Mama Salma Kikwete, kutaka wake wa viongozi wakuu wapewe pension ni kumkufuru Mungu!

Mama Salma Kikwete, kutaka wake wa viongozi wakuu wapewe pension ni kumkufuru Mungu!

Unataka kuniambia kuwa yeye mama Salma, hakupewa mafao yake ya kuacha Kazi yake ya ualimu baada ya mumewe kuwa Rais wa nchi?

Usipende kutetea Hawa viongozi wa CCM, wanyonya damu za watanzania masikini, ambao kwao, matumbo yao ndiyo wanayoyapa kipaumbele.
Sijawahi fungamana na upande wowote wa siasa. Maana waliopo siwataki na wanaotaka kuja siwaamini. Ila tuwe tunasikiliza na kuelewa, si ajabu hujamsikiliza umesoma tu kilichoandikwa ukachanganya na emotions

Msikilize hapa

Huyu mabeho yuko wapi aichukue hii nchi tumechoka na dhihaka.

Na ukifuatilia atakuwa na penshion ya ualimu.

Japo Magu aliniumiza ila ni bora angekuwepo.
 
Sijawahi fungamana na upande wowote wa siasa. Maana waliopo siwataki na wanaotaka kuja siwaamini. Ila tuwe tunasikiliza na kuelewa, si ajabu hujamsikiliza umesoma tu kilichoandikwa ukachanganya na emotions

Msikilize hapa

Pamoja na kuisikiliza hiyo clip, bado hujaniwashawishi kuwa huyo mama alichoongea ni cha maslahi ya Umma.........

Mimi nitaendelea kuamini kuwa alichoongea ni cha maslahi yake binafsi na ya familia yake.
Full Stop 😃
 
Ajabu sana.

Inashangaza pale ambapo familia kama ya Kikwete inakuwa bado na mawazo ya pensheni. Hawa ambao kwa nafasi zao kama wastaafu wanalipwa asilimia 80 ya mshahara anaoliopwa Rais aliyepo madarakani, na vitu vingine vyote kwao ni bure.

Huku upande wa pili kuna familia ya mstaafu ambaye bado hajaanza kulipwa mafao yake zaidi ya mwaka mmoja, ana watoto watatu waliomaliza vyuo bado hawajapata ajira, anajilipia bili za umeme, nyumba na maji, na bado makato ya tozo yako juu yake.
 
yani yule babu yangu wa msoga ana miaka zaidi ya 70 na more than billions in the account.

Hivi kweli mtu hutosheki kuwa umekula nchi kiasi hiko mpaka wife akaropoke huko kiwa anataka vimillion kadhaa vya pension ya utumishi aliokuwa anafanya ??

kwanini asielekeze ziende hata charity kwenye shule ambazo hazina madawati jimboni kwake.
 
We ni fala, nenda kamsikilize utaelewa, sio unaanzisha uzi kijinga kiasi hiki wakati hujamsikiliza, amesema wazi hawapewi hayo mafao pale wanapoachishwa kazi zao ambazo walikuwa wanafanya.
Hakuna ufala wowote hapo, wanatakiwa wajisimamie kwenye biashara zao kama ambavyo wengine wanajisimamia, wasiwe wategemezi wa kodi za masikini.

Pesa zote wanazolipwa kama wastaafu serikalini asilimia 80 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, huduma zote za bure wanazopata, posho na mishahara wanayopokea bungeni, bado unawatetea hawa?

Kubali tu, hapo hakuna kiongozi, tuna mtu asiejielewa aliyepewa ubunge wa viti maalum kama zawadi tu.
 
Tuanze kwanza orodha ya wake was viongozi wastaafu.
1.Mama Sokoine
2.Mama Bilal
 
Watanzania wengi tunatabia ya kukurupuka na hata kudandia mada bila kujipa muda wa kuona au kusikiliza kitu husika.

Mbona madai ya Mama Salma yako sahihi??

Amesema pension zao za kazi ambazo walikuwa wanafanya kama watumishi wa Umma wapatiwe, akaenda mbali kwa kutolea mfano yy alikuwa mwalimu akisema mara baada ya mumewe kuwa Rais aliachishwa ile kazi lkn hakupata stahiki zake kama ilivyotakiwa kwa mtumishi wa Umma pindi anapostaafu.

Kwanini sisi watanzania ni wajinga wa kudandia vitu na kuanza kulaumu bila kuelewa kitu chenyewe??
Pension gan anataka akwende huko!

Marupurupu yote yale ya u-first lady bado anataka tena?

Tena huyuu! Ngoja!

