Kiufupi ni kwamba ukienda kununua samaki chagua duka lenye ma-nzi wengi ndio kuna samaki salama.

Ila unakuta duka la samaki lakini hakuna hata ka nzi kanakozengea maeneo hayo, seriously?

AKILI KUMKICHWA.
Hata butchers utakuta Amna nzi, Dawa hizo za kuhifadhia maiti wafanyabiashara hununua Kutoka Kwa wahuni na madaktari wasio waadilifu Mahospitalini.

Waganga maji ya maiti hununua pia Hospitali, SERIKALI ijiangalie.

Ameeen.
 
Suala la caricnogens bado kwa hapa Bongo halijaeleweka na wananchi wengi, hydrocarbon nyingi, baadhi ya halogen compounds hasa bromides pamoja na nicotine zinachangia sana kusababisha saratani.
 
Nafikiri mtoa hoja hajaiwakilisha vema ipo hivi sio maji ya kuoshea maiti bali dawa ya kuhifadhia maiti zisioze zinapokuwa kwenye mafriji na kushafirisha maiti sio maji ni dawa inayoitwa formalin sio maji na dawa hii huwadunga samaki ili wasioze haraka wakati wa kuwasafirishwa hili ndio tatizo kubwa hasa kwa mikoa ambayo husafirishiwa samaki kama Dar, Arusha, Moshi, Tanga sio sana wao hula sana samaki bahari, Dodoma etc. hili ndio tatizo na sio maji yakuoshea maiti.
 
Wait, hayo maji wanayatumiaje kwa samaki?? Na yanaletaje kansa?
Ninachoweza kukwambia ni kuwa...tuna viongozi wenye midomo isiyo TAHIRIWA.
makamu wa rais hawezi kufunua domo na kusema neno gumu kiasi hicho bila kupima matokeo hasi.
Ameua biashara ya masikini bure.

Kama ni kweli, ameshindwa kufanya msako kimya kimya na kuua hili soo?

Ooh nchi yangu inaongozwa na Punda wa Balaamu yule mwaguzi...pua pua
 
Hili limeshawakilishwa kama tatizo Serikali inabidi ifuatilie na kuchunguza ukweli wake kama ni kweli hatua kali sana zichukuliwe na kuacha siasa kwenye afya za watu.
 
Jabali la kisiasa linalojaza mikutano BILA malori ya CHAMA na serikali limewashika pabaya!!!

Huyo Ndio FDR hata wafanyaje!!

Tunakazia HIVI;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba Mpya"
 
Hadi hali ifikie kuwa mbaya kiasi hicho, mabwana na mabibi afya wanakuwa wapi kufuatilia?
Au nchi hii ni kubwa kuliko uwezo wa viongozi na watendaji husika?
Ni aibu!
Hahahahaaaa.. wananchi wanalia, Makamu wa Rais naye analia, sasa sijui nani wa kuchukua hatua! Only in Tz...kazi iendelee.
 
Hizo samaki unazo ziona ferry pale au soko la ilogonzara kwenye firiji zina subiria wateja wa Dar es salam wafungiwe kwenye ndoa wa ondoke na basi au na ndege watu wa mwanza wengi hawawezi kutumia pesa yao kununua samaki sato/sangala aliohifadhiwa kwenye firiji kwa sh 25k au 30k

wakati kuna visoko vya samaki fresh mitaani jilani na makazi yao kwa sh 2k hadi 5k kwa hao samaki wakubwa ni kwa wageni wasio jua samaki wa ziwa vic kwahiyo hiyo salatani ingetokea kwingine sio mwz tena.
 
Samaki anayenunuliwa fresh kwa ajili ya kwenda kuliwa, unamwekea dawa ya kuhifadhi ili iweje........bei ya hao samaki ni kiasi gani hadi ugharamike kununua kemikali inayouzwa pesa nyingi na ambayo huwezi kuipata kirahisi.
Formalin sio ghali kiasi hicho tusi li-underrate hata kidogo uchunguzi lazima ufanyike kutafuta ukweli kama upo we should brush it over.
 
Hii kitu kama ni kweli tutakufa wengi,wapo baadhi ya watu pindi wakila samaki familia yote inaona madhara kwenye ngozi,majipu yasiyoeleweka,pengine najaribu kukuelewa pamoja tatizo la Kansas kuwa kubwa Kwa baadhi ya maeneo.
Kuna jambo linatafutwa Ili kuhujumu Uchumi Kanda ya ziwa.

Mamlaka zimewanunia. Mwisho wake u karibu.
Ameeen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…