Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha mimi mwenyewe kwa mara ya kwanza walinishangaza na hiyo salamu yao ya "Good Morning" eti kwa vile imeenea sehemu mbalimbali duniani kama kwako ni mchana kwa wenzako ni asubuhi.Hawana lolote zaidi ya utapeli na ile salamu yao ya 'good morning " hata kama ni mchana au jioni huwa siielewi.
Kabisa, wadhibitiwe, ila shida ni wale ambao wameshajiunga, ndio wanaifanyanya iendelee, maana wanahangaika kugomboa fedha zaoQNET ni wafanyabiashara wenye sura ya kitapeli ambao wanauza bidhaa za mtandaoni. Ubaya wa hii biashara ni huu hapa:
1. Watu wanaokutaka ujiunge kwenye hii biashara wanakupotezea muda wako wa kuhudumia wateja na jamii kwa kukuzonga kwa maneno mengi sana yanahusu kuachana na umaskini.
2. Mchakato wa kujiunga na Qnet utakuchukulia muda wako mwingi sana
3. Ukishajiunga na QNET Mchakato kutafuta wateja wapya wa kujiunga na QNET ili ukomboe hela yako utakuchukulia muda mwingi na utawachukulia watu wengine unaotaka kuwaunga muda wao mwingi sana pia. Hivyo kazi za mwajili na kazi zako zitazorota wakati wa harakati za kuingiza watu
4. QNet watakuuzia bidhaa ambayo huitaki kwenye malengo yako ila utalazimika kuinunua tu kama kiingilio kwenye biashara yao kwa ahadi ya kupata faida kubwa sana kupitia qnet.
5. Qnet watakushauri uache kazi ya mwajili ili ufanye kazi ya kuwatafutia wateja wapya. Hapa nimeona madaktari, manesi, walimu, wakiacha kazi zao ili wafanye kazi ya kukimbizana na wateja, wale ambao hawajaacha kazi wanageuka wababaishaji kazini na kuwapotezea muda wafanyakazi wenzao wajiunge nao.
6. Qnet hawatoi risiti, hivyo hatujui serikali inapataje kodi yake, VAT, holding tax
7. Qnet inawawinda wastaafu kwakuwa wanafahamu wamepata hela ya mafao, hivyo ni rahisi kutoa kiingilio.
8. Qnet wanakushawishi kwa nguvu uache miradi yako mingine ili uhamishie hela na muda wako kwao
9. QNET wanawawinda watu muhimu kwenye jamii ambao wanaheshimika kujiunga ili kuwavuta watu wa kawaida kujiunga nao
10. QNET inatumia vishawishi kama picha za magari, nyumba, boti, ndege ili kuwa kama chambo cha kukunasa ujiunge.
11. QNET inakufundisha namna ya ku manipulate watu kujiunga na Qnet
12. QNet watakupigia simu kila wakati hata usiku wa manane kukushawishi ujiunge
13. Qnet utawakusanyia sh. 72,000,000 wewe wanakupa faida ya dola 200 sawa na shilingi 460,000
QNET kama ikiachiwa iendelee kama ilivyo sasa kuna kitu kibaya kwa watu, familia, waajili, jamii na serikali kitatokea.