Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mmmmh!Kwahiyo leo Mpesa wakitapeli wananchi na kuingia mitini na fedha zao basi ndio imetoka kwa wananchi?Serikali itataifisha hizo pesa na biashara inakuwa imekwisha!
Au bank ikifikisika walio weka pesa kwenye hizo bank nao ni hasara yao? Kuna wateule wa boss wamelewa madaraka.
 
Ile si imesajiliwa kama network marketing? Na Kwa maana hiyo ina link watu mbalimbali ili iweze kukua Na kuwafikia watu kwa mapana. Ipo mifano ya biashara zilizo halalishwa zinazo tumia watu ili kuwafikia watu zaidi.
Sasa serikali miaka sita plus inakusanya kodi bila kufatilia mlipaji wake anaendesha biashara kwa njia zipi mpaka leo ndo wanakuja kutuambia kwamba mlipa kodi wao ni tapeli??? Hilo kwako lina make sense ndugu??
Hawajawahi kulipa Kodi popote na hakuna member aliyewahi kupewa risiti.Hawana EFD machine wala TIN number, hawafanyi biashara yoyote zaidi ya kukusanya ela za mafala. Ukijiunga kurudisha kwako pesa mpaka ulete watu.Na serikali haijawahi kuchukua Kodi yoyote toka qnet. Na ofisi zao zimejificha tu.
 
Wewe ndio hutumii akili kwa mawazo yako haya, ukiwa kiongozi wa serikali kuna mipaka unakuwa nayo, kwa Kingwa kushiriki ufunguzi huku akiwa waziri serikalini inatoa uhalali wa serikali kuhusika kualalisha hii kampuni, pia kibali cha kufanya kazi nchini walipewa na nani? Juzi nilimsikia bosi mmoja Brela akimwambia DC Sabaya kwamba hii kampuni haijasajiliwa Brela, serikali ya kipumbavu kabisa.
Mnapigwa pesa kwa upumbavu wenu mnakuja kulalamikia serikali. Wewe kwa akili yako waweza kununua saa milioni 4 na nusu kisa umemuona Kigwangala kwenye kukata utepe!??.. Akili au matope?, Eti ukileta watu kujiunga ndo unapata pesa, kwa uchumi wa Tanzania wangapi Wana uwezo wa kujiunga kwa milioni 4 na point!?, Tena mi naona wapigwe tu maana hawatumii akili. Serikali ina Mambo mengi ya kufanya sio kudili na wapumbavu.
 
Hawajawahi kulipa Kodi popote na hakuna member aliyewahi kupewa risiti.Hawana EFD machine wala TIN number, hawafanyi biashara yoyote zaidi ya kukusanya ela za mafala. Ukijiunga kurudisha kwako pesa mpaka ulete watu.Na serikali haijawahi kuchukua Kodi yoyote toka qnet. Na ofisi zao zimejificha tu.
1.Nakumbuka siku ya uzinduzi wakati huo mhe. Khamis alikuwa naibu waziri wa afya (sina kumbukumbu vizuri) alihutubia akawa anasema kuwa TFDA pamoja na TBS wote wamejiridhisha na bidhaa zinazo tolewa na qnet, kwa maana hiyo hawa watu tayari walikuwa wanafahamika na taasisi za serikali ambazo ndo serikali yenyewe

2. Kweli kwa popularity ya qnet kwenye mitandao ya kijamii na kuoperate kwa kipindi cha miaka sita na inafanya hivyo serikali ikiwa haina taarifa za usajili??

Mwisho katika majibu yote mawili aidha kampuni kama ilikuwa inalipa kodi basi serikali inafanya wizi AU kama ilikuwa inafanya kazi bila kusajiliwa basi serikali ina uzembe wa hali juu sana.
 
Umechelewa sana ndugu kupata hii fursa yaani kifupi ni utajiri nje nje usipoteze nafasi hiyo adhimu wenzio wanaililia,JIUNGE HARAKA KISHA JIPIGE KIFUANI MARA TATU KISHA SEMA "Mimi ni mpumbavu"
hahahahahahaha wewe ni mjinga sana sina mbavu...
 
