king kwengi
Member
- Mar 25, 2018
- 23
- 14
Mkuu kuhusu imani kupotoshwa na Mungu kuruhusu nafkiri alishatuasa kwenye biblia kuhusu kuja kwa manabii wa uongo ambao watapotosha misingi ya imani na kweli na watatupeleka katika kuamini imani zisizo sahihi hivyo ni kazi kwetu sisi tunaofuata imani hizi kutambua ipi ipo kwenye msingi wa imani na ipi imekengeuka ili tusije kujikuta tunaongozwa na makanisa ya manabii wa uongo waliokuja kupotosha imani yetu huo ndio mtazamo wanguKusema ukweli mambo ni mengi sana ambayo tunapaswa kuyajua lakini bahati isio kua njema hatuyajui.
Shukrani kwako mleta mada kila siku nakupa saluti kwa mchango wako hapa JF haswa Jamii intelligence.
Lakini pia shukrani za kipekee kwa wadau kwa michango ambayo inaipa mada husika thamani.
Kwa habari ya huyu mwana mama ni moa kati ya wanawake wachache waliofanya kitu chakipekee tofauti na na wengine na kuondoa ile dhana ya mwanamke ni kuzaa na kulea tuu, japokua jukumu hilo kamwe kwa mwanamke halimkwepi.
Lakini pia tunazidi kujua africa si kama vile tulioamniashwa kwenye vitabu vya historia. Nadhani sasa ni wakati wa africa kuamka pale tulipo angukia na kuendelea japo tumebaki nyuma sana lakini haitalingana na kuendelea kubakia hapa tulipo.
Mkuu Malcom Lumumba kuhusu post yako #45 imeniacha njia panda japo imenitafakarisha sana kuhusu dini. Lakini sina la kusema maana mimi nimeamini na katka imani ninatumaini. Sasa inapokuja changamoto kama hii kuhusu dini maswali yakua kua mengi yasio na majibu.
Kama ndio hivyo ulivyosema je Mungu nafasi yake katika kuzuia hilo iko wapi? au ndio kusema ni idhini yake iwe hivyo? kwa sisi africa tudanganywe kuhusu yeye? Na mwisho wa huu uwongo utakua ni lini?
Nipende kuwatakieni kila jema na wepesi katika mambo yote. Tusichoke kuhabarishana chochote tukipatacho bila kuchoka huwenda siku moja haitakua hivi ilivyo leo.
kuna uzi fulani humu mtu anatusisitiza kuiamsha mizimu,tukimsikiliza huyu na kumuelewa kwa kweli tunahitaji kweli kuiamsha maana anguko letu lilianzia hapo.kuangamiza kwanza imani na tamaduni zetu.hakika tunahitaji kuzitafuta asili zetu.Mzee Jomo Kenyatta (R.I.P) aliwahi kusema hivi:
"When the white-men came, we had the land and they had a Bible. They said close your eyes and lets pray.
When we opened up our eyes they had the land and we had the Bible" Shetani anaishi kwenye nyumba za ibada tangu kipindi Yesu aliposema "Nyumba ya baba yangu haitakuwa ni pango la wanyang'anyi" Washika dini ndiyo wanaongoza kwa kurudisha bara letu nyuma kimaendeleo kwa mafundisho yao potofu. Hili ushahidi wake ni mkubwa sana na haihitaji kuwa na PhD ili kuyaona
Hapo kwenye semitic sijawaelewa ni jamii ipi na vile vile hamitic nayo sijawahi kuielewa.
Baba yangu ni mtanzania mwenye uraia wa rwanda. Alisawahi kuniambia sisi watoto wake ni hamit sio wabantu. Nikatafuta maana ya hayo ila sikuelewa sana embu shusha vitu
Soma huu uziYawezekana Climate factor inachangia mkuu ndo maana wanakua weupe(kama walikua weusi)
Mkuu hayo mambo ya kwamba wazungu walibomoa sanamu za Mary na Yesu wakiwa weusi hua naona ni chai tu maana sijaona ushahidi wa hiko kitu. Mkuu naomba vigezo vinavyokufanya um-term Yesu kua ni black.
nigeri .nimewahi kuona kwenye bibliaWale walikuwa mchanganyiko.
