Wakati Makonda akijiita Rais wa Dar es Salaam na Mkuu wa wakuu wa mikoa yote ya Tanzania alijionesha kama Sehemu ya Matajiri wa Bongo waliozaliwa na kukulia katika jiji la wenyewe jiji la Dar es salaam.Hata Juzi wakati Gharib alipofiwa na baba yake,Makonda alionekana hadharani wakati wa maziko ingawa alionekana kabisa yupo sehemu ambayo hakutakiwa.
Mimi binafsi Makonda ni mmoja kati ya watu amao niliwadharau sana.Kwangu mimi Makonda alikuwa jogoo wa Shamba aliyekuwa natajaribu kuwika mjini.Alikuwa mwenye tamaa nyingi,kiburi kikubwa majivuna pamoja na umbumbu na ulimbukeni wa madaraka.Alikuwa kiongozi mwenye upeo mdogo sana na mara chache alipojaribu kufanya jambo sahihi nyuma ya pazia alikuwa akifanya uozo mkubwa sana.
Katika historia ya dunia na siasa za Tanzania Makonda hakuwa na jambo la kipekee la kujivunia zaidi ya kuwa ni mtu wa kujikomba na kujipendekeza na opportunist ambaye hakuwa na aibu wala heshima binafsi.Makonda huyu ambaye analia kwamba anaonewa na kudhulumiwa alikuwa ni dhulmati asiyekuwa na aibu na ambaye alidiriki hata kuwadhulumu wale ambao walimheshimu na kumpenda.Makonda alimzunguka hayatiMagufuli na kumuingiza katika majaribu mengi sana kiasi kwamba mpaka JPM anaifariki dunia Makonda alikuwa ni mmoja kati ya watu waliochangia kumchafua sana JPM akifuatiwa na Yule jamaa aliyepata mvua 30 na yule anayemiliki timu ya mpira.
Swali langu la kujiuliza leo ni je Ushoga wa Makonda na GSM umefia wapi?Au ndo kama walivosema wahenga Kila zama na kitabu chake?
Makonda Pumzika kwa amani na usitafute huruma ya umma maana kwa Tanzania sisi wewe utabaki stori tu,Jiandae maana bado kuna watu wanataka kujua ile minazi uliyotoa Dar ukapeleka mwanza kama imeota.
Tulia tu dawa iingie vizuri kwa sasa.Mwisho wa yote umethibitisha ukweli wa kwamba madaraka ni koti la kuazima.Kubali yaishe UJIPANGE UPYA