Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mmi nimekutana nao jana, mshikaji wangu kanipeleka. Ilikuwa saa Saba mchana nikashangaa nilipofika nikashangaa wanasalimiana GOOD MORNING nilishituka Nikawaza labda nipo Dunia Nyingine, lakni haikuwa hivyo nikajisemea moyoni kiingereza kimevamiwa na wahuni. Si nikapewa wasilisho na simulizi zote kuhusu Qnet sikuwa najua hili wala lile. Ukafika mda wa maswali na majibu, unajuwa ilikuwaje? Niliwabana kwenye kodi, nikawabana Faida ya Kampuni iko wapi, pia nikawabana mfumo mzima wa uendeshaji wa biashara ili kampuni iweze kupata faida . Majibu yalotolewa hata sikuyaelewa ikabaki siri yangu
Nikakubaliana nao ili yaishe isijeonekana mimi mkorofi, kitu kingine ambacho sikukielewa na sikutaka kukiuliza ni kwanini wanafanya kama siri hii biashara? Niliwaza na kutafakari nikajisemea hapa hakuna kitu; kusema kweli hawa jamaa wamejipanga kushawishi watu.
Baada ya yote waliniomba nirudi tena siku nyingine kwa ajili ya kupata somo awamu ya pili.
Hapa nawaza Je, nirudi tena nikawasikilize au niwapotezee?
Naomba ushauri wana JamiiForums
Rudi mkuu mimi nilirudi kuwasikiliza baada ya hapo tena watakupigia simu usiku na mchana lakini jamaa nilimtandika hoja akashangaa sana mwisho akanambia nitakuletea bos wangu aje ajibu maswali yako lakini paka leo hajaja ananiona mchungu sana
 
Rudi mkuu mimi nilirudi kuwasikiliza baada ya hapo tena watakupigia simu usiku na mchana lakini jamaa nilimtandika hoja akashangaa sana mwisho akanambia nitakuletea bos wangu aje ajibu maswali yako lakini paka leo hajaja ananiona mchungu sana
Bongo kutapeliwa utake mwenyewe tu
 
Me nishawah kuwachora Sana hao qnet nilienda presentation zote mbil huku nikijua kila kitu basi nikawambia somo nimelielewa sasa ngoja kesho niende bank kuchukua loan alaf niwaletee mzigo bwana bwana weeee

Hiyo cku kuna kidada na jamaa aliyenileta pale wakanichukua na kunipeleka mgahawa fulan saf Sana nikaambiwa agiza unachotaka nikaagiza kyepe na nusu kuku alaf nikaagiza na smainoff moja kubwa ,story zikawa zinaendelea kuwa yaan ww una bahat Sana hapa tayal ushatoboa[emoji23][emoji23][emoji1787]

Basi nikamsosomola yule kuku weee nikatupia na kinywaj changu story ndio zikanoga Zaid had mida fulan wakaniacha na kwenda ofisin kwao na wakanipa naul ten wakat sehem ninayoenda Ni 400 tu basi nikabeba kinywaj changu huyo kwangu huku nimeshiba balaa.

Kesho yake asubuh zikaanza kumiminika cm kuwa niwah bank kufanya process za loan mm hapo nawachora tu ,nikawambia msijar ,kufikia saa tano nikapigiwa cm Tena kuwa tayal ushafika bank nikawambia ndio ila Kuna mambo hayako sawa kwenye nyaraka zangu hivyo natakiwa kwenda mahakaman kwenda kuapa hivyo Kuna gharama Zaid ya elfu hamsin maana kuapa ten na mhuri wa mwanasheria nimeambiwa 40 nikawambia kwasasa Sina hiyo pesa had salary itoke ndio ntarud huku bank [emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]kuprocee .bwana bwana weee wamekutana na mhuni mwenzao.

Si wakapiga simu kuwa usiache bana ngoja ofisi ikusaidie hiyo hela ili ukamirishe huo mchakato na huyo nonayewaeioiana nae Ni yule jamaa aliyenialika pamoja na kile kidada ,nikawambia mtakuwa mmenisaidia Sana maana mwenyew natamani kutajirika haraka Sana.

