Mama Salma Kikwete, kutaka wake wa viongozi wakuu wapewe pension ni kumkufuru Mungu!

Sijawahi fungamana na upande wowote wa siasa. Maana waliopo siwataki na wanaotaka kuja siwaamini. Ila tuwe tunasikiliza na kuelewa, si ajabu hujamsikiliza umesoma tu kilichoandikwa ukachanganya na emotions

Msikilize hapa

 
Huyu mabeho yuko wapi aichukue hii nchi tumechoka na dhihaka.

Na ukifuatilia atakuwa na penshion ya ualimu.

Japo Magu aliniumiza ila ni bora angekuwepo.
 
Sijawahi fungamana na upande wowote wa siasa. Maana waliopo siwataki na wanaotaka kuja siwaamini. Ila tuwe tunasikiliza na kuelewa, si ajabu hujamsikiliza umesoma tu kilichoandikwa ukachanganya na emotions

Msikilize hapa

Pamoja na kuisikiliza hiyo clip, bado hujaniwashawishi kuwa huyo mama alichoongea ni cha maslahi ya Umma.........

Mimi nitaendelea kuamini kuwa alichoongea ni cha maslahi yake binafsi na ya familia yake.
Full Stop 😃
 
Ajabu sana.

Inashangaza pale ambapo familia kama ya Kikwete inakuwa bado na mawazo ya pensheni. Hawa ambao kwa nafasi zao kama wastaafu wanalipwa asilimia 80 ya mshahara anaoliopwa Rais aliyepo madarakani, na vitu vingine vyote kwao ni bure.

Huku upande wa pili kuna familia ya mstaafu ambaye bado hajaanza kulipwa mafao yake zaidi ya mwaka mmoja, ana watoto watatu waliomaliza vyuo bado hawajapata ajira, anajilipia bili za umeme, nyumba na maji, na bado makato ya tozo yako juu yake.
 
yani yule babu yangu wa msoga ana miaka zaidi ya 70 na more than billions in the account.

Hivi kweli mtu hutosheki kuwa umekula nchi kiasi hiko mpaka wife akaropoke huko kiwa anataka vimillion kadhaa vya pension ya utumishi aliokuwa anafanya ??

kwanini asielekeze ziende hata charity kwenye shule ambazo hazina madawati jimboni kwake.
 
We ni fala, nenda kamsikilize utaelewa, sio unaanzisha uzi kijinga kiasi hiki wakati hujamsikiliza, amesema wazi hawapewi hayo mafao pale wanapoachishwa kazi zao ambazo walikuwa wanafanya.
Hakuna ufala wowote hapo, wanatakiwa wajisimamie kwenye biashara zao kama ambavyo wengine wanajisimamia, wasiwe wategemezi wa kodi za masikini.

Pesa zote wanazolipwa kama wastaafu serikalini asilimia 80 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, huduma zote za bure wanazopata, posho na mishahara wanayopokea bungeni, bado unawatetea hawa?

Kubali tu, hapo hakuna kiongozi, tuna mtu asiejielewa aliyepewa ubunge wa viti maalum kama zawadi tu.
 
Tuanze kwanza orodha ya wake was viongozi wastaafu.
1.Mama Sokoine
2.Mama Bilal
 
Pension gan anataka akwende huko!

Marupurupu yote yale ya u-first lady bado anataka tena?

Tena huyuu! Ngoja!

Na yale madawa wanayouza yeye na familia yake ya mizoga tutaheshimiana tu!!
 

Swali dogo tu la kizushi yeye si alikuwa first lady analala na mh rais kitanda kimoja kwanini akumshauri mumewe mda ule atekeleze kile ambacho yeye anadai Leo bungeni

.ukiwaza sana unapata jibu mama kakurupuka kuongea akupanga kajinukia tu ili aongee asikike kuwa naye aliongea

Hapo alipo pamoja na ubunge ana walinzi kama wote analindwa as first lady mstaafu anataka Nini uyu mama kama siyo uchawi huo
 
Jk ndiye alieiletea laana nchi hii! mnaomtetea huyo mama msituone sisi mabwege, amesema wazi kabisa kwamba wapewe pension kama first ladies na sio kama wastaaf! Kweli binadam hatosheki.
 
Mama Salma ni mzigo.
Kaisha chafua hali ya hewa!
 
alikua mwalimu wa std 1 na 2.kwamba ndo apewe hayo mafao?
 
Mkuu pension ni haki yao kabisa, Alikua ni mtumishi wa Umma miaka yote kabla ya kuwa mke wa kiongozi

Kwa nini asipate stahiki zake.?
Ana shida zake binafsi, na ndugu anaoweza kuwsaidia, kumbuka anachopata mme wake sio anachopata yeye
 
Mfumo CCM, bila kuondokana nao hatupo salama.
 
CCM ni laana kubwa sn kwa nchi hii. Imeinajisi hii nchi vya kutosha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…