Makonda usikubali kuachia hilo ghorofa na imani kubwa kuna nguvu kubwa inakulinda

Makonda usikubali kuachia hilo ghorofa na imani kubwa kuna nguvu kubwa inakulinda

Kwa ufupi ni kwamba ukisalimu amri ukakabidhi hilo ghorofa kwa GSM jua daraja la umasikini linakunyemelea.

Kwa ninavyowafahamu wasukuma si rahisi kukata tamaa pambana hadi tone lako la damu la mwisho.

Kuna wakubwa wanafuatilia huu mtanange kwa ukaribu zaidi.

Kila la kheri
[emoji3][emoji3]
 
Kwa hiyo aliuziwa kiwanja alafu muuzaji akaingia mkataba wa ujenzi na Mkandarasi?

Mbona picha za uhamishaji wa milki hazina muhuri wa mwanasheria?

Na kama mwenye umiliki halali ni Makonda kwanini funds za Ujenzi zitoke kwa aliyemuuzia?

Hapa kunaweza kuwa na kesi ya utakatishaji wa fedha itakayowakabili wote kwa pamoja + matumizi mabaya ya madaraka kwa aliyekuwa kiongozi wa Mkoa.
 
Kama lilipatikana kwa dhuluma lazima lirudi japo wote ni wahalifu wakubwa hakuna mwenye nafuu hapo
 
Hii ni vita Kati ya aliyewahi kuwa mafia wa madaraka vs mafia wa uchumi. Muamuzi ni wakati.
Bashite hana pa kushika
 
La Makonda na GSM ni mwanzo wa ngoma tusubiri dansi lenyewe kwenye suala la ardhi nchini

Nawashauri tu wenye kumiliki maeneo hakikisheni mna nyaraka muhimu juu ya umiliki wenu

Otherwise kuna kilio kikubwa sana hapo baadaye
Naomba nisisitize hili. Watu acha kusoma umbea tu chukua na dondoo za msingi
 
Naona makonda kawangia kiwanda cha GSM kawatumia salamu za rambirambi....
 
Documents halali zitaamua nani mmiliki halali wa hicho kiwanja na mjengo.

Mpaka sasa GSM kaweka hadharani uhalali wa umiliki wa kiwanja na mjengo.Makonda aka Bashite atumwagie documents zake na si vinginevyo.

Tukimaliza hapo tu nakwenda kuangalia kama hicho kiwanja na mjengo viliorodheswa katika hati ya Tume ya maadili ya viongozi wa umma.

Tukimaliza hapo tutamhoji iwapo ana kipato halali cha kuweza kununua kiwanja husika na kufanya majenzi.

Tukimaliza hapo tunakwenda kumuhuliza wakati wa tukio la Lissu kupigwa risasi alikuwa wapi ?

Tukimaliza hapo tutataka kujua majina yake halali na cheti chake cha kumaliza std 7 & form 4.Tutaomba arejeshe mishahara yake yote tangu akiwa Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa.

Mpaka hapo itabidi arejee koromije.

Ni hayo tu kwa leo.

Ngongo kwasasa Mikocheni.
document yake hiyo apo
FB_IMG_16472387214699850.jpg
 
Nguvu kubwa inayomlinda ndiyo ile ambayo imechoma kiwanda cha GSM?😁😁😁
 
Konda boy anaweza kubanwa na kamati ya maadili kama ame declare mali yenye thamani hiyo.......hizi ndo zinatakiwa ziwe anga pendwa kwa takukuru....
 
Sasa hapo kama wanataka makonda ashtakiwe wanatakiwa waanzie hapo.
mengine yatafumuka yenyewe
Kupambana ni kupeleka hati na vielelezo vingine mahakamani sio kwa mipasho.

Na wakati huo huo atakuwa amewaalika takukuru ili awaambie ni kwa namna gani alizipata Mali hizo ikiwa mtumishi wa uma kwa muda mfupi? Je alikuwa akiorodhesha Mali hizo ktk fomu za maadili?

Pengine alishafanya biashara hatuwez kumuhukumu moja kwa moja, basi atalazimika kuonesha biashara na malipo yake ya kodi.

