Mama Salma Kikwete, kutaka wake wa viongozi wakuu wapewe pension ni kumkufuru Mungu!

Halafu kijana anaetoka Chuo anaambiwa aji Ajiri serikali haiwez muandalia Ajira Ila mke wa Rais anaomba awekewe na sio kuwekewa mazingira ila hadi sheria itungwe kweli?
Yani wanashindwa kutunga sheria ya Vijana wanaotoka chuo wapatiwe Ajira wanataka sheria za wao kuendelea kunufaika?
 
Nafkr kikubwa alipwe alichochangia mifuko ya hifadhi km raia wengine

Kando ya hapo
Mafao ya mwenza yamstiri
 
Huyu mabeho yuko wapi aichukue hii nchi tumechoka na dhihaka.

Na ukifuatilia atakuwa na penshion ya ualimu.

Japo Magu aliniumiza ila ni bora angekuwepo.
Huyo Magu si ndiyo aliwajengea majumba ya kifahari? Nchi masikini kama hii inamudu vipi kujengea marais wastaafu ambao tayari wameshatajirikia madarakani majumba ya kifahari?
 

Mama Salma Kikwete, ana elimu gani?​

 
MAADUI WA MAGUFULI NDIYO MAADUI WA TZ na maadui wa magu ni TEAM MSOGA AMBAO NI UKOO WA KIKWETE NA MSKAMBA NA NAPE NA UKOO WA ROSTAM AZIZI
 
Hao wamekula,wamevimbiwa,sasa wanatutapikia miguuni,huyu mama bila kuolewa na Raisi,angekuwa danga tu mtaani,maana taahaluma yake ni ualimu,sasa ameukwaa ukwasi,kila akigeuka kushoto kulia,anaona fedha za kupiga,Alipiga fedha za WAMA,sasa huyu kila kitu kakipata kiulaiini,haoni shida za wananchi,maana hata huo ubunge hakuutafuta amepewa tu on silver player,haitaji wananchi kuwa bungeni,
Yeye anajiona yeye na jamaa zake na fulsa kibao za kuiba pesa ya umma kwa mbinu zozote za kijambazi.
 
Pension ya nini wakati serikali imeweka utaratibu wa kuwaudumia mpaka kifo kiwakute na kuzawadiwa jumba moja matata sana. Akubali kama wanataka pension tuwaondolee uduma wanayopata bure
 
Kwahiyo asipewe pesa zake za pension ya kazi yake ya Ualimu??
 
Mkuu pension ni haki yao kabisa, Alikua ni mtumishi wa Umma miaka yote kabla ya kuwa mke wa kiongozi

Kwa nini asipate stahiki zake.?
Ana shida zake binafsi, na ndugu anaoweza kuwsaidia, kumbuka anachopata mme wake sio anachopata yeye
Watu wanakaza ubongo tu, ila mama yuko sahihi sana. Wapewe stahiki zao za utumishi wa umma
 
Watu wanakaza ubongo tu, ila mama yuko sahihi sana. Wapewe stahiki zao za utumishi wa umma
Umejiuliza kuna maelfu ya wastaafu wangapi, wanaohangaikia mafao yao, ambayo ni kiduchu tu, lakini hawayapati?

Badala yake wanaishia kufa, kabla hawajaambulia hayo mafao yao ya kustaafu?

Huyo mama, pamoja na yeye kupewa "ulaji" wa ubunge na mwanaye naye "kuzawadiwa" ubunge/u-Naibu Waziri na Mzee Kikwete kulamba pension, ambayo ni 80% ya mshahara wa urais wakati akiwa madarakani, bado tu hajatosheka tu huyo mama??
 
Pension ya nini wakati serikali imeweka utaratibu wa kuwaudumia mpaka kifo kiwakute na kuzawadiwa jumba moja matata sana. Akubali kama wanataka pension tuwaondolee uduma wanayopata bure
Ndicho Mama Samia alichoongea, kuwa wale kwa mujibu wa urefu wa kamba........

Sasa wao wanataka kutuchuna watanzania, Hadi watuache mifupa mitupu? 🥺
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…