Jamaa akadai asingekuwa bize angekuja moja kwa moja bank ili tumalize Hilo swala had kwa mwanasheria had mahakaman ivo wakanitumia muamala wa sh 65 kuwa toa 60 alaf 50 maliza Hilo swala alaf ten ya chakula na maji [emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1787] walipotuma tu muda huo nilikuwa kazin hata Kaz ikabid niombe ruhusa kuwa Kuna dharura nikaenda zangu kitaa nikanunua kuku wawil matetea mmoja akachinjwa cku hiyo hiyo mmoja nikamrushia kwenye Banda la kuku Kama kumbukumbu so akaenda kuongea idad ya kuku niliokuwa nao mwanzon .Nikachukua kvant kubwa na juice kubwa kwa ajil ya mama shemej yenu yeye hanywi pombe.

Bwana weee jion nikapigiwa cm vipi ushamaliza nikawambia kila kitu tayal nasubir mzigo uingie tu niwaletee nasi cku ya Kwanza ya pili wakapiga Tena cm nikawambia nimeambiwa ntapata pesa had zipite cku tano.

Sasa walipojichanganya si wakapiga cm kwa ofisa mikopo kuwa bwana mbona unamcheleweshea mteja wetu pesa yake tunakuomba mfanyie haraka aipate hata leo leo,yule afisa mikopo akauliza jina anaitwa Nan maana hapa wanakuja wengi ,si wakataja jina yule afisa akawambia huyo jamaa hajawah kopa hapa na taarifa zake hazipo hapa [emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Jamaa akanipigia cm kuwa mbona umetudanganya na lawama kibao aiseee nilimfungukia balaa shit za kutosha akaanza lawama sijui umepishana na utajir lakin utaona maendeleo yangu baada ya mwaka mmoja nikamjib sio lazima wote tuwe mataita Nan sasa atamtumikisha mwenzie?

Mara basi rudisha gharama zetu nikamwambia niliwaomba au nyie mlinipa kwa hiari yenu basi akawa mpole tu ,tukikutana kitaa hakuna Salam wala Nini na hapo nikawa nishapiga loss kwenye laki moja ivi.

Maisha yakasogea wee saiz Ni mwaka na nusu umepita naona mtu Hali yake inazid kuwa mbaya Zaid kauza pik pik kauza vitu vya ndan had mke wake aliamua kurud kwao ,aliuza had boma la nyumba ,Sasa mm tukikutana kwa Sasa Nampa Salam kizush tu lakin anajisikia aibu balaa.

Hiki ndio kiss changu na hao watu wa qnet
Hahahah uko vzr
 
Salaam wakuu! Mimi ni mwanachama mpya hapa JF!

Nimekuja hapa kwenu kuomba msaada kama kuna mwenye kazi au connection popote anipe wakuu! Nina elimu ya darasa la Saba!

Sikutegemea kuwa hapa Ila kilichonileta ni hiki hapa nakisimulia japo itaweza kuwa ndefu na pia pengine sitaipangilia vizuri! Penye ufafanuzi nitatoa hata kwenye comments!

Nilikuwa Morogoro nikifanya shughuli Fulani ambayo ilifikia kikomo ikaisha!
Kutokana na uhitaji wa Ajira, kuna Jamaa yangu alikuwa hapa Dar (akiwa kama mwalimu).

Baada ya kuwa nawasiliana nae na kumwambia anipe connection hata ya kazi yoyote halali hapa jijini, akaniambia Nije bila shida. Ahadi hii ya kunishauri nije aliniambia kama wiki iliyopita ambapo Mimi nilimwambia toka mwezi uliopitia.

Sasa baada ya juzi kunipigia simu Rasmi akanipigia akinisisitiza kuwa nije haraka iwezekanavyo maana kuna kampuni inataka watu kama watano na akasema Mimi ni miongoni mwa aliowaombea nafasi hivyo nifanye juu Chini Ijumaa (Jana) Saa NNE asubuhi nifike bila kukosa na natakiwa niwe na angalau kiasi cha pesa cha shilingi 150,000/= Kwa ajili ya mambo kadhaa ambayo hakutaka nifahamu ni ya nanna gani.

