chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Wahuni mtakaa, ngoja tuwanyooshe mbw nyiePambana lakini hutashinda,
Samia haendeshwi na mawazo yenu nyie wahuni.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wahuni mtakaa, ngoja tuwanyooshe mbw nyiePambana lakini hutashinda,
Samia haendeshwi na mawazo yenu nyie wahuni.
TKOBashite kapoteza Pambano Dakika za Awali kabisa
Yes, labda aliliwaHii issue ukimwangalia Baashite unaona wazi ana akili kama za wale madada wanaopewa funguo za gari bila kadi!!
Ipo haja sasa Watanzania tuelimishwe kuhusu neno Jasusi kwani nimegundua linatumika ndivyo sivyo hadi kwa Wapumbavu na Matahaira nao wanahusishwa nalo.Makonda ni jasusi
hakamatiki
Yupo anawachora tu
😂😂😂mako....ndaaa wakazie
Aseme huo izo lakini arudishe kiwanja cha watu mbona simple tuuNaam Uozo Usemwe na walio nyuma yake wasemwe na wote waliokosea hata ikiwemo wewe (Makonda) sheria ifuate mkondo wake muwajibike..., Huenda kufichiana Uozo ndio kulipelekea wewe kupewa hicho kiwanja
Hii nchi haipaswi kuendeshwa kimafioso
The biggest looser hapa ni Tanzania kama nchi..., yaani hii nchi imekuwa kama Telenovella
Kumbe mkataba anao? Kwa jio GSM ni matapeliGhalib hatakiwa kwenda mahakamani, yeye yupo salama, eneo lina hati yake, eneo lina vielelezo vyote namna alivyoliendeleza. anayetakiwa kwenda mahakamani ni bashite ambaye hana hati, wala vielelezo vya kuliendeleza, alichonacho ni mkataba tu ambao gsm anaweza kumruka.
Regent Estate ni eneo ghali sana....kuanzia mwaka 2000 mwenye kumiliki kiwanja eneo hilo ni lazima atakuwa na kipato kikubwa sana....View attachment 2148028
Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.
Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.
Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”
Kama hiyo haitoshi, katika ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliweka video ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambayo pamoja na mengine alieleza haja ya kutaka Jeshi la Polisi kuchunguzwa, kisha akaweka ujumbe:
“Naunga mkono hoja ya Kamati Kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi, wanaolipaka tope Jeshi la Jolisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda niko tayari kutoa ushirikianao.”
Madai ya GSM
Akifafanua zaidi kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, Wakili Mgongolwa amesema, mteja wake Ghalib Said Mohamed alinunua ardhi wilaya ya Kinondoni, eneo la Regent Estate plot no. 60, title no. 186153/60, kwa lengo la ujenzi wa makazi Novemba 21, 2006."
Vilevile, Mgongolwa amesema Septemba 2017, mteja wake aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International (Contract Class One) kwa ajili ya ujenzi wa eneo hilo wenye thamani ya Sh640 milioni.
"Ghalib aliomba kibali cha ujenzi na manispaa ya Kinondoni walitoa kibali hicho Oktoba 16, 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya ujenzi eneo hilo," amesema.
Ameongeza kuwa baada ya kibali hicho kutoka, Group Six walianza ujenzi na walipeleka malipo ya awali ya ujenzi Januari 31, 2018 huku mteja wake huyo akitekeleza sehemu ya mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh51.92 milioni, malipo ambayo yana kithibitisho kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kuhusu mteja wake kuwa na uhusiano wa karibu na mlalamikaji, alisema, "mteja wangu na mtu ambaye kwenye mitandao amekuwa akizungumza kwamba anamiliki eneo hilo, mteja wangu katika kipindi anachozungumza huyo mtu cha mwaka 2012 alikuwa hamfahamu kabisa huyo mtu."
"Mimi leo nathibitisha uhalali wa miliki, unaweza ukawa na uhusiano na mtu lakini sio wa kibiashara wa kuuziana na kuhamishiana miliki licha ya kuingia katika makubaliano ya kuhamishiana miliki,"
Mgongolwa alisema kufahamiana na mtu ni jambo lingine na miliki ni jambo lingine, hivyo ushahidi wa vielelezo kisheria unakingwa na vielelezo hivyo, ambaye anasema ni eneo lake aweke wazi vielelezo vya kisheria.
"Tunatoa changamoto kwa mtu yoyote yule aje akinzane na vielelezo vyetu, huu ni ujenzi kwa mujibu wa mkataba na haujasimamiwa na mjomba au shangazi," amesema Mgongolwa.
