Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

Lissu sasa ashushe ushahidi kama kweli anao na kama hana ushahidi ajitafakari kama mwana sheria.
 
Hivi Makonda anafikiria kila mtu ni mjinga. Akae akijua wazi kwamba huenda ikawa TAL kajitokeza hadharani sababu anao ushahidi tosha wa tukio hilo. Labda Ushahidi huo utakuwa unamlenga mtuhumiwa bwana Makonda moja kwa moja. Huenda tutaona nani kati yao atakuwa mgonjwa wa akili.
tatizo la tundu lisu ni kukurupuka angalia alivyokurupuka kwenye issue ya TIGO
 
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.

Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.

Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.

"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"

"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"

"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"

BASHITE anafikiri kuwa Watanzania ni Wajinga na Wasahaulifu. Yaani kama kuna wa kwenda Mirembe basi ilitakuwa ni yeye. Nimeshangaa watu kumpigia Makofi kwa ujinga na uongo ulioutoa pale jukwaani.
 
Iweee! Kumekucha, kumbe uchaguzi ujao tuwe makini, nchi inaweza kuongozwa na chizi
Chizi mmoja anaitwa chizi
Wakiwa 10 wanaitwa machizi
Wakiwa 100 wanaitwa machizi 100
Wakiwa 1000 wanaitwa machizi 1000
Hawa 1000 wanaweza wakachagua chizi akawa kiongozi wao. Naye akaitwa kiongozi wa machizi
Turejee ya MAKONDA
 
BASHITE anafikiri kuwa Watanzania ni Wajinga na Wasahaulifu. Yaani kama kuna wa kwenda Mirembe basi ilitakuwa ni yeye. Nimeshangaa watu kumpigia Makofi kwa ujinga na uongo ulioutoa pale jukwaani.
Wewe una njaa upewe 10 hutapiga makofi kweli???
Popularity is popularity even Negative popularity is also popularity [ BASHITE, 2016]
 
Huyu ni muuaji, mahali anapostahili kuwa kwa sasa ni gerezani akisubiria siku ya kunyongwa hadi afe, ila ajue jinai haiozi ipo siku tutaruka naye tu.
 
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.

Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.

Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.

"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"

"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"

"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"
Tukio la jaribio la kumwua Tundu Antipas Lissu lilikuwa tarehe 7 mwezi Septemba 2017.

Kampeni ya ya afya na matibabu ilikuwa tarehe 6-10 Septemba 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda anawatangazia Wananchi wote wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni ya Upimaji wa Afya Bure kuanzia siku ya Jumatano ya tarehe 06 hadi10 Septemba, 2017 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Lengo la Kampeni hii ni kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na kuwahamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kuendesha maisha yao kwa gharama nafuu zaidi na kuwaepusha na magonjwa ambayo yangeweza kutibika iwapo wangepata taarifa mapema.

Makonda aja na Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho

MICHUZI BLOG at Friday, October 06, 2017

Mwendelezo wa zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye Matatizo ya Macho linaendelea na sasa ni Huduma ya Matibabu ya Macho kwa Wananchi waliobainika kuwa na Matatizo ya Macho kwenye Kampeni ya RC Makonda ya Upimaji wa Afya Bure.
Zoezi hilo ni kufuatia ahadi iliyotolewa na *Jumuiya ya Waislamu wa Dhehebu la Khoja Shia Ithnasheri Jamaat K.S.I.J iliyojitolea kumuunga Mkono RC Makonda kwa kujitolea Matibabu ya wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo ya Macho na Mtoto wa jicho kwenye Kampeni ya Upimaji Afya Bure iliyofanyika Mnazi mmoja.
Zoezi hilo linasimamiwa na *Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji.
Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa RC Makonda ameomba Taasisi hiyo kupima na kufanya matibabu kwa Wagonjwa 1,000 badala ya 500 iliyoahidi ambapo wameridhia ombi hilo.
Amesema kuwa kwa kawaida *Garama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda.
RC Makonda Anawahimiza Wananchi wenye Matatizo ya Macho kufika kwenye kambi ya matibabu ya Macho iliyopo mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili ili wapatiwe Vipimo, Matibabu na Miwani Bure kwa wenye uhitaji.
Ameshukuru wadau hao kwa kumuunga mkono na kueleza kuwa lengo lake ni kuwawezesha wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu kupata huduma.*

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongea na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho

Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho

Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho.

Ufafanuzi please....................

The onus to prove an alibi lies on the defendant. The duty to prove that the defendant was at the place the criminal act occurred lies on the prosecutor.

1. Je, PC Makonda alihudhuria huo mkutano wa afya tarehe 6 Septemba 2017 kisha tarehe 7 Septemba akasafiri kwenda Dodoma na kurejea Dar Es Salaam, tarehe 8 Septemba 2017? Uthibitisho unahitajika
2. Je, PC Makonda alienda Dodoma tarehe 6 Septemba 2017 na kusimamia kile kinachodaiwa jaribio la mauaji tarehe 7 Septemba 2017? Uthibitisho unahitajika
 
Timing ya interview ya Makonda na akina kikeke na zembwela ni ya kijinga sana, anafifisha mijadala ya utopolo wa tamisemi kwenye mchakato wa Uchaguzi Tarajiwa wa Serikali za Mitaa.

Huo kondoo anavutiwa waya tu sasa yupo kama dodoki wakati utafika atajikataa.

Baghosha Daud Albert Bashite a.k.a Dekio Makondanyo.

