SoC01 Malezi bora kwa watoto ndani ya familia na taasisi za kielimu ni msingi bora katika kuwajenga vijana wenye maadili ,wachapakazi na waaminifu

SoC01 Malezi bora kwa watoto ndani ya familia na taasisi za kielimu ni msingi bora katika kuwajenga vijana wenye maadili ,wachapakazi na waaminifu

Stories of Change - 2021 Competition

Kaladero

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
6
Reaction score
3
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wengi wetu ni mashuhuda wa kushuka kwa maadili miongoni mwa vijana na watoto wa sasa .Vijana wengi wamekosa nidhamu si kutowaheshimu wakubwa bali hata nidhamu ya kazi imepungua sana kwenye jamii zetu. Watu wengi wamependekeza bodaboda kama msingi mzuri kwa vijana kujitafutia kipato lakini huku huku ndo vijana wanaharibikia wachache sana wanaotambua umuhimu wa kazi hii kama ajira kwao.

Bodaboda wengi utawakuta na lugha zao ambazo hazina maadili hata kidogo nyingi zikitawaliwa na matusi. Vijana wengi heshima kwa wazazi imepungua sana hawawaheshimu wakubwa wao ,wengi wavuta bangi ambazo zimewaharibu na kuwafanya watu wa kutegemea vipato visivyohitaji nguvu.

Watoto wengi mjini wamekuwa wazururaji ,si kwamba wametoka vijijini hapana wengi wao wamezaliwa mjini na unawakuta wanawazazi na walezi lakini ni kuzurura asubuhi mpaka jioni na kurudi nyumbani usiku.

Vijana mashuleni matumizi ya lugha za matusi na zisizo na maadili yamekuwa makubwa hii ni sekondari mpaka vyuoni .

Baadhi ya vijana kushindwa kujitegemea katika mambo binafsi kama kufua nguo, kupika ,kufanya usafi wa ndani ,kulima na mambo mengine mengi. Wengi wa vijana hawa wakitoka kwenye familia zenye uwezo kiuchumi.

Nimefuatilia mambo yanayosababisha yote haya nikagundua malezi bora yamedolora kwenye familia nyingi na hasa mjini japo hata vijijini mambo yako hivyo.

Taasisi za elimu pia zimedolora sana katika kuwalea watoto na pengine hakuna muunganiko mzuri wa watoto kutoka malezi kwa wazazi pomoja na walimu mashuleni .

Shule za binafsi zimekuwa hodari katika kuwandaa vijana kwenye elimu ya darasani lakini mafunzo ya maisha binafsi kwa wanafunzi imekuwa jambo gumu .Wanafunzi wengi katika shule hizi hawawezi kupika, kufua hawawezi na hata kufanya shughuli mbalimbali zinazohitaji nguvu wanashindwa .

Mambo ya kufanya kukabiliana na wimbi hili la kudolora kwa malezi .
1. Wazazi watenge muda wa kukaa na watoto wao na kuwafunza maadili mema na kufanya kazi za ndani. Tusiwaachie vijana wa kazi malezi tushirikiane nao kama wazazi . Tusipofanya hivi tunatengeneza utengemezi mkubwa kwa watoto wetu .

2.Wazazi watoe uhuru wenye mipaka kwa watoto wao ,wawakaripie inapobidi. Mtoto mdogo mwenye simu mlinde muelekeze yapi mazuri ya kutumia kwenye simu muongeze mpaka umri wa kuweza kuyachambua ,tusiwaache watoto wetu kuchezea tu simu na hatujui wanafanyiamo nini.

3. Siyo kila taka ya mtoto ni hitaji lake wazazi tuangalie. Siyo kila muda mtoto akitaka kitu anapewa. Tuwatengeneze watoto waweze kutambua kuwa kuna milima na mabonde kwenye maisha ili kuwajengea akili ya kupambana wakati wa magumu. Inaumiza jambo ambalo angelitatua mtoto wa miaka kumi kijana wa miaka ishirini anashindwa kulitatua.

4. Wazazi wanapoondoka nyumbani asubuhi tuwaachie kazi watoto wetu, hii ni hasa kwa watoto wa mjini. Inawajengea akili na moyo wa kupambana na kuchapa kazi.

5. Taasisi za elimu zitenge muda wa wa kazi kwa wanafunzi. Hii inajenga moyo wa kujishughulisha .

6. Masomo ya dini yatiliwe mkazo mashuleni ili kujenga vijana wenye maadili.

Hitimisho
Jamii ibadilike familia tuwajengee watoto uwezo wa kujitegemea na moyo wa kufanya kazi. Tuwasaidie ili wajenge mahusiano mazuri baina yao.

Na ,
Kaladero
 
Upvote 0
Back
Top Bottom