Alisema yeye yuko radhi kumsikiliza ili wakapambane, alisema kama kuna mtu anadhani anayo haki katika umiliki huo, lakini kwa sasa hawatafanya chochote na endapo ataendelea na matukio hayo hivyo basi ngazi za kisheria zitafuatwa.
"Hata tunaondokana na hisia tunaenda na uhalisia, yoyote yule anayesema aridhi ni ya kwake iwe kimahusiano au lah, aje na vielelezo kwetu, mtu mwenye dhana tofauti milango ya kimahakama iko wazi, ila kwa sasa hawatakwenda mahakamani," amesema Mgongolwa na kuongeza kuwa wajibu wangu kama mwanasheria ni kuthibitisha umiliki halali kwa mteja wangu.
"Hatua tutakazozichukua kuanzia sasa itategemea na matukio ambayo yatafuata kwani ndiyo yatatupa mwongozo wa nini tukifanye, ikitokea hatua ya kwenda mahakamani tutakwenda, ikitokea kuangalia ngazi nyingine tutalipeleka kwa kuwa maelekezo yetu yako wazi tunatakiwa kulinda haki ya teja wetu sambamba na jina lake," amesema.
Source: Mwananchi
Na Ritz na Home Shopping Centre=GSM mnafahamu mahusiano Yao? Niishie hapo!!!!Makonda akumbuke Naibu waziri Wa wizara ya Ardhi ni Ridhiwani Kikwete!
Picha inaanza subiri Kuna siku utashindwa kuongea haya. Unajifanya as if hazikuwepo enzi zake anatanua matako yake .Makonda amekuwa tishio sijui kwanini
Wengi wanamsema vibaya wakiwa uvunguni mwa kitanda
Yani kutoka kolomije uje kumiliki kiwanja regent estate anakoishi wakubwa aisee huyu dogo anatania sana.Regent Estate ni eneo ghali sana....kuanzia mwaka 2000 mwenye kumiliki kiwanja eneo hilo ni lazima atakuwa na kipato kikubwa sana....
Over
Makaburi yanafukuliwaHivi ule msikiti walipkuwa wanaujenga kwa pamoja ulikamilika?
Huyu akamatwe na kunyongwa tu, hana faida na nchi....aliumiza sana wananchi.Wakati Makonda akijiita Rais wa Dar es Salaam na Mkuu wa wakuu wa mikoa yote ya Tanzania alijionesha kama Sehemu ya Matajiri wa Bongo waliozaliwa na kukulia katika jiji la wenyewe jiji la Dar es salaam.Hata Juzi wakati Gharib alipofiwa na baba yake,Makonda alionekana hadharani wakati wa maziko ingawa alionekana kabisa yupo sehemu ambayo hakutakiwa.
Mimi binafsi Makonda ni mmoja kati ya watu amao niliwadharau sana.Kwangu mimi Makonda alikuwa jogoo wa Shamba aliyekuwa natajaribu kuwika mjini.Alikuwa mwenye tamaa nyingi,kiburi kikubwa majivuna pamoja na umbumbu na ulimbukeni wa madaraka.Alikuwa kiongozi mwenye upeo mdogo sana na mara chache alipojaribu kufanya jambo sahihi nyuma ya pazia alikuwa akifanya uozo mkubwa sana.
Katika historia ya dunia na siasa za Tanzania Makonda hakuwa na jambo la kipekee la kujivunia zaidi ya kuwa ni mtu wa kujikomba na kujipendekeza na opportunist ambaye hakuwa na aibu wala heshima binafsi.Makonda huyu ambaye analia kwamba anaonewa na kudhulumiwa alikuwa ni dhulmati asiyekuwa na aibu na ambaye alidiriki hata kuwadhulumu wale ambao walimheshimu na kumpenda.Makonda alimzunguka hayatiMagufuli na kumuingiza katika majaribu mengi sana kiasi kwamba mpaka JPM anaifariki dunia Makonda alikuwa ni mmoja kati ya watu waliochangia kumchafua sana JPM akifuatiwa na Yule jamaa aliyepata mvua 30 na yule anayemiliki timu ya mpira.
Swali langu la kujiuliza leo ni je Ushoga wa Makonda na GSM umefia wapi?Au ndo kama walivosema wahenga Kila zama na kitabu chake?
Makonda Pumzika kwa amani na usitafute huruma ya umma maana kwa Tanzania sisi wewe utabaki stori tu,Jiandae maana bado kuna watu wanataka kujua ile minazi uliyotoa Dar ukapeleka mwanza kama imeota.
Tulia tu dawa iingie vizuri kwa sasa.Mwisho wa yote umethibitisha ukweli wa kwamba madaraka ni koti la kuazima.Kubali yaishe UJIPANGE UPYA