Majirani wazuia jeneza la kijana kuingia kwa wazazi wake

Majirani wazuia jeneza la kijana kuingia kwa wazazi wake

Unamaanisha nini ?

Nimejibu comment ya mtu hapo juu huhusu huyu mtoto kutelekezwa nikauliza 32 years ni mtoto....

Sasa kama mtu at 32 alisha-conquer the world ije kuwa mtu at 32 kupambana na msalaba wake ? au wewe ndio hauelewi !!!!
Mkuu nimekuelewa vizuri tu na kikawaida haifai kwa mtu wa miaka 32 kuwa katika hali ya kutegemea wazazi wake lakini maana ya comment yangu ni kwamba mfano wako umeenda mbali sana.

Kwanini nimesema hivo?

Hatukuwahi kufanana na hao watu(whites) hadi hii leo ndyo maana unaona tuna viongozi wetu wamesoma haswa lakini unaona namna gani nao wanavyopelekeshwa na hao watu weupe.

Labda ungejaribu kufananisha mtu wa umri huo kikawaida kwa hapa kwetu bongo na pengine Afrika nzima kwamba anakuwa na chochote cha kujishughulisha,lakini mbali na kuwa na kitu cha kujishughulisha mtu wa miaka 32 kwa hapa Tanzania anakuwa na familia kabisa ikimaanisha kwamba anatakiwa ategemewe.
 
Am all kwa kutoa msaada lakini ni msaada sio obligation..., mfano mzazi ana wajibu wa kusomesha, kulisha na kutoa basic needs mpaka mtoto anapokuwa mtu mzima..., zaidi ya hapo sio wajibu tena bali ni ubinadamu...

Ndio haya mambo watoto wanakuombea ufe ili warithi yaani mali sio yako tena ni yao / yenu...

Mwisho wa siku ni appreciation which matters; hujaona mtu anasomesha mtoto wa mtaani alafu huyo mtoto anamkumbuka na kumjali maisha yake yote (appreciation) lakini mtoto wake binafsi mtu kauza mpaka shamba ili mtoto asome ila baadae mtoto analaumu hakupelekwa english medium kama mtoto wa jirani ?
Mkuu upo sahihi, ni kama ile kesi ya mkoani Mwanza iliyopo viral kwenye mitandao. Mama kwa kushirikiana na wanaye wanne kumuua baba yao mzazi kwa kumchija!
 
Mkuu nimekuelewa vizuri tu na kikawaida haifai kwa mtu wa miaka 32 kuwa katika hali ya kutegemea wazazi wake lakini maana ya comment yangu ni kwamba mfano wako umeenda mbali sana.

Kwanini nimesema hivo?

Hatukuwahi kufanana na hao watu(whites) hadi hii leo ndyo maana unaona tuna viongozi wetu wamesoma haswa lakini unaona namna gani nao wanavyopelekeshwa na hao watu weupe.

Labda ungejaribu kufananisha mtu wa umri huo kikawaida kwa hapa kwetu bongo na pengine Afrika nzima kwamba anakuwa na chochote cha kujishughulisha,lakini mbali na kuwa na kitu cha kujishughulisha mtu wa miaka 32 kwa hapa Tanzania anakuwa na familia kabisa ikimaanisha kwamba anatakiwa ategemewe.
Binafsi fikra zangu zipo tofauti na lawama zangu zinaenda tofauti Conficus alisema “In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.

Sasa kwa nchi ambayo watu wanalamba asali na kula keki ya taifa hadi makombo; kizazi kijacho kitakuwa hata hakina pension; vijana ambao ni nguvu kazi sio kwamba ni wazembe bali hakuna kazi zenye ujira... kwahio uzeeni watakuwa hawana pension, kijiji wala pa kukimbilia...

Kijana ambae ametoka Chuo baada ya mzazi kuuza shamba lake anarudi bado ni tegemezi na kwa mzee wake ambae huenda na yeye hana hata pension na jua limeanza kuzama..., unadhani emotionally huyu kijana ambae amegeuka kuwa mzigo atajiona vipi, ukizingatia hata kumsaidia hawezi...

Individually mtu mmoja mmoja hatuwezi kulaumu mtu yoyote (sababu kila mtu atabeba msalaba wake) ila as a community we have failed maisha yetu sio sustainable na tunajenga kesho ngumu na hatari sana kuliko leo...

