Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu

Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu

Makonda anatambua kuwa wananchi ndio wanaiajiri serikali . Viongozi wengine wajifunze kwa Makonda ubora huu .
 
Kila kitu kina utaratibu wake, kama alikuwa hamsikii angemwambia kistaarabu aongeze sauti, sio kumjibu kama alivyomjibu
Huyo Makonda ni mdhalilishaji mpaka kwa mkewe. Hawezi kumshauri chochote. Kuna wakati nilienda Serengeti mbuga ya wanyama. Wakati naandikisha details langoni ili niingie hifadhini, story kubwa miongoni mwa wahudumi wa pale langoni ilikuwa ni jinsi Makonda alivyomdhalilisha mkewe hapo langoni jana yake. Sikutaka hata kujua details za tukio lenyewe. Kila mmoja miongoni mwa wale wahudumu alitoa lake, lakini mmojawapo alisema, 'mimi mwanaume wa hivyo hapana. Ikitokea kwa bahati mbaya nimempata wa hovyo hivyo, siwezi kusafiri naye maana ukikosa uvumilivu mtajidhalilisha mbele ya watu"

Inaonekana Makonda ndivyo alivyo. Labda ametumia muda wake mwingi kuishi na ng'ombe kiasi kwamba hata akiwa na wanadamu, anawaona kama ni ng'ombe.
 
Hii tabia ni endelevu.
Kunamdau mmoja aliwahi andika uzi kuhusu udhalilishaji unaofanywa na huyu kiongozi

Alieleza madhara ya udhalikishaje akieleza swala la vinyongo ambavyo matokeo yake huwa si mazuri

NAdhan chama na serikali kwa pamoja wafanye kitu kuzuia hii tabia endelevyo la sivyo itajenga uhasama na uadui hasa lwa alotendewa udhalilishaji
 
MWACHE AHOJIWE NA ANATAKIWA ATOE MAJIBU SIYO KUMUNGUNY AMANENO WAMEIBA SANA MKOMBOZI KAINGIA ARUSHA WACHA WANYOROSHWE BADO LEMA
Hovyo wewe ni mkombozi wa nini huyo? unajua chochote juu ya utawala wa sheria wewe? unajua jinsi serikali inavyofanya kazi? unajua haki za watumishi ? unajua hawa watu wakati mwingine hawana hata mafuta ya kwendea field? mnaleta mihemko na kuandika ujinga ambao hamuwezi hata kuutetea? angekuwa mamako ndo anafanyiwa haya ungefurahi? anayeiba si anapelekwa mahakamani?
 
Akiwa kwenye ziara yake Longido, Makonda kama kawaida yake akiwa anatatua kero za wananchi, kamati hii ilihojiwa sababu ya ujenzi wa shule kusuasua.

Wakati mwanakamati huyo anajieleza Makonda alimwamvia haongei na mchumba wakw bali wananchi, nina mke mzuri nyumbani!

Kwamba alokuwa anaongea kwa lengo la kumtega? Na yeye angemjibu nina mume handsome nyumani angekuwa amekosea? Maadili ya kazi yanasemaje? Hata kama unamhoji mtu ameiba ndio unatakiwa umdhalilishe namna hiyo?

Dada pisi kali anataka kuposa mkuu wa mkoa 🤣🤣🤣🤣. CCM inakiwa iwe na kina makonda kama 50 hivi mambo yatakuwa burdaani.
 
Hovyo wewe ni mkombozi wa nini huyo? unajua chochote juu ya utawala wa sheria wewe? unajua jinsi serikali inavyofanya kazi? unajua haki za watumishi ? unajua hawa watu wakati mwingine hawana hata mafuta ya kwendea field? mnaleta mihemko na kuandika ujinga ambao hamuwezi hata kuutetea? angekuwa mamako ndo anafanyiwa haya ungefurahi? anayeiba si anapelekwa mahakamani?
Mkuu; Kutanguliza makasiriko sio suluhisho ya kilichotokea. Wenye busara waliwahi kusemaga hv: "Mkubwa hakosei" na wengine walisema: "Funika kombe mwanaharamu apite" Huyo mwanakamati ametumia busara kubwa sana kwa kukaa kimya na kutokutoa majibu kwa kile ww unachokiita "udhalilishaji".
Kama umewahi kufanya kazi kama mwajiriwa Serikalini, hilo wala halikupi shida.
Serikalini ni kawaida sana wakubwa(Mwenye cheo kukuzidi) kuwafokea masubordinates wake. Unatakiwa uwe mvumilivu ili uilinde ajira yako na siku zinaendelea. Hao akina makonda watapita na kukuacha unadunda na ajira yako. Kumbuka wao(akina makonda et al) wameshika kwenye mpini na wewe mdogo umeshika kwenye makali. Chukua tahadhari.
 
Aliambiwa mara nyingi aongeze sauti.Wacheni kutetea ujinga.Unapotakiwa kutoa maelezo ili wananchi wakusikie inabidi uzungumze kwa sauti ili usikike.Alihimizwa azungumze kwa sauti mara zaidi ya mbili akawa anarudia vile vile.
Kumbe na wewe ni mpuuzi!
 
Kuna watu wajinga sana nchi hii.
Huyu jamaa saa ngapi anafanya kazi za mkoa wake.
Nna mke mzuri ,kwani nani hana wake wazuri dunia hii.
Its too much
 
Aliambiwa mara nyingi aongeze sauti.Wacheni kutetea ujinga.Unapotakiwa kutoa maelezo ili wananchi wakusikie inabidi uzungumze kwa sauti ili usikike.Alihimizwa azungumze kwa sauti mara zaidi ya mbili akawa anarudia vile vile.
OK; Kwani kulikuwa hakuna kipaza sauti? Watu wanatofautiana katika kuonea- wengine ni wapayukaji, wengine sauti kama yote lakini wengine ndo hivo tena Sauti yao kimaumbile ni ndogo na ukizingatia huyo bwana ni mwenye vitisho, hiyo pengine iliweza pia kuchangia sauti kuwa hafifu zaidi.
 
Upumbavu sio tusi! Na ujue mpumbavu huwa haelewi tena!
Mkuu, kumwita mtu ni Mpumbavu (Stupid)manake huyo mtu akili yake, kufikiri kwake na mang'amuzi yake vimefikia ukomo (limit) kama ulivyobainisha hapo juu kwamba haelewi tena. i.e. hata ufanyeje hawezi kufundishika tena, ni kilema chake hicho. That's too bad. Ni tusi hilo.
 
Back
Top Bottom