Nilijaribu kumdadisi hasa Kwa kila ninalopaswa kufahamu Ila akanisisitiza kuwa mambo na vipengele ni vingi hivyo ni vizuri nije Tu nifahamu kila kitu ofisini. Kwa kuwa nilihitaji Mimi Ajira basi nikamwambia sawa!

Huyu Jamaa yangu tangu kunipa taarifa za Ajira sijawahi tena kumpigia simu yaani yeye ndio amekuwa akinipigia kana kwamba yeye ndio anatafuta Ajira. Hiki kitu kilinipa wasi wasi Ila nilijipa Moyo nikiamini kwamba pengine bado kuna watu wema hivyo Jamaa ni mtu Mwema amejitoa Tu kunisaidia, nikayatoa mawazo negative nakamchukulia positive!


Juzi tarehe 21/10/2021 nikajichanga, nikajiandaa Kwa safari ya kuja Dar! Nimetoka Morogoro Saa Tisa alasiri, nikiwa kwenye gari Jamaa ananipigia Tu kuniuliza kuwa nimefika wapi!

Hatimaye nikaja kushuka Mbezi Luis Saa moja usiku. Baada ya kushuka, nikampigia Jamaa maana alisema anakaa hapo hapo Mbezi. Baada ya kuwasiliana nae akaniuliza kuwa "Je, wewe (Mimi) ni mwenyeji kidogo wa Dar" nikamwambia ndio wakati sio kweli.
Swali lile na mengine ambayo ni personal zaidi yalizidi kunitia wasi wasi ambapo nilijisemea itabidi nichukue tahadhari zaidi.


Baada ya kumwambia kuwa Mimi ni mwenyeji akaniambia nichukue boda boda niende Hadi Sheli ya Meru hapo Goba road, nikamwambia sawa!

Nilichofanya hapo likanijia wazo nikamtafuta Jamaa tuliyefahamiana mtandaoni (yupo Sinza) nikamwambia anipe hifadhi Kwa usiku huo Tu akaniambia niende Tu bila shida.
Basi baada ya kutoka hapo Stendi ya Mbezi nikapanda daladala naelekea huko Sinza na Jamaa huyu niliyejuana nae mtandaoni akanipokea!


Baada ya Jamaa huyu Mwalimu niliyekuja Kwa niaba yake kunipigia Sana simu Kwa kunisubiri Kwa muda mrefu, hatimaye nikapokea na kumdanganya kuwa kuna mtu nilimletea mzigo na alitakiwa aje apokee hapo Stendi Saa 12 jioni Ila Kwa vile nilichelewa kufika ameniomba nimpelekee Kwa vile hataweza kuja tena Stendi maana yeye ameingia tayari kazini (kazi ya ulinzi). Nilimwomba aniwie Radhi Sana na kuwa nitajitahidi kujihimu asubuhi Sana. Akaniambia sawa japo niligundua kuwa hakufurahia.


Usiku huo nikalala Sinza na asubuhi ya Jana nikaamka Saa 12 nikapanda daladala Hadi hapo Sheli ya Meru nikampigia simu akaniambia nipate chai kabisa ili aje anikute tuende ofisini kabisa, nikasema sawa!

Baada ya masaa mawili akaja tukaona, tukaenda. Tukiwa njiani akawa kama anachati na mtu hivi, tukafika sehemu fulan hivi tukasimama akasema nisubiri akaenda pembeni kuongeza na simu! Baada ya mwendo kama wa dakika 10 Kwa miguu tukafika kwenye nyumba moja hivi kuna geti kubwa halafu kuna vijana wawili nje (wa kike na wa kiume).