Kama wana wa Mussa walikuwa wana weusi kwasababu mama yao Zippora alikuwa mweusi. Manase na Efraimu walikuwa wana weusi kwasababu mama yao Asenati alikuwa ni mmisri wa Kemet. Ushahidi mwingine ni wale Wayahudi wa Ethiopia kabila la Dan ni weuso tiii lakini bado ni wahebrania.....
NB: Kumbuka siyo kila Semitic amekaa kama mwarabu au mhindi. Kuna watu Semitic lakini ni weusi tiii, kama kabila la Wairaqwi kule Manyara. Wale siyo Hamitic kama tulivyo wabantu lakini ni wuesi
Ndugu yangu wala hiyo mizimu haiwezi kutusaidia kitu kama hatujajifunza kung'amua ukweli kutoka kwenye uongo.kuna uzi fulani humu mtu anatusisitiza kuiamsha mizimu,tukimsikiliza huyu na kumuelewa kwa kweli tunahitaji kweli kuiamsha maana anguko letu lilianzia hapo.kuangamiza kwanza imani na tamaduni zetu.hakika tunahitaji kuzitafuta asili zetu.
ni sawa sikumaanisha kwenda kutambika nilimaanisha kuanzia walipotuvizia na kulishana upya chakula ya ubongo bila ya unafiki.Ndugu yangu wala hiyo mizimu haiwezi kutusaidia kitu kama hatujajifunza kung'amua ukweli kutoka kwenye uongo.
Hiyo mizimu ilishindwa kuwasaidia wazee wetu kipindi hicho cha kabla ya ukoloni, haiwezi kutusaidia sisi leo. Mtu ni Kichwa na siyo kinginecho, leo mkiamua kwamba tunaiokomboa Afrika ni lazima muanze na akili za watu kwanza. Hayo mengine ni mbwembwe tu, dini yoyote inaweza kutumika vibaya kuleta unyonyaji, iwe ya Mzungu, Mweusi au Mwarabu.
Hapo nakuunga mkono kabisa mkuu.ni sawa sikumaanisha kwenda kutambika nilimaanisha kuanzia walipotuvizia na kulishana upya chakula ya ubongo bila ya unafiki.
Labda history inayofundishwa katika mfumo wetu wa elimu ukawa na madhaifu yao hasa kwa namna tulivyotawaliwa na kupewa si kupigania uhuru kama wenzetu.Ni kweli kabisa... Historia tunayofundishwa waAfrica imeegemea zaidi kwenye kushindwa kwetu dhidi ya wazangu...
Wakati kuna mengi mazuri na makubwa tumefanya...
Cc: mahondaw
Labda history inayofundishwa katika mfumo wetu wa elimu ukawa na madhaifu yao hasa kwa namna tulivyotawaliwa na kupewa si kupigania uhuru kama wenzetu.
Je Elimu ya huko kwao Ethiopia haziwazungumzii watu hawa?
tutachelewa lakini tutafika ila tatizo waliotangulia na wanaoweza kuyaanzisha haya ni wanafiki na wabinafsi ila kweli inahitaji kuchimbuliwa.Hapo nakuunga mkono kabisa mkuu.
Mwanadamu huanza kufanikiwa pale tu anapoanza kujikubali na kuridhika na alivyo. Huwezi ukamshinda mzungu kwa kutumia akili ya mzungu, its waging war against Mars (The Roman god of War). Kuna kitabu cha Willie Lynch kinaitwa The Making of a Slave, kinaonyesha ni jinsi gani wazungu walipanga kuharibu akili ya mwafrika ili asiwe kikwazo ndani ya jamii yao. Wameweka na nukuu kabisa za hotuba ambazo wazungu walikuwa wanapeana bila aibu.
Mkuu Malcolm bora leo umegusia issue hii ya hamites..... Nimesoma classification za wanadamu katika makundi matatu yaani negroids,caucasians na mongoloids nikaona kwenye caucasians amewekwa semites,hamites na aryans huku kwenye negroids amewekwa dravidans yaani wahindi weusi wa Goa pamoja na jamii zingine zilizopo afrika sasa sijaelewa kwanini hamites wametengwa na jamii zingine za watu weusi if at all tumetoka nature mojaKuna jamii aina tatu katika mtazamo wa historia ya watu wa mashariki ya kati.