Na yale madawa wanayouza yeye na familia yake ya mizoga tutaheshimiana tu!!
 
Hivi huyu mama ni kwanini hatosheki?

Mume wake amekuwa Rais kwa vipindi viwili.

Hivi sasa yeye na mwanawe Ridhiwani wanakinga shilingi zaidi ya milioni 12, kwa kila mmoja kwa kuwa waheshimiwa wabunge.

Mzee Kikwete naye anakinga 80% ya mshahara aliokuwa anapata kama Rais.

Familia ya aina hiyo bado tu anataka na mafao ya pension ya mke wa Rais mstaafu?

Hakika Hawa viongozi wa CCM ni wanyonya damu za watanzan

Hivi huyu mama ni kwanini hatosheki?

Mume wake amekuwa Rais kwa vipindi viwili.

Hivi sasa yeye na mwanawe Ridhiwani wanakinga shilingi zaidi ya milioni 12, kwa kila mmoja kwa kuwa waheshimiwa wabunge.

Mzee Kikwete naye anakinga 80% ya mshahara aliokuwa anapata kama Rais.

Familia ya aina hiyo bado tu anataka na mafao ya pension ya mke wa Rais mstaafu?

Hakika Hawa viongozi wa CCM ni wanyonya damu za watanzania!
Swali dogo tu la kizushi yeye si alikuwa first lady analala na mh rais kitanda kimoja kwanini akumshauri mumewe mda ule atekeleze kile ambacho yeye anadai Leo bungeni

.ukiwaza sana unapata jibu mama kakurupuka kuongea akupanga kajinukia tu ili aongee asikike kuwa naye aliongea

Hapo alipo pamoja na ubunge ana walinzi kama wote analindwa as first lady mstaafu anataka Nini uyu mama kama siyo uchawi huo
 
Jk ndiye alieiletea laana nchi hii! mnaomtetea huyo mama msituone sisi mabwege, amesema wazi kabisa kwamba wapewe pension kama first ladies na sio kama wastaaf! Kweli binadam hatosheki.
 
Kwa kweli nilishtushwa Sana niliposikia mama Salma Kikwete, akilitumia Bunge la Jamhuri ya Tanzania, badala ya kuongelea Shida za watu wa Jimbo lake la Mchinga, anaongelea mambo yake binafsi.

Eti anataka yeye kama mke wa Rais mstaafu, naye alipwe pension!

Hivi hawa viongozi wa CCM wanatuonaje watanzania?

Hivi Katika kipindi kama hiki, ambacho Taifa linapitia Katika kipindi kigumu mno cha uchumi, kwa kupanda bei kwa kila kitu, kutokana na kupanda Sana kwa bei za mafuta, wakati kipato cha mtanzania hakijaongezeka, hivi ni wakati sahihi wa kutumbukiza maoni binafsi ya kuomba kulipwa pension kwa ajili tu ya kuwa ni mke wa Rais mstaafu?

Hata hivyo nimuulize mama Salma, hivi hatosheki na kipato anachopata cha maslahi ya ubunge wa "kupewa" wa kipato cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ukiacha maslahi mengine ya Mheshimiwa mbunge, kama vile "seating allowance" ya kila kikao cha Bunge kinavyoendelea?

Hebu nimuulize tena mama Salma, hivi haridhiki na pension anayolipwa mumewe, Jakaya Kikwete, ya kuwa Rais mstaafu, ambayo ni 80% ya mshahara aliokuwa akiupata alipokuwa Rais wa nchi hii?

Hebu pia nimuulize mama Salma, hivi haridhiki na "upendeleo" aliopewa mwanaye Ridhiwani Kikwete, ya ubunge, ambapo pia "amezawadiwa" u-Naibu Waziri, ambapo anapata maslahi kibao?

Hivi mama Salma, hayaoni matatizo ya mamilioni ya watanzania, wanaohangaika kila kukicha, kutafuta riziki zao za kila siku, ambao hata wakifika umri wa uzeeni hawalipwi pension yoyote?

Hivi mama Salma, hayo uliyoyaongelea Bungeni, ndiyo mawazo ya wapiga kura wako wa Jimbo la Mchinga, waliyokutuma uwasemee?

Hakika baada ya kusikia kauli za mama Salma, alizozitoa Bungeni, nmeamini kabisa, kuwa hatuna wawakilishi wa wananchi huko Bungeni, bali tuna viwavi wa CCM wanaotaka kula kwa kuvimbiwa na watuache watanzania tukiwa hatuna kitu kabisa!