Baada ya kutokea Tu mbele Yao wale vijana wote macho Yao yote yakawa kwangu ambapo kama kulikuwa na umakini Fulani hivi na tahadhari inachukuliwa huku, hapo hapo kabla hatujasimama Jamaa (Mwalimu) akanikaribisha moja Kwa moja ndani ya geti, na baada ya kuingia ndani tuliwakuta vijana wengi kama 20+ hivi ambao walikuwa busy wakikaa Kwa vikundi vikundi! Ile tulipoingia Tu kila mtu aliacha anachokifanya wote wakanyanyuka na kusogea karibu yetu huku ukimya na umakini ukitawala (hakuna hata aliyeongea tena) lakini macho Yao yote yakawa kwangu huku wengine wakitabasamu na kutikisa kama vichwa hivi.

Hapo nilihisi Jambo la hatari Sana na ukiangalia humo kuna vijana wadogo Tu ambapo kama kuna mwenye umri mkubwa ni miaka 27 Tu huku mabinti wakiwa wengi! Kwa mionekano Yao wamevaa vizuri Sana, wanaume wamevaa suti na wanawake pia wamevaa vizuri Ila wamevalia suruali Ila sio za jeans!


Hapo kuna mtu alipewa ishara Fulani akaingia ndani baada ya kama dakika moja nikaongozwa niingie ndani tukapanda floor ya juu tukafika kwenye ukumbi Fulani ambapo kuna wengine walitoka vyumbani wote tukatengeneza kama duara Fulani huku nyumba yote ukiwa kimya hakuna anayeongea! Kilichonipa wasi wasi Sana sikujua ni nini kinaendelea na kila kinachoendelea ni kama wanapeana ishara Fulani ambazo Mimi sikuziona wala kuzielewa! Nilichokuwa Naona Mimi ni Yale matendo Tu.


Pale Yule Mwalimu akatoa salamu akasema "Good morning" wote nao wakaitikia "Good Morning.....!!! Kwa nguvu na Kwa heshima Fulani. Haya yote yakiendelea watu wote macho kwangu huku wengine wakitabasamu Kwa mbali! Niliona hasa hizo Pisi ndo wanatabasamu zaidi! Zile movement za Kwanzia getini Hadi ndani kwenye ukumbi, nilihisi mambo kadhaa kwamba, mle kuna mambo ya nguvu za Giza natakiwa nijiunge.
Pili, lile jumba ukiingia unabakwa n.k...
Kiukweli hapo ukumbini nilianza kuogopa Sana kiasi cha kuanza kutetemeka Ila nilijikaza huku nikijiambia sihitaji kuwaonyesha kuwa uwoga umeniingia! Basi pale kiongozi wao (Mwalimu) anataka kila mmoja ajitambulishe kuwa yeye ni Nani n.k....

Baada ya utambulisho kila atakayetoa Neno lazima asisitize kuwa wanafurahi Mimi kuwepo pale na nitaenda kuona kitu kipya ambacho sijawahi kuona na kitabadilisha Maisha yangu yote!

Tulipomaliza pale ukumbini nikaambiwa twende tukupeleke ofisini sasa ukaonyeshwe kile kilichonileta mahali hapo! Nikapewa Jamaa mmoja! Tukaingia chumbani na mlango ukafungwa! Humo kuna meza na viti vitatu! Nikakaa Jamaa akasema "zima simu au uiweke silence maana mkuu anakuja" Baada ya hapo akaja Jamaa akajitambulisha akaanza kuniuliza maswali personal kabisa... Nikajua yeye ndio kiongozi mwenyewe kumbe sio! Yeye alikuja Tu Kwa niaba ya huyo kiongozi aje anikumbushe kuwa nahitaji niwe attention kumsubiri kiongozi! Kwa zile movement zote nilijipa hitimisho kuwa mle kuna mambo ya nguvu za Giza hivyo niwe tayari mzimu utatokea muda wowote pale chumbani! Niliogopa Sana, nilianza kusali kimya kimya na kilichoniuma zaidi hakuna hata ndugu wala Jamaa niliyemwambia kuwa naenda wapi na kufanya nini! Pale nilipotoa Tu simu kuweka silence, Mama yangu akapiga! Niliumia Sana! Nikasema yaani Mama yangu ameshajua kuwa naenda kufa!? Yaani nakufa Leo ikiwa Mama yangu ninayempenda kuliko mtu yeyote hapa duniani akiwa jina lake ndio la mwisho kuliona machoni kwangu!?