Tumeshindwa na tunashindwa kuweka misingi bora na endelevu tunajenga matabaka ya masikini wengi ambao ni nguvu kazi ambazo zingezalisha... tunazifundisha kuwa wachuuzi na omba omba na jawabu la matatizo yetu limekuwa ni kujiajiri...., na ajira hizo ndio Bahati nasibu, machinga / wachuuzi wa bidhaa kutoka ughaibuni....
 
32 years jamani si umri wa kua dependent, hata ikitokea ukakosa msaada si ku lalamika.
Maisha ni kupambana.
Watu wengi bana, mnajifanyaga much know sana, muombe sana Mungu wako asikupungukie kwa kila kitu
 
Unamaanisha nini ?

Nimejibu comment ya mtu hapo juu huhusu huyu mtoto kutelekezwa nikauliza 32 years ni mtoto....

Sasa kama mtu at 32 alisha-conquer the world ije kuwa mtu at 32 kupambana na msalaba wake ? au wewe ndio hauelewi !!!!
We we naona ni mpuuzi, Alexander the great alikuwa mtoto wa mfalme na kaachiwa ufalme akiwa na miaka 16+.
Ni sawa na mtu anayesema Mo in bilionea mwenye umri mdogo wakati kiuhalisia amerithi na alikuwa na foundation ya management kutoka kwa familia kuhusu biashara.
Btn Alexander alikuwa anaenda vitani na baba yake toka ni mdogo.
Sio wakati wote juhudi na akili vitakufanya ufanikiwe wakati na bahati ni part kubwa.
 
Mama wa kambo weng Wana roho mbaya sanaaaaa sijui wakoje yaani speaking from my very own experience
Nasemaga hivi wanangu ni sehemu ya mwili wangu sitaruhusu walelewe na mama wa kambo labda nife na nasemaga always nikifa wanangu waende orphanage tu kuliko kuishi na mama wa kambo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwahyo tukiachane nisivute binti mzuri tulizo la nafsi kisa hutaki watoto walelewe na mama wa kambo we kama uliolewa bila mtoto utaondoka bila mtoto
 
Page-3-BEDA-780x470.jpg
Wananchi wa Mtaa wa Maganga, maeneo ya Nurulyakini, Temeke, Dar es Salaam wamezuia mwili wa marehemu Pius Beda maarufu Stahimili (32) kuingia nyumbani kwa wazazi wake, kuonesha hasira zao kwamba wazazi hao walishindwa kumhudumia alipokuwa hai.

Kijana huyo alikutwa amekufa kwa kujinyonga nyumbani kwa jirani alikokuwa anasaidiwa mahala pa kulala.

Wakizungumzia mkasa huo Dar es Salaam jana, majirani wa Stahimili walisema amekuwa akiishi maisha magumu kiasi kwamba hata alipotafuta msaada kwa baba na mama yake wa kambo aliokuwa anaishi nao hakusaidiwa.

Walisema sababu ya kuzuia jeneza lililokuwa limebeba mwili huo ni kwa kuwa wazazi wake walishindwa kumsaidia pale alipohitaji msaada kiasi cha majirani kuingia jukumu la kumsaidia mahali pa kuishi ingawa bado chakula pia hakuwa anakipata.

“Tulizuia maiti isiingie ndani kwa wazazi wake kwa sababu tulikuwa tunajua maisha anayoishi. Msaada wake mkubwa ulitoka kwa majirani wakati wazazi wake wana uwezo, sasa tukasema kama hawakumsaidia mwanzo watuachie wenyewe,” alisema mmoja wa majirani zake ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Jirani mwingine ambaye wazazi wake walimpa hifadhi kijana huyo alisema Stahimili ambaye alikuwa pia na matatizo ya kiafya, alikuwa na mgogoro na familia yake na alipokuwa akijaribu kutafuta suluhisho hakusikilizwa.

Kwa mujibu wa jirani huyo, kijana alikwenda nyumbani kwao kuomba msamaha ili kuweka mambo sawa ila mambo yalishindikana.

Alisema alikuwa akifanya kazi viwandani baadaye kazi iliisha kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya (kupoteza fahamu mithili ya kifafa), baadaye alikosa fedha za kula na kulipa kodi akaamua kurudi nyumbani kwao kuomba msaada ila alielezwa hana nafasi kwao labda aende kwa baba yake mdogo.

Baada ya vurugu za wananchi wa eneo hilo la Temeke Maganga kuzuia maiti, iliwekwa nje ya jumba moja bovu alikolazimika kuishi, jirani na nyumbani kwao na kuagwa.