Semitic, Hamitic na Japhaetic. Semitic linatokana na jina la Shem (Mwana wa Nuhu) na ndiyo baba wa Waarabu, Wahebrania ,Wahindi nk. Hamitic linatokana na jina Ham (Mwana wa Nuhu) ambaye ndiyo baba wa Kush, Put, Mizrahim (watu weusi). Japhaetic linatokana na jina Japhet (Mwana wa nuhu) ambaye ndiyo baba wa Tubal, Ashkenazi (Watu weupe). Kiufupi ndiyo vizazi vya Nuhu.
Tunasema watu wa kale walikuwa ni weusi kwasababu wana wa Ham walikaa Mashariki ya katina kufika hadi Afrika.
Wazao wa Mizrahim walikaa Misri, Wazao wa Put walikaa maeneo ya Libya na wazao wa Kushi walikaa Arabia pamoja na sehemu za pembe ya Afrika. Walikuwa wanatumia hadi usafiri wa majini kupitia ghuba ya Aden kufika Arabia. Ushahidi wa haya mambo upo sana na unaonyesha Ethiopia waliwahi kwenda kuwapiga waarabu pale mashariki ya kati baada ya kuona Wakristo na Wayahudi wanateswa na walitumia tembo. Walikuwa na muingiliano mkubwa sanaa sanaaaa.
Turudi kwenye swali lako sasa,
Dr Ivan Van Sertima anasema watu weusi wako hadi aina sita hivi. Kuna wale wana ngozi nyeusi sana pua pana na miili mikubwa (The Bantu). Kuna wale wana ngozi nyeupe kidogo na pua nyembaba na warefuu sanaa (The Nilotes) ambao ni Wanyarwanda, Wasomalia, Wamassai, Wasudan na wengine. Hivyo watutsi ni Nilotic kwasababu walitokea ukanda wa Nile na kuja kukaa hapa Afrika Mashariki na kujenga falme zao. Hivyo siyo kila mweusi ni mbantu, kwasababu hata baadhi ya Wachagga siyo wabantu na ushahidi wa kwenye lugha upo. Maana lugha nyingi za kibantu huwa zina hulka ya kufanana sanaa kwenye mizizi yake.
Hata Wanyakyusa baadhi yao ni Nilotic kwa maana wakoloni wa Uingereza wanasema walitokea Sudan kipindi hicho ni falme za Kush na Nubia. Hadi kwenye Oral Traditions zao za zamani wanyakyusa wanasema kwamba wao walitokea kwa Malkia moja wa kule Nubia anaitwa Nyansebo. Ilitokea vurugumai ya kugomabia madaraka kwasababu miaka hiyo wanawake kwenye falme za Kushi walikuwa wanaruhusiwa kutawala. Lakini wengi hawakumpenda malkia wao na wakamwondoa na likatokea vurugumahi na wakaanza kuhama sana. (Kwenye nyaraka za wapepelelezi wa Uingereza na Ujerumani kabla ya Ukoloni)
Kuna Oral Tradition nyingine inasema kuna jamii ilitokea ukanda wa Misri kwa kupitia mfereji wa Suezi na kuamua kufanya makao hapa Afrika Mashariki, pembeni ya ziwa viktoria. Sasa kuna mijadala ilikuwepo mikubwa sana na mtu kama Dr. Rudolf Windsor alishindwa kutoa ushahidi kwamba hii jamii ni ya watu gani aidha Bahaya, Baganda au Banyarwanda (Who knows). (Oral Traditions na Prof Rudolf Windsor)
Ndio maana nikasema bado kuna nchi Africa ambazo mifumo yao ya elimu husema kweli na kuwaweka watu wao maarufu katika mioyo ya vizazi vipya kwa njia ye Elimu ikiwepo Ethiopia na si kama sisi ambao si tu tunaona ni ushamba kuusema ukweli juu ya Kinjekitile na kina isike bali pia tunadharau na kuona hawana maana katika kizazi hiki za teknologia habari!Ethiopians wana kiwango kikubwa sana cha Uafrika kuliko jamii yoyote ile. Aina ile ya kiwango cha kupenda uafrika nimeiona kwa wajamaica tu. Wao hawana hata siku ya Uhuru kama sisi, wao wanasherehekea ADWA, siku Mfalme Menelik II alipomtwanga Muitalia. Hata lugha yao ya kusomea ni Amharic, ile ile ya vizazi na vizazi: Wanafundishwa sana na vizuri kuhusu wenyewe na ndiyo maana ukienda sehemu za vijijini utakuta wanahulka ya kudharau sana weusi wa kibantu. Wao huamini kwamba hapa Afrika hakuna jamii kama yao (Japo nilivyoishi nao ni watu wazuri na wakarimu)
