Makonda: Hakuna nilichojifunza, nitawanyoosha. Wasiopaka rangi nyumba zao katikati ya Mji TUTABOMOA

Makonda: Hakuna nilichojifunza, nitawanyoosha. Wasiopaka rangi nyumba zao katikati ya Mji TUTABOMOA

Daud Albert Bashite hawezi kujifunza chochote ni jinsi gani aongoze,bado anadhani ni ule utawala wa Jiwe uliokuwa unambeba licha ya kuwa na mapungufu mengi.
 
Hizi ni miongoni mwa kauli zilizotolewa na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha katika hotuba kabambe ya Utambulisho aliyoitoa Mjini humo alipokuwa anakabidhiwa ofisi .

Hapa akikuwa akiwapa makavu waliokuwa wanamsengenya kwamba hajajifunza pamoja na kuwekwa benchi muda mrefu.
---
Makonda: Hamna nilichojifunza zaidi ya kuwashughulikia wazembe, wavivu na Wala Rushwa

View attachment 2958155
Akitoa hotuba baada ya utambulisho wake Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha Paul Makonda amesisitiza Viongozi wote kuwajibika na kutoa tahadhari kwa Wazembe. Akiongea mbele ya watu waliojitokeza kumpokea Paul Makonda amesema:

Mmenifurahia sana ila tutageukana muda sio mrefu. Sitajali wewe ni nani, baba yako ni nani, ulipataje hicho cheo, aidha ulipata kwa kuhonga, kwa rushwa au kwa uganga nitakula sahani moja na wewe.
Lazima kila mtu awajibike kwenye nafasi yake. Msiseme huyu alikuwa Mwenezi sasa katoka kwenye Uenezi atakuja amepoa. Wengine wanasema eti saivi labla atakuwa amejifunza, hamna nilichojifunza zaidi ya kuwashughulikia wazembe wavivu na Wala rushwa. Sina elimu yoyote mimi hata niwe Mkuu wa Mkoa wa siku moja inatosha lakini awepo mtu mmoja tu ajue kuna mwanaume amepita hapa.
Kwahiyo kila mtu kwenye nafasi yake, kama ni Mkuu wa Wilaya shika Wilaya yako barabara kama ni Mkurugenzi ishike Halmashauri yako kikamilifu.

Makonda: Majengo yaliyopauka yaliyo katikati ya mji lazima yapakwe rangi kama hawataki tutabomoa

View attachment 2958158
Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka wamiliki wa nyumba zilizopo katikati ya jiji hilo kuzipaka rangi ili ziwe na mwonekano mzuri vinginevyo nyumba hizo zitabomolewa.

Makonda amesisitiza kwamba Arusha lazima iwe na mwonekano na mandhari ya kuvutia watalii kwani mkoa huo ndiyo kitovu cha utalii nchini. Katika kueleza jambo hilo Makonda amesema

Tunataka Arusha iwe salama salimini tunapata watalii wengi sana haitapendeza wakija wakute hapapo salama. Usalama namaanisha wa kila kitu pamoja na kufanya biashara usiku. Hatutaki Arusha iwe mji mkubwa uliolala. Hao Watalii wakija hapa halafu baadaye wanaenda kulala hiyo hela tunaipata lini? Wametoka kwao hawajaja kulala huku wamekuja kushangaa. Lazima tuhakikishe usalama pamoja na usafi wa mji wetu.
Nilikuwa namdokeza RAS siku moja inabidi akae na wale watu wenye hizi daladala za hapa mjini angalau nasisi tuwe na mabasi ya ghorofa katikati ya mji. Na wenye majengo yao katikati ya mji Wapake rangi kama hawawezi tutabomoa, hatuwezi kuwa na mji umejaa uchafu rangi zinachanganyikana tu. Kamji kazuri haka, kana mandhari nzuri ni sisi wenyewe kukapanga
Nyote inaimba wimbo mmoja tu Makonda!
 
Makonda ni sawa na gunia la kinyesi kibichi, ukilibeba lazima yale maji maji yakuvujie, mama anabadili mbinu za kulibeba, lakini litendelea kumpa shida ya kulowana na harufu mbaya ya kinyesi
🤣🤣🤣
 
Hapo sawa kabisa Arusha kuna nyumba za zamani katikati ya mji hizi lazima ziboreshwe na ikiwekana akitika huko ahamishiwe Mbeya aje kusafisha jiji.
 
Hizo nyumba zipakwe rangi ya kufanana, si kila mtu ajiamulie rangi yake, tena ichaguliwe rangi ya kuvutia na kupendeza
 
Kwhyo Makonda ameshindikana si ndio!? Lkn nyie ndio mlimfata mkamrudisha kazin yeye alkuwa amekaa zake huko sjui Mwanza sjui Dar mkamfata mkampa uenezi bas acheni afanye kaz yke
 
Kwa ukumbusho tu...Mkoa wa Arusha

Mkoa wa Arusha.png
 
Huyu ndiye anawaamsha watanzania kuiondoa CCM madarakani.
 
Chadema lazima mnyooke kwa Makonda nimemsikiliza vizuri kwenye clip kuwa lazima wenye nyumba katikakati ya mji wazipake rangi zipendeze ziupambe mji wa Arusha kama hawataki wazibomoe….
Hata sheria za majiji zinawataka wapake rangi nyumba na majengo yaliyo katikati ya mji….
Makonda kanyaga twende
Nipe kifungu cha hiyo sheria nijisomee mkuu maana elimu haina mwisho.
 
Sisi wa kanda ya ziwa ndio tupo kimyaa, tumeridhika, wala hatuna kashfa mbaya dhidi ya serikali yetu. Hivi mnaonaje kaskazini mkatupilia mbali hivyo vyama miaka yote hakuna madiliko, maandamo si maandamano, mara udini mara ukabila, je! Tukiwapa nchi sisi wa kanda ya ziwa/dar na pwani kwa ujumla tutapona kweli!!

Najivunia sana ukanda wetu THE LAKE ZONE, Peace and love

Dar/Pwani/Lake zone/kanda ya kati na magharibi+Tanga💪🏽💪🏽❤❤✔✔✔
 
Back
Top Bottom