Majirani wazuia jeneza la kijana kuingia kwa wazazi wake

Majirani wazuia jeneza la kijana kuingia kwa wazazi wake

Page-3-BEDA-780x470.jpg
Wananchi wa Mtaa wa Maganga, maeneo ya Nurulyakini, Temeke, Dar es Salaam wamezuia mwili wa marehemu Pius Beda maarufu Stahimili (32) kuingia nyumbani kwa wazazi wake, kuonesha hasira zao kwamba wazazi hao walishindwa kumhudumia alipokuwa hai.

Kijana huyo alikutwa amekufa kwa kujinyonga nyumbani kwa jirani alikokuwa anasaidiwa mahala pa kulala.

Wakizungumzia mkasa huo Dar es Salaam jana, majirani wa Stahimili walisema amekuwa akiishi maisha magumu kiasi kwamba hata alipotafuta msaada kwa baba na mama yake wa kambo aliokuwa anaishi nao hakusaidiwa.

Walisema sababu ya kuzuia jeneza lililokuwa limebeba mwili huo ni kwa kuwa wazazi wake walishindwa kumsaidia pale alipohitaji msaada kiasi cha majirani kuingia jukumu la kumsaidia mahali pa kuishi ingawa bado chakula pia hakuwa anakipata.

“Tulizuia maiti isiingie ndani kwa wazazi wake kwa sababu tulikuwa tunajua maisha anayoishi. Msaada wake mkubwa ulitoka kwa majirani wakati wazazi wake wana uwezo, sasa tukasema kama hawakumsaidia mwanzo watuachie wenyewe,” alisema mmoja wa majirani zake ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Jirani mwingine ambaye wazazi wake walimpa hifadhi kijana huyo alisema Stahimili ambaye alikuwa pia na matatizo ya kiafya, alikuwa na mgogoro na familia yake na alipokuwa akijaribu kutafuta suluhisho hakusikilizwa.

Kwa mujibu wa jirani huyo, kijana alikwenda nyumbani kwao kuomba msamaha ili kuweka mambo sawa ila mambo yalishindikana.

Alisema alikuwa akifanya kazi viwandani baadaye kazi iliisha kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya (kupoteza fahamu mithili ya kifafa), baadaye alikosa fedha za kula na kulipa kodi akaamua kurudi nyumbani kwao kuomba msaada ila alielezwa hana nafasi kwao labda aende kwa baba yake mdogo.

Baada ya vurugu za wananchi wa eneo hilo la Temeke Maganga kuzuia maiti, iliwekwa nje ya jumba moja bovu alikolazimika kuishi, jirani na nyumbani kwao na kuagwa.

Lakini wazee wa busara na viongozi wa dini walituliza hali, kukawa tulivu. Wakati wa kupeleka mwili kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Wailes, Chang’ombe wananchi walizuia pia asibebwe na gari lililokuwa limekodiwa na wao wakaamua kuubeba wenyewe.

Baba wa kijana huyo, Beda Malya alikataa kuzungumzia sakata hilo huku mama yake mzazi, Segolina Alphonce aliyekuwa akiishi Moshi, Kilimanjaro na ambaye alikuja kwa ajili ya msiba wa mtoto wake akisema mwanaye alikuwa akiishi na baba yake tangu akiwa na umri wa miaka saba na hakujua lolote linaloendelea ila anamwachia Mungu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Temeke kwa Maganga, Jaffar Shoo alisema sio vizuri kutoa hukumu kwa wazazi wa kijana huyo na kwamba watafanya uchunguzi wa kile kinachoelezwa kama ni kweli ila anachoamini kijana huyo ni mtu mzima na hakuna aliyemlazimisha kujiua isipokuwa siku yake imefika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema atafuatilia sakata hilo kujua kinachoendelea.

HABARI LEO
Kwa wachaga hawana utu hata wenyewe wanalijua Ilo Bali Ni pesa mbele tu. Yaani cheki wale wachaga masikini huwa rafiki zao Ni makabila mengine. Huwa hawaendi kwao likizo Mana kudhihakiwa na kutumwa Kama watoto mwanzo mwisho. Wewe Ni me Mara utasikia mdogo wako wa kike anakuambia nioshee Ilo benzi langu dogo.
Wewe ndiye unayetumwa Kama mtt.

Na ndio Mana ukioa uchagani uwe na hela halafu kwao hawana hela ndio utalijua jiji lazima tu utajenga kwao,uwape mtaji wadogo zake ama wakubwa whether you like or not ukikataa tu utasikia majambazi wamevamia umeuwa.

Kuna wachaga wanajenga Ila wanapanga wake zao wasijue Kama tayari wameshajenga. So Ilo mie silishangai.

Wachaga Wana hela wafanyabiashara wanawakimbilia wa Asia ama waarabu Ni wasomi wao ndio wanaomiliki miradi mikubwa hapa Tanzania. Ndio wasomi wengi hata huko vyuoni na taasisi nyeti serikalini hata Delta binafsi. Tunao Neurosurgeons Kama Tisa nadhani wengi wa hao Tisa tanzania nzima Ni wachaga.kiufupi wanafanya biashara ikiwa damuni sio Kama makabila mengine wanafanya Kama option. Yaani mchaga na pesa/biashara Ni sawa na mmasai na ng'ombe.

Lile la kwanza watakataa na watanishambulia mana Ni ukweli na ukweli kawaida ya ubongo inaukataa na unauma Ila hili la mwisho watafurahia na Mana nimewajaza ego ego yao yaani nimewalisha ikashiba
 
Una akili mgando sana fala sana, wachaga ni funza gani
 
32 years jamani si umri wa kua dependent, hata ikitokea ukakosa msaada si ku lalamika.
Maisha ni kupambana.
 
32 Years ?

Alexander the Great had a profound effect on world history. His conquests covered the entire known world at the time, and he was responsible for the spread of Greek culture throughout the ancient world. In Babylon in 323 BC, Alexander died when he was nearly 33 years old.

RIP kijana..., anyway si vema kuleta lawama kwa mtu yoyote yule..., In life we make our own beds hence we should be ready to lie on them....
Umejaribu kufananisha vitu viwili tofauti kabisa,yaani ni kama unajaribu kuaminisha watu kwamba usiku na mchana ni sawasawa
 
Hakuna Mtu ninaemchukia hapa duniani kama muabudu hela, anamtosa yeyote, Nina maana yeyote yule ili mradi apitiwe angalau tu na harufu ya hela. Hata asipoipata.kwa ujumla si binadamu kabisa...
 
Tatizo kubwa hapo ni roho mbaya ya mama wa kambo. Daima Mama wa kambo sio Mama
Asilimia kubwa wengi wana roho mbaya japo hata mimi siku moja naweza jikuta mama wakambo.Ila wapo wazuri japo wachache sana.
 
Back
Top Bottom