Mama awashinda watoto wake Kesi ya Mirathi ya Nyumba Kariakoo

Hao hao unaowaita wavaa kobazi ndiyo wamiliki wa maghorofa mengi kuanzia Kariakoo, Upanga , Mnazi Mmoja na maeneo mengi ambayo ni potential.

Sasa hata ukiwaita majina yakupendazayo wala hawana muda na wewe wala hawakufahamu.
Wote ni waarab na wahindi na tena wengi zaidi ni shia wala siyo suni kama wewe hata msikitini kwao hautakiwi
 
Nani huyo aliweka hiyo sheria ya thumni? Sijaelewa hapo.
 
Vijana wa hivi nimewashuhudia kinondoni sana na Mwananyamala aisee, Yan wao ubishoo mwingi ila ikifika jioni anarudi kwa mama kula na kulala jitu zima hd aibu aisee
 
Wewe niwale wale
 
N
Nani ameweka hiyo sheria, sheria ya waarabu unasema Mungu kafafanua?
 
Mitoto jinga hii yamezoea umwinyi tu ona yalivyoaibika mahakamani.Imagine ni watoto wake wa kuwazaa ndo wamemtenda haya.Pole sana bibi yetu iyo nyumba ukifa itoe Sadaka.Kuliko kuwaachia hao mashwetani.
 
1. Watoto walifungua mirathi. Hawakumjumuisha mama yao kwenye orodha ya warithi.

Hivyo, Mama akawa nje ya warithi. Akaondolewa kwenye mirathi.

2. Mama akapinga hilo. Akataka nayeye awe miongoni mwa warithi.

3. Mama ameshinda kesi. Mahakama imeona kuwa mama huyo nayeye ana haki kwenye mirathi hiyo. Mama amerejeshwa kwenye mirathi. Anakuwa miongoni mwa warithi.

N.B: Watoto wapo 6. Kati ya hao sita, ni mtoto mmoja tu ndiye alikuwa upande wa mama akimtetea ajumuishwe kwenye mirathi. Watoto wengine 5 walikuwa hawataki mama awe kwenye mirathi. 😎

-Kaveli-
 
Hongera sana Mahakamankwa kutenda haki. Watoto watafute mali yao.
Ndiyo tatizo la kulelea mitoto kinenani, unless kama walibaini kuna zoba 'kamkamata' mama yao na kuna dalili anajazwa mkenge kwa sababu ya mahaba ili waiuze na asepe na pesa.
Nyumba ni yao wote(mama na watoto wake) ila kama ni kweli walikuwa wakimfukuza asifike(labda kwa ushauri wa wake zao kama wametoa kwani it very strange watoto kumfukuza mama yao) basi ni vizuri uamuzi uliotolewa.
NB: There are always different sides of the story, labda tukisikia upande wa watoto pia tutashangaa zaidi japo si lazima uwe ukweli hundred percent. Ukweli unaweza ukabaki kuwa mystery licha ya mahakama kuamua in favor of the mother lakini watoto kumfukuza mama yao that's a very terrible thing to do.
 
Kuna familia zingine za ajabu sana
Familia za Kiswahili ndio zipo hivyo.
Kuna wahuni wanapambana na baba yao mkubwa mwaka wa 15 sasa wakitaka kuuza ardhi wanayodhani ni ya baba yao, kumbe baba yao alimuuzia baba yao mkubwa wakiwa watoto sana, muda mfupi baada ya kuuza akafariki kabla ya kuhamisha familia,ndugu wakaomba mama yao aendelee kuwalelea pale, mama yao anefariki wamekuwa wakubwa, wanataka kumvimbia baba yao mkubwa.
 
Mali ya mume na mke haiwezi kuwa ya watoto. Watoto wanapewa Kwa willing ya wazazi. Urithi siyo jambo la lazima, bali matakwa ya hiari ya wazazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…