Nampenda Sana Mama yangu wakuu! Yeye ndio amekuwa mtu anayenifanya nipate Moyo na nguvu ya kupambana.
Amekuwa tayari kutofautiana na mshua ili Mimi nisonge na kufanya kile ninachokiona! Mama ni mtu wa pekee anayeheshimu mawazo na maamuzi yangu! Sina mahusiano mazuri na mshua na amekuwa akinikatisha Tamaa Kwa kila ninachotaka kufanya! Asili yangu ni ufugaji hivyo Baba yangu amekuwa hataki kabisa nijihusishe na chochote nje ya ufugaji! Naishi Pwani ambapo Hali ya ukame imekuwa changamoto hasa na kupelekea kupata hasara Kwa mifugo Mingi kufa!
Nilifaulu vizuri nikiwa shule ya msingi Ila Baba hakutaka niendelee kusoma. Umri unasogea bado nipo Kwa Baba, sina elimu ya kutosha, sina uzoefu wa kitu kingine chochote ambacho naweza kufanya nje ya ufugaji. Hivyo mimi kama kijana nimeona ni take risk nisitegemee ufugaji Tu! Na hiki ndio kilichonifanya niachane na wazazi wangu hasa Mama yangu ninayempenda. Ninatakiwa kuwaza na kufanya kitu nje ya kile nilichozoea. Natakiwa niende na wakati, na hata kama nitafanya ufugaji Ila sio huu anaoufanya Baba yangu toka zamani. Naamini huu ni ukurasa wangu mpya wa Maisha, sijawahi kuishi mjini, sikati Tamaa na najua chochote nitakachokutana Nacho ni kama namna ya kujifunza! Naamini ule msemo wa wazungu "life begins at 40"
Nayaamini pia maneno ya Jack Ma wa Alibaba aliwahi kusema "When you are 20 - 30, learn from your boss, learn what bosses do. When you are at 30 - 40, do what you learned from bosses" Yaani kwamba hapo ndo Ile kauli ya life begins at 40 huanza kutumika hapo kwamba unaanza kuyaishi au kufanya Yale uliyofanya ikiwa na mabosi tangu ukiwa na miaka 20 Hadi 30. Hivyo naamini haya ninayopitia ni mafunzo Tu!

Tuendelee.......

Baada ya kutoka simu chap nikaandika SMS Kwa mjomba wangu nikamwambia "Nipo Mbezi karibu na Sheli ya Meru Barabara ya Goba"


Pale ukumbini niliambiwa mle ofisini itanichukua Saa moja na nusu Hadi mawili Hadi tutoke! Baada ya Kama dakika 5 kiongozi mlango ukasukumwa Jamaa akanipa ishara tusimame chap, kiongozi (Mwalimu 😂😂) akaingia akampa Jamaa mkono wakasalimiana Kwa salamu Ile Ile ya Good Morning nami hivyo hivyo! Hakuna salamu nyingine!


Hapo sasa nikaambiwa nitaenda kubadilishwa Kwa kutumia Catalog ambapo nikaanza kuulizwa kuhusu utajiri, mafanikio na maswali mengi Tu personal! Nikaulizwa kuhusu level ya elimu, nikaulizwa kama nimewahi kusoma kitabu cha Robert Kiyosaki na blah blah nyingi Tu.... Mara wanichoree jedwali la Waajiriwa, Wafanyabiashara wadogo, Wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji! Kiufupi waliniletea mbwembwe nyiiingi Hadi ule uwoga ukaniisha, wakanichosha Hadi nikawa nasinzia! Hapo Mimi sikutaka kuonyesha dalili zozote zile za kuwapinga au kuwakosoa nikiwa kwenye himaya Yao! Nilikubali kila kitu kuwasikiliza!

