Mama yangu angeni-abort wakati bado niko tumboni mwake, angekuwa amenifanyia wema mkubwa sana

Mama yangu angeni-abort wakati bado niko tumboni mwake, angekuwa amenifanyia wema mkubwa sana

Nini kifanyike sasa
Ni kumuomba Mungu akupe njia bora na faraja pamoja ,kutubu na kujitakasa kama una muamini Yeye.

Hatua ya pili ni kuamka kuangalia wapi ulipokosea na kupambana kwani hata ulie ,ulaumu ,ujiue ,unywe mapombe bado haitasaidia kitu na jua linaendelea kuchomoza mashariki na kuzama magharibi bila kujali kuwa wewe umekaa na haupo comfortable
 
Kama hizi za Kumb 28?
"63 Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki. 64BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. 65Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini BWANA atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; 66na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; 67asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona"

Siku zote usipomtii BWANA Mungu kuna madhara, uwe Myahudi au Mtanzania!


Katika hiyo kumbukumbu hayo maneno anaambiwa myahudi au Mtz??
 
Akili hiyo ni ma genius tu tunao weza kukubaliana nayo na kukuelewa ...mimi nikimwona mtoto mdogo anakufa huwa namwonea wivu sana.

Genius ni yule anayejua kusudio la maisha yake hapa duniani.
 
Mama yangu angenitoa na kunitupilia mbali kipindi bado niko kwenye tumbo lake la uzazi, ingekuwa ni faida kubwa sana kwangu, ningejihesabia mwenye bahati sana, sababu nisingekuwa na haja ya kuja Duniani na kupitia mateso, usaliti, hofu, Karaha za kila namna, magonjwa, e.t.c kisha mwisho wa siku dini zinakwambia ukiteleza kidogo kwenye dhambi unaenda kuchomeka motoni milele baada ya kufa.

Kutokana na maisha na majaribu tunayopitia hapa Duniani, sisi binadamu uwezekano wa kwenda motoni baada ya kifo ni mkubwa kuliko kwenda mbinguni. Hii Dunia sio nzuri kabisaaaa, kiuhalisia ni mbaya mno na inatisha sana.

Kungekuwa na uchaguzi wa kuja Duniani au kutokuja duniani kabla ya kuzaliwa, mimi ningekataa katu katu kabisa kuja Duniani.

Najiuliza Mungu anafaidika nini kwa kutuumba sisi binadamu? Alivyotuumba amefaidika nini, na asingetuumba angepungukiwa nini? Yeye si muweza wa yote, amejikamilisha kwa kila kitu? Anatuhitaji sisi binadamu kwa ajili gani? Je, anafurahi sana kuona binadamu kila siku tunavyomkasirisha kwa dhambi, tunavyoteseka na tunavyorukaruka na sarakasi za hapa Duniani?

NB: Sina mawazo ya kujiua, na kwa sasa sina shida kubwa sana ninazopitia, maana kutokana na hii post kuna wengine watafikiria nitachukua maamuzi hayo ya kujiua, wengine watafikiria sasa hivi nina matatizo makubwa sana napitia ndio maana nimeandika hii post, la hasha, siwezi jiua maana najua ntakakoenda baada ya kujiua ni kubaya zaidi ya hapa Duniani. Mimi nimewaza tu.
Kupanda kwa gharama za maisha kumesababisha watu wajute kuishi🤣🤣🤣🤣
 
Hii inanikumbusha movie ya Capernaum, dogo aliwashitaki wazazi wake kwa kumzaa!.. 😢

movies_capernaum-web.jpg
 
Balqior ulishaabortiwa na mama yako mzazi mkuu ukapewa chance ya pili ndo huyo mama msamaria akakuzaa
 
Ukipitia msoto flani haya mawazo yanakujaga sana 😂😂😂
Ndo mana mnanda waliimba " nikifikiria dunia mwenzenu najijutia nawahi kukufuru Mungu kwanini nilizaliwa!!!
 
Wewe siyo kundi la magenius hivyo uwezi kuelewa hiyo ni akili kubwa sana.


Kwahiyo kundi la magenius ni nyie mtoto akifa mnamuonea wivu??!!---kwahiyo mtoto wako akifa utalia kwa uchungu wa kufiwa au utamuonea wivu kwa kufa kwake??!!, ewe Genius hebu jibu hapo!🤣
 
Nakubali kabisa, dini zinatutaka tujione wenye bahati kuja duniani.

Unajiuliza bahati gani kwa ugumu huu? Tusingezaliwa tungepata shida gani?
 
Back
Top Bottom