Habari wana janvi nilikuwa naomba kupata ufafanuzi juzi ya kampuni ya Qnet jinsi inavofanya biashara na nikweli kuna mafanikio ukijiunga nayo nimekuwa
nikipata ushawishi tika kwa marafuki zangu mbalimbali kujiunga na kampuni hii.
Uwe unafuatilia current news
 
Kuna kuna tapeli mmoja wanaoweka matangazo mjini y KUJIUNGA NA FREEMASON , mganga mama tuva kutoka kigoma baada ya kuhojiwa kuwa anatumia mbinu ya zamani ambayo watu wameshaijua alijibu " WAJINGA WANAZALIWA KILA SEKUNDE"

Huu ujinga wa hawa watu wanaokudanganya kuwa IAM A BILLIONAIRE, GOODMORNING watu walishalizwa sana na hakuna na wameongeza umaskini mpaka serikali imeingilia kati juzi juzi mtu ndio anaibuka leo unataka na yeye apigwe.

Ukiona biashara inayoitwa multilevel marketing, iwe mfumo wa bidhaaa unapewa furushi na madawa , au virutubisho, au tunaweka fedha wanakuambia ukatafute watu wengine ili uwe unapata fedha za gawio nyingi kimbia ufe hiyo ni PYRAMID SCHEME iliyopigwa rangi mpya
 
Watu wa ukumbi huu habarini

Nimeona nije kwa hii inayoitwa QNET kampuni ambayo wanasema kwamba inatoa fursa ya kibiashara kwa watu ulimwenguni.

Binafsi nimehudhuria mikutano miwili ya QNET kupata maelezo mbali mbali kuhusiana na hii biashara lakini nilichokuja kugundua hawa QNET huwatumia hawa mawakala wao kusema uongo kwa watu wasiojua mambo ya bisahara za Online inakuwane, lakini pia kwenye mafunzo yao hulinganisha kama tunavyonunua bidhaa kutoka Ebay, Alibaba nk.

Sasa hapa nimekuja kuonyesha huu udhaifu wa QNET na hiyo mitandao mengine wanayoipigia kelele.

1. Unaponunua bidhaa Ebay kwa mfano hapa nina uzoefu mkubwa kwamba inabidi niongee na seller/muuzaji anayeuza ile bidhaa tena naongea naye binafsi lakini kwa QNET ni tofauti inabidi uongee na kampuni ya QNET kupitia wakala/ ama mteja kama wewe utakayekuwa kupitia duka lake la Online.

2. Ebay tunakuwa na uhuru wa malipo tunalipia kupitia online mimi mwenyewe binafsi baada ya kufanya maongezi na seller nikitaka juu ya ile bidhaa, Lakini QNET inabidi fedha zako milioni 5 labda na laki 2 au 3 (inategemea na rate dola ) umpe mteja kama wewe mkononi akunulie wewe kwenye Kampuni ya QNET kupitia account yake ya online. (Hapa ikumbukwe kwamba unapolipa online siku zote bei za dola huwa zina varies kwaiyo lazima kutakuwa na chenji sina hakika kama wanawarejeshea wale watu walio lipia zile bidhaa chenji iliyobaki.