Basi pale wakaendelea na porojo nyiiingi sijui Maisha yako Leo yamebadilika sijui achana na kuajiriwa, sijui utaingiza Million 14 Kwa miezi 8 n.k.... Baadae wakanipa kitabu fulan hivi kuna picha za majengo, sijui nn na nn.... Ila nilipoona Tu QNET, nikawarahisishia kuwa nimeelewa kila kitu twendeni hatua inayofuata! Wakaniambia Toa 50k Tshs Kwa ajili ya accommodation nikawaambia hakuna shida nikawaomba niende toilet nikatoka nikawaambia pesa sina mkononi Hadi nikatoe bank hivyo naomba nimpigie Yule Jamaa yangu wa Sinza aje na begi langu nitoe Kadi ya Benki. Wakagoma wakasema Bora niende na Jamaa mmoja hapo ili tukachukue nikawaambia hakuna shida!

Hapo kabla Mwalim alipokuja kunipokea cha Kwanza aliniuliza Kwanza begi mbona sina nikamwambia nimeliacha Kwa sababu kule nilipoweka begi Jamaa yangu wa Sinza kuna sehemu alienda akafunga mlango hivyo nilishindwa kuchukua begi. Jamaa (Mwalimu) akalaumu Sana Kwa nn nimeacha akasema itabidi Tu nibaki halafu itafutwe namna begi lije!


Baada sasa ya kutoka na Jamaa niliyepewa niende nae, njiani nikafeli Kwa kumfanya ajue kuwa namewajua kuwa wao ni Akina Nani, na kitu ambacho walikuwa wananisisitiza ni kuwa sipaswi kumwambia mtu yeyote chochote kuhusu wao maana ukifika ofisi zao ndio utajua uzuri wao!


Baada ya Jamaa kugundua hicho nadhan akawaambia wenzake Kwa SMS ambapo baada ya kama dakika kadhaa akaniambia tupite hapa njia ya shortcut yaan hapo ndo nilipofeli kabisa! 😭😭😭

Tulifika kwenye kichochoro Fulani ambapo hapo ndo tulikutana na Jamaa kama wanne wakatukaba wakachukua kila kitu pesa yangu yote, pamoja na simu yangu ndogo! Nashukuru Mungu simu kubwa niliiacha chaji huku Sinza nisingekuwa na mawasiliano!

Hao Jamaa nadhani ni kitu kimoja na hao vibaka na wamefanya hivyo Kwa kugundua kuwa nimeshawajua na sipo tayari kujiunga na huo upuuzi na utapeli wao!

Hiki ndio kilichonifanya nije hapa kwenu wakuu!

Naombeni msaada wa kazi au hata kama connection Kwa ndugu Jamaa na marafiki!! ASANTENI SANA.
 
Qnet kama Qnet, nakumbuka mbali sana 2018, kuna demu aliunganishwa na rafiki yangu kwangu, alinipigia simu na tukakutana fresh, maeneo ya river side, tulifanya mazungumzo, baadae akaniunganisha officine kwao mikocheni.

Nilikaribishwa na blah blah zao kama kawaida. Lakin mwisho wa siku niliwagundua.

Demu tuliendelea na mazoea naye kama kawaida, kuna siku nikaomba gemu akanichomolea, nikasema sawa, lakin number zake nilimpa kaka yangu akapiga

Toka siku hiyo sijui yuko wap na alikata mazoea na mm.

Mara moja moja nilimuomba turuwe marafiki alikataa, kumbe alikuj kugundua kuwa na mahusiano na kaka yangu.
 
Qnet kama Qnet, nakumbuka mbali sana 2018, kuna demu aliunganishwa na rafiki yangu kwangu, alinipigia simu na tukakutana fresh, maeneo ya river side, tulifanya mazungumzo, baadae akaniunganisha officine kwao mikocheni.

Nilikaribishwa na blah blah zao kama kawaida. Lakin mwisho wa siku niliwagundua.

Demu tuliendelea na mazoea naye kama kawaida, kuna siku nikaomba gemu akanichomolea, nikasema sawa, lakin number zake nilimpa kaka yangu akapiga

Toka siku hiyo sijui yuko wap na alikata mazoea na mm.

Mara moja moja nilimuomba turuwe marafiki alikataa, kumbe alikuj kugundua kuwa na mahusiano na kaka yangu.
Dah, sawa
 
Back
Top Bottom