Lakini wazee wa busara na viongozi wa dini walituliza hali, kukawa tulivu. Wakati wa kupeleka mwili kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Wailes, Chang’ombe wananchi walizuia pia asibebwe na gari lililokuwa limekodiwa na wao wakaamua kuubeba wenyewe.

Baba wa kijana huyo, Beda Malya alikataa kuzungumzia sakata hilo huku mama yake mzazi, Segolina Alphonce aliyekuwa akiishi Moshi, Kilimanjaro na ambaye alikuja kwa ajili ya msiba wa mtoto wake akisema mwanaye alikuwa akiishi na baba yake tangu akiwa na umri wa miaka saba na hakujua lolote linaloendelea ila anamwachia Mungu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Temeke kwa Maganga, Jaffar Shoo alisema sio vizuri kutoa hukumu kwa wazazi wa kijana huyo na kwamba watafanya uchunguzi wa kile kinachoelezwa kama ni kweli ila anachoamini kijana huyo ni mtu mzima na hakuna aliyemlazimisha kujiua isipokuwa siku yake imefika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema atafuatilia sakata hilo kujua kinachoendelea.

HABARI LEO
Wachaga wana roho mbaya sana.
 
We we naona ni mpuuzi, Alexander the great alikuwa mtoto wa mfalme na kaachiwa ufalme akiwa na miaka 16+.
Ni sawa na mtu anayesema Mo in bilionea mwenye umri mdogo wakati kiuhalisia amerithi na alikuwa na foundation ya management kutoka kwa familia kuhusu biashara.
Btn Alexander alikuwa anaenda vitani na baba yake toka ni mdogo.
Sio wakati wote juhudi na akili vitakufanya ufanikiwe wakati bahati ni part kubwa.
Kwanini Baba yake ndio haku-conquer the world ? na ku-expand empire kama Alexander ?

Jaribu kuweka uwiano wa mambo..., hapa issue imekuja umri kwamba ni mtoto; kwahio jibu likaja kwamba at 32 unaweza / inawezekana mtu aka-achieve kiasi gani, sio kwamba watu wawe kama yeye...., bali ukiona hauna viatu kumbuka kuna wengine hawana hata miguu....

Issue hapa sio mafanikio issue ni kuangalia ni vipi watu walio at a disadvantage kuliko hata wewe wameweza kufanya makubwa zaidi;

Unaweza kulalamika una chongo na hauoni vizuri wakati kuna kina David Blunkett walizaliwa vipofu ila waliweza kuwa mpaka mawaziri..., au unasema hauma mbio kwahio unashindwa kucheza mpira wakati kuna kina Garrincha (certified kilema) ila alikuwa mpiga chenga duniani haijawahi kuona.....

Life is purely a matter of perspective.
 
Miaka 32 unalilia msaada kwa wazazi [emoji276]?,Dunia ina maajabu yake!,sisi wengine tulioanza kujipambania kuanzia miaka 16 sijui tulifeli wapi [emoji851]
 
mwanamke ana nguvu sana,haya yote yameletwa na mama wa kambo,angekuwa mwanaye angesema hana nafasi?
na mwanaume ukishikwa masikia utajazwa sumu mpaka umchukie mtoto
 
Miaka 32 unalilia msaada kwa wazazi [emoji276]?,Dunia ina maajabu yake!,sisi wengine tulioanza kujipambania kuanzia miaka 16 sijui tulifeli wapi [emoji851]
muwege mnasoma habari mnaimaliza nini hichi umeandika sasa
 
Alaf haya MAJINA ya kuwapa watoto tuwe nayo makini "STAHIMILI"
Ulaya kuna mchezaji anaitwa Hazard unaelewa maana yake ?

Acheni Mila potovu nyie waswahili. Kwani ukiitwa God ndio hutakufa au utakuwa na maisha mabaya ?

Hazard ana maisha mazuri kushinda mamilion ya watanzania wanaoitwa Samson

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kijana HAZARD ni Mbelgiji.. Huwenda neno HAZARD kwao lina maana tofauti. Zaa mwanao muite MSIBA,MASUMBUK,SHIDA,MASHAKA etc hujakatazwa.
 
Wazazi tuzae watoto tunaoweza kutunza, hivi unamkataaje mwanao wababa wwchache sana hujali watoto.
Umeshawahi kuishi na mama wa kambo?
Halafu baba Yako Hana sauti ?

Mama wa kambo ndy tatizo,,
 
Back
Top Bottom