Nimeamini kuwa nchi hii kuendelea kuwachagua wawakilishi toka chama tawala cha CCM ni kuendeleza laana, ambayo itaendelea kututafuna kwa vizazi vingi vijavyo!
Mama Salma ni mzigo.
Kaisha chafua hali ya hewa!
 
Nilichomwelewa ni kwamba anadai kabla ya waume zao kuwa viongozi wakuu (rais, vice & waziri mkuu) walikuwa na ajira zao. Baada ya waume zao kupata nyazifa za juu, walilazimika kuacha kazi zao na kufanya majukumu kama wake wa viongozi wakuu.

Sasa point yake ni haki ya mafao yao ya kazi walizokuwa wanafanya mwanzo ndo wanazitaka😎😎😎
alikua mwalimu wa std 1 na 2.kwamba ndo apewe hayo mafao?
 
Mkuu pension ni haki yao kabisa, Alikua ni mtumishi wa Umma miaka yote kabla ya kuwa mke wa kiongozi

Kwa nini asipate stahiki zake.?
Ana shida zake binafsi, na ndugu anaoweza kuwsaidia, kumbuka anachopata mme wake sio anachopata yeye
 
Kwa kweli nilishtushwa Sana niliposikia mama Salma Kikwete, akilitumia Bunge la Jamhuri ya Tanzania, badala ya kuongelea Shida za watu wa Jimbo lake la Mchinga, anaongelea mambo yake binafsi.

Eti anataka yeye kama mke wa Rais mstaafu, naye alipwe pension!

Hivi hawa viongozi wa CCM wanatuonaje watanzania?

Hivi Katika kipindi kama hiki, ambacho Taifa linapitia Katika kipindi kigumu mno cha uchumi, kwa kupanda bei kwa kila kitu, kutokana na kupanda Sana kwa bei za mafuta, wakati kipato cha mtanzania hakijaongezeka, hivi ni wakati sahihi wa kutumbukiza maoni binafsi ya kuomba kulipwa pension kwa ajili tu ya kuwa ni mke wa Rais mstaafu?

Hata hivyo nimuulize mama Salma, hivi hatosheki na kipato anachopata cha maslahi ya ubunge wa "kupewa" wa kipato cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ukiacha maslahi mengine ya Mheshimiwa mbunge, kama vile "seating allowance" ya kila kikao cha Bunge kinavyoendelea?

Hebu nimuulize tena mama Salma, hivi haridhiki na pension anayolipwa mumewe, Jakaya Kikwete, ya kuwa Rais mstaafu, ambayo ni 80% ya mshahara aliokuwa akiupata alipokuwa Rais wa nchi hii?

Hebu pia nimuulize mama Salma, hivi haridhiki na "upendeleo" aliopewa mwanaye Ridhiwani Kikwete, ya ubunge, ambapo pia "amezawadiwa" u-Naibu Waziri, ambapo anapata maslahi kibao?

Hivi mama Salma, hayaoni matatizo ya mamilioni ya watanzania, wanaohangaika kila kukicha, kutafuta riziki zao za kila siku, ambao hata wakifika umri wa uzeeni hawalipwi pension yoyote?

Hivi mama Salma, hayo uliyoyaongelea Bungeni, ndiyo mawazo ya wapiga kura wako wa Jimbo la Mchinga, waliyokutuma uwasemee?

Hakika baada ya kusikia kauli za mama Salma, alizozitoa Bungeni, nmeamini kabisa, kuwa hatuna wawakilishi wa wananchi huko Bungeni, bali tuna viwavi wa CCM wanaotaka kula kwa kuvimbiwa na watuache watanzania tukiwa hatuna kitu kabisa!

Nimeamini kuwa nchi hii kuendelea kuwachagua wawakilishi toka chama tawala cha CCM ni kuendeleza laana, ambayo itaendelea kututafuna kwa vizazi vingi vijavyo!
Mfumo CCM, bila kuondokana nao hatupo salama.
 
Hivi huyu mama ni kwanini hatosheki?

Mume wake amekuwa Rais kwa vipindi viwili.

Hivi sasa yeye na mwanawe Ridhiwani wanakinga shilingi zaidi ya milioni 12, kwa kila mmoja kwa kuwa waheshimiwa wabunge.

Mzee Kikwete naye anakinga 80% ya mshahara aliokuwa anapata kama Rais.

Familia ya aina hiyo bado tu anataka na mafao ya pension ya mke wa Rais mstaafu?

Hakika Hawa viongozi wa CCM ni wanyonya damu za watanzania!
CCM ni laana kubwa sn kwa nchi hii. Imeinajisi hii nchi vya kutosha!
 
Back
Top Bottom