3. Kwenye Ebay huwa kuna uhuru wa kuchagua bidhaa mbali mbali kwa maelfu na bei tofauti kabisa yaani kuna bidhaa unanunua ata $1 au chini ya $ 1 na kuendelea lakini QNET wao ili ujiunge na ule mradi wao wa ile chain ya mtu 1 kuliani kwako na 1 kushotoni kwako nilazima ununue ile bidhaa kwa milioni 5 labda na laki 2 au 3 huwezi pata chini ya hapo labda watoe ofa huwa inatokea mara chache sana, na bidhaa zenyewe utashangaa wamechagua bidhaa maalum kama water filter, saa ya kuvaa mkononi, mkufu wa dhahabu, bio disk labda na dawa za virutubisho (bidhaa zao ni chache) nje ya hapo huwezi pata bidhaa nyengine. Lakini cha kushangaza zaidi mimi katika maisha yangu sijawahi kwenda dukani nikakuta bidhaa 5 tofauti mwenye duka akanambia zote hizo bei ni moja tu kila ntakachogusa, lazima kutakuwa na tofauti ya bei, lakini swali jengine kwanini hizi bidhaa ni kuanzia milioni 5? ukienda kwenye Ebay ambayo wanailinganisha utakuta haya mambo ni tofauti sana zaidi ya sana.

4. Ebay unaweza nunua bidhaa lakini kama sivyo uliyotaka labda ina kasoro ya kile ulicho ki-brouwse kwenye mtandao unaweza ku complain kwa seller na akakurejeshea fedha zako (refund) na labda bidhaa yake ukamrejeshea itategemea na makubaliano yenu mtakavyoelewana lakini QNET ukishanunua bidhaa hata ije na kasoro gani huwezi ku- complain na hela yako ndio imekwenda wala hakuna guarantee wala chochote ikija bidhaa kama umeipenda ni hiyo kama hujaipenda ni hiyo hiyo (no refund). Binafsi Ebay wameshanirejeshea hela zangu kwa sababu bidhaa niliyonunua waliniletea rangi tofauti na rangi niliyoichagua na kuipenda wakati wa ku-browse mtandaoni.

6. Ebay kuna uhuru ata wa kumpigia simu yule seller mkaongea vya kutosha na ku-bagen yaani akupunguzie bei na sellers wanafanya hivyo ni jambo la kawaida lakini QNET bei unayoikuta kwenye hilo duka la mtu haina bagening, bei zao ni fixed huwezi punguziwa bei ata iwe vipi.

7. Ebay wanakuweka wazi kabisa kwa mfano kipindi hichi cha Corona kwamba bidhaa yako inaweza kuchelewa kufika labida inaweza kuchukua ata miezi 4 kutokana na safari za ndege kupigwa marufuku wakati wa kusafirisha bidhaa yako kwa baadhi ya nchi, sasa kama unataka kuendelea kununua unanunua hutaki unaacha lakini QNET mpunga ukishaupeleka kwa yule wakala yeye kashatia $200 zake mfukoni kwa kila wateja wateja 2 haya ya bidhaa kuchelewa hayajadiliwi tena wala chochote ndio imetoka tena usubiri tu.

8. Ebay na Makampuni mengine kama Alibabab na AliEpress unaweza kujenga urafiki na hawa Sellers japo hamujuani kwa mambo mengine mbali mbali lakini QNET huyo Victor VJ mkuu wa kampuni yao kule China ata hana habari na wewe kabisa wala hana time wewe hoja zako utaishia kwa mteja mwenzako aliyekuunganisha na kukusajili.

9. Ebay na Makupuni mengine unaweza nunua bidhaa kwa ajili ya biashara yaani wanakuletea bidhaa kama ni viatu au spea zikifika hapo ukaweza fanya biashara na kutengeneza faida halafu ukaagiza tena na tena lakini QNET unanunua ile bidhaa kwa matumizi ya nyumbani tu halafu unapatwa na kazi ya kutafuta watu wengine uunganishe.

10. Bei ya bidhaa ya QNET sio bei halisi ya ile bidhaa unayonunua utakuta kama hii water filter inauzwa mpaka Tshs 600,000/= tuseme laki 800,000/= lakini QNET huwezi ipata chini ya milioni 5., yaani hapa mimi nimegundua kwamba hawa QNET zile milioni 5 nyuma ya pazia ni kwamba ni bei ya kujiunga tu na ile kampuni lakini hudanganya na kusema ni bei ya bidhaa mana bidhaa ile ile ukiagiza Ebay basi unaipata kwa bei yenye wastani wa laki 6 au 8 Tshs.

