Mzee mgonjwa apumzike jaman hii wanaupalia uraisi
 
Kila kitu ni protokali na usalama wa viongozi ni taaluma so asitupangie.
 
Yanajali basi.
 
Nadhani Mzee Filipo kabla ya kuongea hoja yake, alitakiwa aulizane na wataalamu wa usalama kwa nini wanataka barabara iwe wazi, na jinsi gani yeye akiwa anataka kupita sehemu, basi apite kwa wakati aliowaahidi Polisi. Kuliko achelewe na apite nje ya ratiba aliyoahidi wana usalama, halafu alalame

Zile confidence za enzi za corona kukataa chanjo na kuacha kuvaa barakoa, tuliona matokeo yake, pia taifa lina kumbukumbu ya ajali ya Edward Moringe Sokoine, taifa haliko tayari kurudia makosa.
 
Kuna siku PM alikua anapita mbeya, na vile mbeya barabara ni finyu ilikua shida sana ile siku.

Ukitokea mjini kuna maeneo huwezi kufika bila kupita main road na ndo hiyo PM anatarajiwa kipita saa zisizojulikana zijazo...

Foleni ikawa kubwa kichizi bila sababu tangu saa moja huyo Pm anapita saa 3.
 
Halafu kanichefua alipochomekea eti "mtoto wa masikini Mpango anapita" hawa watu ndo maana miaka na miaka bado wametuweka utumwani maana hawana akili wala utashi wa kuchukia umasikini. Mtu kujiita maskini anaona sifa sana alale kwenye nyumba ya tembe basi.
 
Mnapoiambia Dunia kuwa TANZANIA ni kisiwa Cha AMANI, Huwa mnamaanisha nini?

Kiongozi wa wananchi akipita spidi ni 120. Yaani anakimbizwa Kasi kuzidi AMBULANCE ya kuwahisha wagonjwa.!!!!

Jiji kama Mwanza kuzuia Kwa 4hrs Si sawa.

Viongozi wa Nchi MASKINI wanalindwa kuliko msafara wa kusafirisha PESA.

Hii Si sawa.
 
Huyo anasaka kiki za kijinga. Huo uhuni unafanyika ni zaidi ya miaka 7 sasa, viongozi wa nchi hii wamejigeuza miungu watu wanatupotezea muda kwenye misafara wakati wako madarakani kwa wizi wa kura.
 
Tuna mambo ya hovyo sana.

Nchi hii, kwa kiasi kikubwa, umaskini unachangiwa na Serikali na watendaji wake.

Serikali haioni thamani ya muda. Kuna wakati nakumbuka nilikuwa Mwanza. Saa 9 alasiri tumesimamishwa Nyegezi kupisha msafara wa Waziri Mkuu. Muda huo wa saa 9, Waziri Mkuu alikuwa Shinyanga. Halafu alipotoka Shinyanga akasimama Misungwi kuwasalimia wananchi.

Mwanza alifika saa 12.30 jioni
Yaani zaidi ya masaa 3 wananchi wamesimamishwa eti kupisha msafara wa Waziri Mkuu.

Fikiria watu wamesimamishwa tokea Nzega mpaka Mwanza. Ni watu elfu ngapi. Kama watu ni watu 10,000 shughuli zao zimesimama, na kama kila mmoja anaingiza sh 20,000 kwa saa, ina maana ni sawa na 20,000 x 3 x 10,000 = 600,000,000. Hiyo ni kwa siku 1 na kwa kiongozi mmoja. Bado kuna Rais, Makamu wa Rais, siku hizi mpaka makamanda wa polisi wakipita mnasimamishwa. Kwa mwaka, mambo haya ya ajabu yanaliingizia Taifa hasara kiasi gani?

Nadhani tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa Polisi wa kufikiri na kupanga. Kinachofanyika hakistahili kuwa hivyo. Uwekwe utaratibu ambao utazuia kuwasimamisha wananchi zaidi ya nusu saa kupisha misafara ya viongozi wa kitaifa.

Huu upuuzi haupo kwenye mataifa yaliyoendelea. Sisi maskini tuliotakiwa kuutumia muda vizuri zaidi, ndiyo tunaoongoza katika kutothamini muda. Umaskini wa kichwani unatufanya kuwa maskini wa kila kitu, isipokuwa kuzaliana..
 
Kusimamisha watu barabarani masaa matatu hadi manne kisa kuna kiongozi ni ulofa na upumbafu wa hali ya juu.polis mjitathimini.
 
Na wananchi wenye mawazo kama mtoa mada pia ni wengi
 
Baada ya kusoma hapo kwenye "Kusa mtoto wa masikini Mpango anapita" , hapo tayari najua anatania tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…