Mama yangu alifariki huku akijua simpendi

Acha kusingizia ukamilifu
Kuna vitu vingine havihitaji hata maelezo vinahitaji umakini mkubwa hasa wazazi .

Kwanini hukuja kuomba msaada mwanzo ukaamua mwenyewe?
Sasa utaambiwa nini tuku comfort na mzazi ameshakwenda?
hongera mkuu
 
Hii post yako imenisaidia sana
Mama yangu nilimzika mwenyewe na alifariki akiwa na furaha na amani kubwa sana. Alinipatia baraka.

Baba huwa ana roho mbaya sana...to the extent nilitamani mama yangu abaki atangulie baba...! Baba ni mbinafsi na always ananiombea mabaya. Nikifanikiwa hana raha na atafanya juu chini kunishusha.
Ila kwa post hii sitafunga mwaka bila kwenda kwa baba yangu kujishusha na kumuomba msamaha hata kama amekosea yeye. Ila ukaribu wa sana sitaupenda.
 
hivi inakuwaje mtu usimpende mzazi wako? hivi unajua mzazi asipokubariki hata wewe huwezi kuwa na baraka kwa ajili ya watoto wako?
 
what if ikawa ni zaidi ya kunitoa uhai?

usijione mkamilifu mkuu usijikute unaakili sana kuzidi engine maisha haya ni mapito


Kuna kosa kubwa zaidi ya kifo??, au alitaka kukufanya msukule??!!-- hayo mambo yapo kwa baadhi ya wazazi.
 
hivi inakuwaje mtu usimpende mzazi wako? hivi unajua mzazi asipokubariki hata wewe huwezi kuwa na baraka kwa ajili ya watoto wako?


Mimi nadhani hakuna haja ya kumlaumu huyu ndugu kwani wazazi wetu wanatofautiana, hatujui ni kitu gani kibaya huyo ndugu alifanyiwa na Mama yake na ni hapo tu wengine tunashindwa kutoa ushauri.
 
Mama ni mama tu, lazma alikata roho akiwa amekusamehe kwa ulchokuwa unamfanyia, nenda katubu naamin utakuwa na aman moyon
 
Hujaeleza sbb za kumchukia lkn
 
Asante sana Nakadori

Nimetimiza miaka 77 majuzi tu hapa. Nimeona mengi kidogo kuliko ninyi vijana.

Ndiyo. Pamoja na kwamba mzee ana hayo matatizo, kama kweli ni baba yako wa damu deep down anakupenda sana. Siku anakata roho kama utakuwa karibu naye si ajabu akakuomba msamaha. We anza right away kwa kumsamehe na kumtakia mema.

Wajua nini? You can break him kijanja tu. Kimatani matani tu mwambie we baba najua hunipendi hata sijui nilikukoseaga nini. Unaniangusha sana dad maana mi nakupenda sana. Mpe kielfu hamsini chake halafu sepa!

Na mara moja kila mwezi mpigie tu na kumsalimia. Baba nilikuwa namwomba Mungu hapa basi Roho Mtakatifu akaniongoza nikuombee. Nakupenda sana babangu. Na ukiwa na kielfu 20 mrushie hata kama ana hela zake anajitegemea.

Utaona!

Lakini kamwe usikubali akaja kukata moto wakati mna mahusiano mabaya.

Wabeja
 
Mama ako kukubeba tumboni miezi tisa ni upendo wa ajabu kwako.hakuna wa kufananisha nao.
Alipitia mengi mazito kwa ajili yako.
Hata akosee nini kikubwa kiasi gani.hukupaswa kumchukia hata siku moja.
Unaambiwa mzazi hakosei.
Binadamu sio mkamilifu,kuna muda anakosea

Mzazi hakosei kivipi?ama mzazi tunamtoa kwenye kundi la binadamu?

Wazazi wanazinguaga kinyama tu,wewe sema hatutakiwi kuwa na chuki kama ya mleta mada
 
Fanya hivyo utakuja kushuhudia hapa, Mungu atafungua milango ya baraka hadi utashangaa mwenyewe.
 
Mwandikie barua!
Andika kila ulichotamani asikie kuwa ni hisia zako.
Mweleze kila ulitaamani ajue hasira yako
mwambie alipokosea
mwambie ulivyoumia
mwambie ulivyokuwa na hasira nae
mwambie umemsamehe
mwombe akusamehe kwa kushindwa kuzungumza nae mpk anakata roho
mwambie unatamani mnegeweza kurekebisha kabla hajafa
Talk to her!
ANDIKA!
Ukimaliza nenda kaburini kwake, read that letter .
kisha ichome moto!
Utamake peace with her.
Utaface your fears
Utamface yeye kimawazo.
Inawea kukusaidia, it helped me facing my past demons!
 
Huwa hata umpe nini ana dharau sana
Me ninachotaka kufanya ni kumuomba msamaha then niwe namsalimia mara moja moja maana hata kabla mama hajafa alinambia nitengeneze amani na baba kwakuwa ndie baba yangu bila kujali madhaifu yake.
 
katuokoa wengi kwa kweli abarikiwe sana
 
kuna mambo hua inapaswa kuyarekebisha before its too late
 
asante mkuu
 
Binadamu sio mkamilifu,kuna muda anakosea

Mzazi hakosei kivipi?ama mzazi tunamtoa kwenye kundi la binadamu?

Wazazi wanazinguaga kinyama tu,wewe sema hatutakiwi kuwa na chuki kama ya mleta mada
kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…