Kiufupi huu mgogoro unamuweka pabaya
 
Kwa ufupi ni kwamba ukisalimu amri ukakabidhi hilo ghorofa kwa GSM jua daraja la umasikini linakunyemelea.

Kwa ninavyowafahamu Wasukuma si rahisi kukata tamaa pambana hadi tone lako la damu la mwisho.

Kuna wakubwa wanafuatilia huu mtanange kwa ukaribu zaidi.

Kila la kheri
yeye alipata wapi? kama si lake ni muhimu apokonywe tu maana hamnna jinsi
 
yaani kung'ang'ania kiwanja cha mtu mwenye umiliki wa title deed ya miaka 99, building permit, land forms no 35, 28, 29 sales agreement etc sio tuu ukichaa bali kunaibua maswali mengi tuu ya uelewa huyo ex mkuu mkoa kama uko sawa, na kwa kuzidi kujichanganya eti sasa anatoa vitisho kuwa asipo pewa hicho kiwanja ataanika uovu ya mwenye kiwanjaa, shezi typee sijui TAKUKURU wako wapi yaani mtuu analazimisha rushwa hadharani???
 
Kwa ufupi ni kwamba ukisalimu amri ukakabidhi hilo ghorofa kwa GSM jua daraja la umasikini linakunyemelea.

Kwa ninavyowafahamu Wasukuma si rahisi kukata tamaa pambana hadi tone lako la damu la mwisho.

Kuna wakubwa wanafuatilia huu mtanange kwa ukaribu zaidi.

Kila la kheri
So hata kama alilipata kwa njia haramu.
Kumbuka hakutegemea boss wake angekufa akiamini baada ya boss 2045 ye ndo atakuwa Raisi.
Kumbe mganga aliwalia pesa zao, Hakuna mganga ajuaye kesho yako
 
Hilo eneo alinunua au alipewa kama zawadi na GSM? Alipewa eneo wazi au na hilo jengo/ghorofa?

Sijapata undani wa hili Sakata.. Thread zote hazielezei Kwa kina. Zinatoa muendelezo tu kama vile watu wote wanajua yanayoendelea huko Daslam

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanadai mchongo ulikuwa 2013,GSMu walimuuzia Bashite kiwanja maeneo nyeti hapo Daslam kwa 120M.Wao watoto wa mjini walikinunua 500M 2006.

Wanadai pia 2019 aliwaambia ni maelekezo kutoka kwa Mzee wa Chattle,
Kwamba mzee anataka GSMu wambarikie hekalu.

Wanadai tena GSMu wakashtukia mchongo Mkoromije alitaka kuwapiga tu, ajimilikishe Hekalu,Kwanza Mzee wa Chattle alisha RIP.

Sasa watoto wa mjini wamechukua chao na wana nyaraka zote,Mkoromije amebaki analialia na nyaraka zinasambaa zina picha juu ya muhuri.

Wadau pia wanahoji 2013 mbona Bashite alikuwa bado yupo koromije ata kama alikuja Daslam,alikuwa na uwezo gani wakupiga dili na Gisemu,
Maana hata hapo alikuwa bado hajamfunga kamba viatu Rizimoko mtoto wa msoga ili aingizwe kwenye sisitimu ya wakubwa.
Wadau tena wanahoji hata kama alinunua aliwa RC wa Daslam,bado mshahara hautoshi kupiga dili la 1B+ alizitoa wapi!?

Sa hivi wengi wanadai apelekwe kwa Pilato asurubiwe .
 
KWA MUJIBU WA MAELEZO YA LAWYER WA GSM NADHANI WANAUHALALI KWA DHATI KABISA
Usiamini sana maelezo ya mtu aitwaye wakili.

Hao wataaluma wana technic za kufubaza neno hata kama lina makali kuwili.

Dawa ya hili sakata, kesi itandazwe mahakamani, mtuhumiwa naye alete mawakili na vielelezo vyake wapambane.

Hata hivyo sielewi ilikuwakuwaje wakaanza vita ya kugombea na kunyang'anyana hako kakiwanja kama wafanyavyo walalahoi uswahilini?
 
Back
Top Bottom