SASA TUJE KWENYE MAMBO MENGINE TOFAUTI NA MTANDAONI:

Ndugu zangu QNET hawa mawakala wao hutumia neno fursa, yaani akija mtu kutaka ujiunge na QNET atakwambia kuna fursa nzuri ya kutengeneza maisha yako kwa muda mfupi sana lakini nataka nikuzindue kitu unapoingia QNET inabidi utoe milioni 5 kununua ile bidhaa na kujiunga lakini ili fedha zako zirudi ni kwamba mpaka uweze kuwashawishi watu wengi kidogo ndio fedha zako ziwe zimerudi kwasababu mpaka unawashawishi watu 16 tu kujiunga QNET tayari kwenye hawo watu 16 QNET kama kampuni washatengeneza milioni 80, wameshatengeneza milioni 80 lakini wewe uliyetoa milioni 5 bado utakuwa umerejesha hela zako kama milioni 3 tu hivi bado una kazi ya kushawishi wengine ili urejeshe pesa zako. Sasa emu niambie itakuchukua muda gani kuwapata watu 2 kushotoni na kuliani kwako lakini itachukua muda gani hao watu 2 nao kupata kila mtu watu 2 kuliani na kushotoni mpaka kufikia hao 16? Utagundua ugumu wa hii wanayoiita fursa ya Kibiashara.

Mimi nilikuwa aproached ni Dr. mmoja anasema yeye alikuwa daktari Muhimbili sasa ameacha kazi kwa sababu QNET imemletea tija mpaka mke wake na watoto wake wako huko QNET, Lakini kuna jirani yangu mmoja hapa amejiunga sasa ana miezi 4 hela yake tu haijarudi alimfata aliyemuunganisha jibu alilompa alimwambia mwanzo mgumu jitahidi, sasa kama mtu aliuza bishara yake ya duka akapata hela ya kujiunga au aliuza ngombe wake au aliacha ajira yake akafuatilia QNET au alitoa msingi wake wa bishara au alienda kukopa mahali hela za kujiunga ndani ya miezi minne hujajeresha hela huyu mtu atakuwa na hali gani mpaka tuiite QNET ni fursa ya kibisahra?

Lakini nimejaribu kufanya research watu wengi waliojiunga na QNET huwa hawasemi ukweli juu ya udhaifu niliouonyesha mara nyingi lugha yao imekuwa ni moja nikawa napata tabu sana kwanini hawa watu wanakuwa hivi lakini nikaja nikagundua kumbe hawa wateja wa QNET ambao tayari washajiunga kumbe huwa wanaitwa na kuhudhuria madarasa mbali mbali ya kufundishwa namna mbali mbali ya aidha kujibu hoja za watu zitakazoibuka juu ya QNET lakini hupewa elimu wao wenyewe bila ya kujijua wakajikuta QNET wanaona ni mpango mzuri sana Lakini cha kushangaza wapo watu ambao nawaona wamejiunga kitambo tena lakini physically sioni maisha yao kubadilika nawaona kawaida tu, anaye kula kwao anakula kwao, anaetembea kwa miguu sijamuona na gari nk.

Binafsi naona QNET kama hakuna budi mtu anataka kujiunga basi awe anazo hizo milioni 5 ambazo haziko kwenye bajeti yake ya maisha na ajaribu kuzisahau au achukulie kama zimepotea tu akiweza fanya hivi hapana budi basi anaweza kujisajili QNET.


Mimi kiimani ni muislamu lakini weakness nilizoziona hapo juu kwa mujibu wa sheria zetu za kiislamu nimejiridhisha kwamba biashara hii haifai, ndani yake kuna shubha na hila nyingi sana hasa hasa muanzilishi wa biashara ni mtu kutoka China na hajaweka wazi kwenye hii biashara wao kama kampuni huwa wanafanya nini na nini yaani sijaona financial details zao, pengine wanachezesha kamari, pengine freemason nk.

Naomba kutanguliza
 
Back
Top Bottom