Makonda: Kuna watu hawakumuona Mzee Lowassa wakati anaumwa, leo hii amefariki wanajifanya walikuwa pamoja

Makonda: Kuna watu hawakumuona Mzee Lowassa wakati anaumwa, leo hii amefariki wanajifanya walikuwa pamoja

Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo Makonda amefika msibani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Lowassa ambapo amedai kuna watu anawajua hawakwenda kumjulia hali wakati anaumwa, walijikausha hivyo waendelee kukaa hivyo hivyo kimya.

Amedai mtu mwema ni yule ambaye mwanzako akipata matatizo utamjulia hali, hata ikitokea bahati mbaya akafariki basi unachakuzumngumza.

Tuache unafiki kuna wengine wanajiita marafiki wa Lowassa na hawakwenda kumuona akiwa hospitali wala nyumbani, alafu baada ya kufariki wanajifanya wao marafiki zake.

Lakini hawakujitokeza hapo nyuma hebu waache kumsemea mtu mazuri baada ya kufa.
 
Sawa sana. Isiwe double standards kwenye ukweli mwingineo ... tuhuma zilizopo.
Othrrwise, well said na R.I.P eternally Edward Ngoyai Lowassa
1000067529.jpg
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo Makonda amefika msibani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Lowassa ambapo amedai kuna watu anawajua hawakwenda kumjulia hali wakati anaumwa, walijikausha hivyo waendelee kukaa hivyo hivyo kimya.

Amedai mtu mwema ni yule ambaye mwanzako akipata matatizo utamjulia hali, hata ikitokea bahati mbaya akafariki basi unachakuzumngumza.

View attachment 2901905
Aise madaraka yanaleta uadui sana huyu kwa maneno haya inaonyesha ana bifu sana na bwana yule
 
Sitarajii kuona Lissu,Mbowe,Lema,Mnyika na sampuli zingine za. Wetu kama hawa wanapewà microphone Kutoa salamu za rambirambi kwenye Msiba wa Mzee wetu Mpendwa Lowassa kwani waliwahi kumchafua pakubwa sana
.
 
Mwenezi wa CCM mh Makonda amesema Watanzania waache Unafiki kwa kufanya marafiki wa Lowasa sasa ilhali wakati anaumwa hawakwenda kumuona

Tuache tabia ya kumsemea mtu mazuri baada ya kufa

Source: EATV
Naungana naye kwenye hilo la kumsemea mazuri mtu baada ya kufa.

Kwa nini mtu asipewe maua yake angali hai kama alivyoimba Roma!!??
Hivi hata kwenye hili Watanzania tunashindwa kuweka unafiki wetu pembeni kweli!!??
 
Back
Top Bottom