Mkuu Malcolm bora leo umegusia issue hii ya hamites..... Nimesoma classification za wanadamu katika makundi matatu yaani negroids,caucasians na mongoloids nikaona kwenye caucasians amewekwa semites,hamites na aryans huku kwenye negroids amewekwa dravidans yaani wahindi weusi wa Goa pamoja na jamii zingine zilizopo afrika sasa sijaelewa kwanini hamites wametengwa na jamii zingine za watu weusi if at all tumetoka nature moja
Asee ahsante kwa clarification inaonekana hawa wajerumani wameanza ubaguzi zamani sana nakumbuka kuna documentary moja ya History channel ambapo Hitler alidai super race ni ARYANS ambayo ndio imeumbwa kutawala hii dunia na sisi wengine tumeumbwa kuwa subjects kwao dah ni shida sana yaani wanadamu wote tumetoka kwa Baba mmoja ila tunabaguana hivi kwa misingi ya rangi hivi Nuhu akifufuka si anaweza pata kiharusi pale atakapoona kuna wengine wanaitwa manyani na wengine wanajiita nchi teule!!Mkuu Zitto,
Ukisoma kitabu cha From Babylon to Timbuktu, Dr Windsor anasema kwamba hadi kufika karne ya 15 wanadamu walikuwa wamegawanywa kwenye makundi matatu. Hamitic, Semitic and Himitic: Lakini tatizo lilikuja pale ambapo mwanasayansi wa Kijerumani Johann Friedrich Blumenbach alipoleta ya kwake na kuwagawanya binadamu katika makundi kama matano hivi:
1. Caucasian
2. Mongoloid
3. Malayan
4. Ethiopian
5. American Indian
Baada ya mgawanyo huu basi Pandora Box likawa limefunguliwa na wanadamu hawakuishia hapo kuanza kuwagawnya wenzao.
Negroid lilikuja baadae sana kama kundu la jamii ya watu wa Ethiopia. Aryan likaja baadae baada ya kuligawa kundi la Caucasian na mwisho wa siku ni mvurugano mtupu ambao tunao leo.
Hao wazungu ndio walioitunga wametuficha mengi sana, hakika waafrika ni mbumbumbuNi kweli kabisa... Historia tunayofundishwa waAfrica imeegemea zaidi kwenye kushindwa kwetu dhidi ya wazangu...
Wakati kuna mengi mazuri na makubwa tumefanya...
Cc: mahondaw
Kwenye falsafa ya Ujerumani hata kabla ya Hitler kuwepo kuna kitu wanakiita The Volk-Geist wakimaaisha Volk kama People na Geist ni Spirit/Ghost. Hii falsafa inadai kwamba ili mtu ailewa Ujerumani ni lazima awe ni mtu wa jamii hiyo. Wakina Von Savigny ndiyo waliipigia sana debe hii kitu.Asee ahsante kwa clarification inaonekana hawa wajerumani wameanza ubaguzi zamani sana nakumbuka kuna documentary moja ya History channel ambapo Hitler alidai super race ni ARYANS ambayo ndio imeumbwa kutawala hii dunia na sisi wengine tumeumbwa kuwa subjects kwao dah ni shida sana yaani wanadamu wote tumetoka kwa Baba mmoja ila tunabaguana hivi kwa misingi ya rangi hivi Nuhu akifufuka si anaweza pata kiharusi pale atakapoona kuna wengine wanaitwa manyani na wengine wanajiita nchi teule!!
Kazi kwelikweli
historia ya kinjeketile ngwale huijui, unatuletea za watu wa nje