- Clouds -Tundu Lissu -Sumu
Content ya kuzubaisha ujinga mtupu

Time has no boundaries with Makondanyo

That's it

Pang Fung Mi
 
Andikaa hapo mleta madaa hatujamwelewaa alichotaka kutuambia dhidi ya mada yakee..
FB_IMG_1731931623196.jpg
 
Bwana mdogo Makonda ilikuwa ni heri kukaa kimya kuliko kufanya hicho unachofanya, kwa sasa tunapambana kuokoa watanganyika wenzetu walioangukiwa na ghorofa Kariakoo
Akae kimya vipi wakati hilo swali limeulizwa na mwanahabari live kwenye public.
Sasa ni m hezo mbaya msiamini maneno ya yeyote iwe Lisu ama Makonda Kwa asilimia 100, coz hao ni wanasiasa .

Kama watu mnashadadia eti Makonda ndo mhusika mna ushahidi Gani au kuamini tuu ya kuambiwa kama kondoo Ebu tuwe logical kidogo,eti mtu unaushahidi alafu unabaki kuongea tuu majukwaani Ama kweli siasa ni mchezo tena mchafu .
 
Tukio la jaribio la kumwua Tundu Antipas Lissu lilikuwa tarehe 7 mwezi Septemba 2017.

Kampeni ya ya afya na matibabu ilikuwa tarehe 6-10 Septemba 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda anawatangazia Wananchi wote wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni ya Upimaji wa Afya Bure kuanzia siku ya Jumatano ya tarehe 06 hadi10 Septemba, 2017 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Lengo la Kampeni hii ni kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na kuwahamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili waweze kuendesha maisha yao kwa gharama nafuu zaidi na kuwaepusha na magonjwa ambayo yangeweza kutibika iwapo wangepata taarifa mapema.

Makonda aja na Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho

MICHUZI BLOG at Friday, October 06, 2017

Mwendelezo wa zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye Matatizo ya Macho linaendelea na sasa ni Huduma ya Matibabu ya Macho kwa Wananchi waliobainika kuwa na Matatizo ya Macho kwenye Kampeni ya RC Makonda ya Upimaji wa Afya Bure.
Zoezi hilo ni kufuatia ahadi iliyotolewa na *Jumuiya ya Waislamu wa Dhehebu la Khoja Shia Ithnasheri Jamaat K.S.I.J iliyojitolea kumuunga Mkono RC Makonda kwa kujitolea Matibabu ya wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo ya Macho na Mtoto wa jicho kwenye Kampeni ya Upimaji Afya Bure iliyofanyika Mnazi mmoja.
Zoezi hilo linasimamiwa na *Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji.
Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa RC Makonda ameomba Taasisi hiyo kupima na kufanya matibabu kwa Wagonjwa 1,000 badala ya 500 iliyoahidi ambapo wameridhia ombi hilo.
Amesema kuwa kwa kawaida *Garama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda.
RC Makonda Anawahimiza Wananchi wenye Matatizo ya Macho kufika kwenye kambi ya matibabu ya Macho iliyopo mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili ili wapatiwe Vipimo, Matibabu na Miwani Bure kwa wenye uhitaji.
Ameshukuru wadau hao kwa kumuunga mkono na kueleza kuwa lengo lake ni kuwawezesha wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu kupata huduma.*

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akiongea na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho

Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho

Madaktari bingwa wa macho wakimhudumia mwananchi aliyejitokeza katika zoezi la upimaji wa afya bure kwa Wananchi Mkoa wa Dar es Salaam wenye matatizo ya macho.

Ufafanuzi please....................

The onus to prove an alibi lies on the defendant. The duty to prove that the defendant was at the place the criminal act occurred lies on the prosecutor.

1. Je, PC Makonda alihudhuria huo mkutano wa afya tarehe 6 Septemba 2017 kisha tarehe 7 Septemba akasafiri kwenda Dodoma na kurejea Dar Es Salaam, tarehe 8 Septemba 2017? Uthibitisho unahitajika
2. Je, PC Makonda alienda Dodoma tarehe 6 Septemba 2017 na kusimamia kile kinachodaiwa jaribio la mauaji tarehe 7 Septemba 2017? Uthibitisho unahitajika
Naona umeamua kumkaanga bashite.
 
Lisu na chadema waache ku deal na Makonda Wala kumtaja taja maana wanamfanya aonekane yupo juu sana,Inampa umaarufu na nguvu kubwa ndani na nje ya chama chake
Lakini pia wanajikuta wanatumia nguvu nyingi kupambana naye badala ya kutumia nguvu hizo kupeleka sehemu sahihi kwenye kunyakua kiti Cha kiongozi mkuu wa nchi
Chadema nawapenda ila mnanisikitisha sana ,mbona mnachezeshwa michezo ya kitoto na nyie mnacheza na mnapoteza uelekeo
Achaneni na Makonda Sasa.
 
Makonda alileta timu ya madakitari kutibu wananchi bure pale Arusha watu wengi walitibiwa na kupona hii ni jinsi Makonda alivyo na Huruma juu ya maisha ya watu Mimi binafsi nampongeza sana kwa ubunifu huu je wandishi wa habari mnalikumbuka takio hii? Tumpe maua yake mheshimiwa Makonda akiwa abatumikia wananchi
 
Mtu akupe tuhuma nzito kama hzo ukae kimya kwamba ndo uungwana.Lissu kama ana ushahidi auweke hadharani na wengine tumuamini tofauti na hapo namuona kama mtu mwenye msongo.
Kwa mtu kama Lissu angekuwa na ushahidi nadhani pangechimbika, ila sasa hivi hana uhakika ni nani alihusika, amachofanya ni kukisiakisia kwa wale aliowahi kutofautiana nao.
 
Back
Top Bottom