Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Pole sana, mimi nimetumia sana eBay sijawahi kupigwa,kwa uzoefu wangu mara nyingi sisi wanunuzi ndio tunakosea wakati wa ununuzi.
Mimi nanunua bidhaa nyingi kwa ajili ya biashara unanunua mfano ktk mwezi product 50, zinakufikia 30. Tena kwa maseller walewale nimeachana nao. Bora AliExpress na Amazon
 
AliExpress , eBay ndio kabisa na nimeacha kutumia.
Pole sana mkuu. Kila kitu duniani kina pande mbili. Pengine hukuwa na taarifa za kutosha wakati unatepeliwa. Aliexpress huko ambako we umetapeliwa, mi kunaniweka mjini. Hata simu tu nnayoandikia hapa nimeitoa huko.

Muhimu ni wewe unachagua kuona upande upi katika jambo husika.
 
Mleta mada umeharibu zaidi badala ya kuifanya Qnet ieleweke na watu kuvutiwa kujiunga.
Karibu kila msukule wa Qnet ukimuuliza swali la kimantiki atakimbilia kwenye blah blah za kusema inahitaji uje ufundishwe kwanza, atakuletea vilink vya kuungaunga, atakwambia hii sio zingine nk. Yaani wamekaririshwa matango ya ajabu ajabu mnoo.
 
Unaweza kujificha kwenye kichaka cha kutoa elimu, alafu ukakuta umeharibu zaidi katika kupendezesha mada. Ukiwa na muda, naamini unao wakutosha tafakari juu ya uwezekano wako binafsi wa kumiliki hilo duka la viatu vya 100m Tshs ili utuuzie watanzania.
haya mawazo ya ajabu sijui mnapata wapi. Bahati mbaya unakutana na jamaa waliobahatika kwenda shule, mpaka unapata hasira kuona ujinga unavyokua katika taifa kila siku.
Mkuu nadhani hujaelew au umeamua tu kugoma kuelewa. Nilitoa tu mfano ya mtu anavyoshangaa kuhusu bei ya bidhaa fulani kuwa si ya kawaida na kw saabu hizo akaamua kuita scam kampuni inayouza bidhaa hizo.
Kwa kukujibu wewe ni hivi... Qnet shop lipo for the world na bidhaa zipo za bei mbali mbali hadi kwa kila jamii. Pia sielewi unamaanisha nininunavyozungumzia kumiliki duka la viatu vya milion mia..
Embu jithidi kusoma na uelewe maana ya aandishi. Baki kwenye mada kadri ya uwezavyo.. mashambulizi ya mwili yaepuke jeng hoj yako na tetea hoja yako achana a kusema watu mzee.
Ila usijali taratibu taratibu tutaenda sawa juu ya mada kuwa QNET ni E COMMERCE.
 
AliExpress , eBay ndio kabisa na nimeacha kutumia.
Embu weka bayana ulipigwa na eBay au AliExpress au ulipigwa na supplier fake.
Kwa kifupi ulikuwa ukideal na wahuni ukidhani unadeal na wasambazaji.
Nakushauri tu ukiwa unafanya manunuzi kwa ecommerce kuwa makini na mbinu unayochagua kulipia epuka. T.T pendelea LOC na jitahidi kufany hatua za ununuzi ndani ya mfumo.. kwenye alibaba wana kitu kinaitwa trade assurence...
Pole ni mhimu mno kiwa makini ukiwa online for B2B or B2C.
 
Walimu wamepigwa sana na wameachwa na umaskin wao
Hapa sijakuelewa ni wapi kwenye MADA husika umejikita, hasa unapozungumzia kuhusu upigwaji.
Je walinunua bidhaa na wakawa awajazipata?
Au walinunua bidhaa zikawafiki zikiwa si zike walizozihitaji. Embu niweke sawa kabla ya kukujibu kwa kina.
Naomba uwe ndani ya mada.
Thanks
 
