Ndugu zangu Watanzania,
Mimi leo wala sina maneno mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa .
Kwa hasira kali na kuonyesha moyo wake kujaa jazba na uchungu moyoni ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki,wajinga na wanasiasa uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.
Amesema huo ni unafiki mkubwa sana na ujinga kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja kwa kuzunguka katika Taifa zima.hivyo anachokifanya Rais Samia ndicho alichofanya Hayati Dkt Magufuli na huwezi kuwatenganisha au kuwatofautisha ,hivyo Rais Samia anaendelea na kazi hiyo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
Ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe ndio mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga huo wa kumuweka kando au kuwatenganisha Hayati Dkt Magufuli na Rais Samia katika mafanikio ya Rais Samia. amesema kuwa Waziri Mkuu Mh kasimu Majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia na Serikali ni moja na chama ni kile kile kimoja yaani CCM.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.