Makonda akabidhi ofisi kwa RC Kunenge, adai ofisi hiyo ina majungu mengi

Wakuu Shalom naona mubashara hapa RC Matata Bwana Makonda akidai kua anafurahia sana kwenda kumtunza Mwanae na kwamba hajapoteza lolote na amedai70% ya wananchi wa Dar ni wambea uzi tayari ntazidi kuwajuza[emoji23]

===

ATASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU, 2020
Ukishakuwa mstaafu unarudi kwa wanakijiji wenzako…, tutakaa na wananchi wenzetu tutakuwa tunashauriana namna ya kufanya mambo ya pale

Nafahamu kwamba upo mchakato unaoendelea katika ngazi ya Wilaya, mkoa na ngazi ya taifa. Lakini kazi yetu kama wanaCCM, ambalo hili haliwezi kufichika, na hili RC ulitegemee sana. Nitapiga debe mtaa kwa mtaa, kata kwa kata, tarafa kwa tarafa, wilaya mpaka mkoa kuhakikisha kwamaba Dkt. John Pombe Magufuli anaibuka kidedea kwenye mkoa huu wa Dar es Salaam, wabunge wanashinda wa Chama cha Mapinduzi.

Sasa hivi mimi ni raia lakini lakini kadi yangu ya CCM haijapotea. Nasubiria wakati tu. Kama ni kuniona tegemeeni kipindi cha kampeni nikiungana na Mwenyekiti wangu wa Mkoa na Mwenyekiti wangu wa Wilalya ya Kigamboni tukisaka kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 wa Rais, Wabunge na Madiwani.

UPIMAJI WA TEZI DUME: ENEO ANALOSIKITIKA KUONDOKA MADARAKANI BILA KULITEKELEZA
Eneo moja ambalo bado ambalo nalikumbuka na sijalifanya kwakweli, na moyo wangu unaweza kuwa unajuta na kujisikia vibaya, ni suala la tezi dume kaya kwa kaya. Nilitamani sana kulifanya, lakini kwasababu ya ratiba na muingiliano wa mambo mengi, tumekwama.

Kansa ya tezi dume inatesa sana watu. Ukipita kwenye idara ya afya utaona takwimu watu wengi wanavyopata shida. Shida kubwa sana. Ndoto yangu ilikuwa ni kuanzisha utaratibu wa kupita kaya kwa kaya kupima, kwasababu watu wanaaminii wakienda hospitali au sehemu Fulani itakuwa ni aibu. Lakini nilitamani niwafuate wananchi kwenye makazi yao.

Laiti ningelipata nafasi, ningefurahi sana kwamba kila kaya tungepima tezi dume. Na watu wanafikiri tezi dume ni kwa wanaume tu, la hasha! Hata wanawake wanapata tezi dume. Si ugonjwa wa aibu, si ugonjwa wa jinsia moja, lakini ni ugonjwa hatari unaoua Watanzania wengi.
Apumzike kwa amani.

Tukio liko mubashara Clouds tv karibu.

Up dates;

Makonda anasema alikuwa hafanyi kazi kwa kukurupuka maamuzi yake mengi aliwashirikisha RAS Kunenge na RPC Mambosasa

Makonda anasema baada ya kustaafu ataendelea na maisha yake ya kawaida huko nyumbani kwake kigamboni na milango iko wazi kwa yoyote yule atakayehitaji ushauri wake.

Kadhalika amemtaka RC Kunenge na RAS mpya kuwa makini sana na watumishi kwani ofisi hiyo imejaa wapiga majungu

Makonda amemkabidhi Kunenge Ilani ya uchaguzi na amemtaka asimwangushe katika kuitekeleza.

Maendeleo hayana vyama!
Mwambieni asisahau kukabidhi na BIO ya Twitter inatuchanganya
Hii ndo inadhihirisha Dar ni Jiji linaloshikiria roho ya Nchi ofisi imekbidhiwa utadhani Laizer anatoa madini kwa serikali tukio live kabisa..
1.Mh Rais Magufuli
2.Mh Samia Suluhu
3.Mh Kassim Majaliwa
4.Rc wa Dar
Aende zake hana mpya piga chini ata akigombea udiwani wa kolomije.
na watu wengi wa Dar humchukia sababu huwa anawapa za uzo
Ajiandae kugombea serikali za mitaa,kumbe kajenga Kigamboni.
Akatunze hilo broiler lake.
 
Kanunua nyumba moja ya serikali pande za ma saki nadhani ilikuwa kwenye matengenezo makubwa utasikia vijana wa Lumumba tataambiwa wivu wa kike, takukuru tunawasubilia.
Kasema mwenyewe atakuwa anaishi Kigamboni. Huko Masaki labda atapangisha.
 
Huyo ni mpiga domo. Siyo mchapa kazi. Projects zake zote alizopigia domo hakuna hata moja alofanikisha mpaka mwisho. Hivi walimu wanapanda daladala bure ?Ombaomba wale kwenye foleni wamekwisha ?Wajane ?Wale watoto walikusanywa baba zao wawahudumie ?

Walimu wanapanda bure mradi awe na kile kitambulisho.

Ombaomba hili suala hakuna aliyeliweza ni wananchi wangeacha kuwapa ombaomba hela lingeisha ila tunajifanyaga tuna huruma sana kwa kuwapa vimia mia.
 
Amesema mipango yake ya kupima tezidume kaya kwa kaya ipo palepale tatizo mambo yamekuwa mengi
 
"Asilimia 70 ya huu mkoa ni wambea, na wanapenda umbea kuliko chochote kile, msikubali wakawatenganisha wewe na RAS
wako.wanapiga majungu sana hawa msiwaone hivi, wanamjua mtu kuliko anavyojijua yeye". Aliyekuwa RC Dar es Salaam-Paul Makonda

NB: MAKONDA tuache wana DSM na mkoa wetu.
Acheni umbeya.
 
Mkuu wa mkoa mstaafu Paul Makonda amesema katika uongozi wake jijini Dsm alifanikiwa kurejesha serikalini nyumba zaidi ya 50 zilizouzwa kinyemela na kifisadi.

Makonda amemshukuru Mungu kwa kumpa ujasiri.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi huyu kizibo anapojiita yeye ni mstaafu hua anamaanisha nini?

Mtu anastaafu vipi ilhali hajafikisha hata miaka 55.

Au ni ule ubashite wake at its best??!!!
 
Back
Top Bottom