Mleta mada umeharibu zaidi badala ya kuifanya Qnet ieleweke na watu kuvutiwa kujiunga.
Karibu kila msukule wa Qnet ukimuuliza swali la kimantiki atakimbilia kwenye blah blah za kusema inahitaji uje ufundishwe kwanza, atakuletea vilink vya kuungaunga, atakwambia hii sio zingine nk. Yaani wamekaririshwa matango ya ajabu ajabu mnoo.
Nitajitahidi kutokukushambulia wewe kama wewe ingawa kwa namna unavyoandika naamini si mimi tu anayeyasoma na kuyatilia shaka maandish yako. Unadhihirisha kasoro kubwa uliyonayo kwenye swala la kufikiri na kutafakari..
Unaruka ruka sana mzee baba hutulii..
Sipo hapa kushawishi mtu. Nimetoa mada kuelezea QNET ni ECOMMERCE basi. Nimekwmbia uwe na subra.
Mbona watu wanasoma miaka 7+4+2+3= 16 ili tu kuw wataalamu kwa degree kwenye jambo fulani! wewe unashindwa nini kusubiri.
Baki kwwny mada next time nitakuja aeneo yako.
Shukran.
 
Pamoja na mtoa mada kuwa na uwezo mkubwa wa kujibu maswali na kuwa na utulivu wa hali ya juu bado paka muda huu akuna ata mmoja anayemuunga mkono
Kwa vile UZI wangu haukuwa n nia ya kuungwa mkono bali tu ni kutoa maarifa. Naamini maarifa haya yamesaidia baadh ya watu.
Wengi wanaokuja hapa wanakuwa wapo nje ya mada husika ingawa wanahoja nzito na muhimu ambazo nitazielezea vyema kipindi kingine. Na naamini tunaenda nao sawa.
Asante.
 
Mimi nilkarbishw huko pasipo kuelezwa kusudi halisi. aniliambiw kuna fursa ya biashara niende nikasikilize. Nilichojifunza ni kuwa, Qnet ukienda kwao wanakukataza kutafuta habari kwa watu wengine ila kwao tu. Cha ajabu waliojiunga muda mrefu sioni wakitajirika kwa kasi ile wanayoisema kwenye semina zao, zaidi sana naona kama wanapotez matumaini kila siku hata ile mialiko haipo tena siku hizi.
 
Acha mbwembwe scammer
Qnet ni kituo cha mauzo ya bidhaa. Kutohitaji kwako kununua bidhaa fulani kwa umasikini wako kusipelekee kukashifu bidhaa au duka la watu. Yapo magari ya 5mil USD.. (10 billions tsh). Vipi unaweza sema hizo kampuni ni scamm kisa huna pesa?
Bei ya kawaida ni ipi? Au hujui kuwa kun biatu bya milion 100 tsh duniani. W unataka bei ya elfu 30 ya Sinza mori?
Any way ipo siku nitalezea pia hii taharuki kwa mapana yake.
 
Ipo siku ipo siku ipo siku ipo siku . Siku ipi hiyo ?
Sijagusia hili pia kwenye Uzi wangu. Wala sifahamu yupi ni yupi. Yawezekana asiwepo au akawepo but lengo langu lilikua kuelezea Qnet ni E commerce system.
But navutiwa sana na nakuja sababu yako ya kupenda kujua mafanikio ya mjasiriamali fulani ni ipi! Usije ukawa kama walio wengi huafuata mkumbo kwenye kufanya maamuzi kwa sababu ya fulani kapata sana kwenye biashara fulani ngoja na mimi nifanye... hii sio dhana sahihi.. ipo siku nitaelezea hii kasumba na athari zake.
Thanks.
 
Mimi nilkarbishw huko pasipo kuelezwa kusudi halisi. aniliambiw kuna fursa ya biashara niende nikasikilize. Nilichojifunza ni kuwa, Qnet ukienda kwao wanakukataza kutafuta habari kwa watu wengine ila kwao tu. Cha ajabu waliojiunga muda mrefu sioni wakitajirika kwa kasi ile wanayoisema kwenye semina zao, zaidi sana naona kama wanapotez matumaini kila siku hata ile mialiko haipo tena siku hizi.
Je Umesoma UZI wa MADA hii au umekuta watu wamajadili ukaamua tu na wewe ulete story yako mzee?
Embu jitahidi kureply Uzi kulingana na mada iliyopo mdau.
Ingawa yawezekana kabisa next time utajifunza zaidi kwenye maandishi yangu na utagundua nini kilichopelekea wewe kuwa hivyo ulivyo. Kuna jambo la muhimu sana kwenye hadith yako linalotafakarisha.
Asante kwa kushiriki.
 
Back
Top Bottom