Mambo ambayo ni uongo lakini yanajulikana ni kweli kwa wengi

Mambo ambayo ni uongo lakini yanajulikana ni kweli kwa wengi

Hii mada ya Leo ni msumali wa moto
Unaunguza nafsi, moyo mpaka akili
Piga na upande wa pili wavaa kobaz
Piga na upande Marasi
Piga na upande wa nne wapagani
Piga na upande wa Tano wasioamini kwamba Kuna Mungu na Miungu
Piga upande wanaoamini dini zao za jadi
 
Wapi nimesema kuwa Lila Mzee mhitaji amechezea Maisha?
Au mwenye Maisha magumu ni mvivu?

Yaani unakitungia maujinga yako yaliyopo kichwani Mwako unadhani kila MTU anawaza Kwa namna yako.

Ukitoa hoja zinazohusu kumkosoa MTU kosoa kile alichoeleza, na sio ukosoea ujinga uliomo kichwani Mwako ukidhani ndio mawazo ya MTU unayemkosoa.

Karibu Sana Mkuu
Hiyo ni mifano, wewe umesema usimsaidie mzazi kwa sababu hakuweka saving,

mim nimekutolea mifano tunawasaidia wazazi wetu wakiwa wazee kwa sababu ya circumstances tofauti tofauti kitu wewe ambacho wewe unapinga

Kiufupi wewe ni mtoto na hujui maisha, ukiwa kijana na nguvu, unahisi utakua fresh all the time lakin maisha hayako hivyo Ila ukikua utajua
 
Wapi nimesema usimsaidie Mzazi?
Mbona unawaza mambo yako kichwani alafu unanilisha mimi, Acha uongo.
Embu nukuu hiyo sehemu niliyosema usimsaidie Mzazi.

Jitahidi ukiwa kwenye mijadala uwe na Utulivu wa Akili ndipo utoe hoja zako.
Kuliko unavyoendekeza mihemko ya kihisia. Alafu kama ni MTU mzima ndio haileti picha nzuri, mihemko Kwa Watu wazima ni aibu na mara nyingi huwadhalilisha.

Kama hukuelewa ungeuliza
 
Logically uongo + uongo= Ukweli
Na sio uongo kama ulivyoandika. Karudie tena kusoma Logic implication.
Uongo+Uongo=Kweli kuwa ni uongo .

Ukitoa ushahidi wa kwanza ukaonekana ni uongo,ukatoa ushahidi wa pili nap ukaonekana ni uongo, hitimisho lake kwamba kweli wewe ni muongo.
 
Unazidi kupotea dogo, kadri siku zinavyosonga ndivyo unavyozidi kuandika pumba.

Ulipata umaarufu kwa kuandika mada konki ila sasa unaandika utumbo tu.

Kipi ni pumba hapo?
Ingefaa ujadili Kwa hoja. Alafu siandiki ili niwe maarufu au nipate chochote, naandika ukweli na Haki.
Ukiona nimeandika Jambo kinyume na Haki na ukweli hapo uje uniseme tena Kwa hoja.
 
Hii mada ya Leo ni msumali wa moto
Unaunguza nafsi, moyo mpaka akili
Piga na upande wa pili wavaa kobaz
Piga na upande Marasi
Piga na upande wa nne wapagani
Piga na upande wa Tano wasioamini kwamba Kuna Mungu na Miungu
Piga upande wanaoamini dini zao za jadi

Nimeona nianzie huku kwetu ili nisionekane Mbaya. Ukitaka kumulika nyoka unaanzia miguuni Mwako.
Ningeenda Kwa Ndugu zetu waislam wangesema ninawasakam kisa Mimi mkristo
 
Wapi nimesema usimsaidie Mzazi?
Mbona unawaza mambo yako kichwani alafu unanilisha mimi, Acha uongo.
Embu nukuu hiyo sehemu niliyosema usimsaidie Mzazi.

Jitahidi ukiwa kwenye mijadala uwe na Utulivu wa Akili ndipo utoe hoja zako.
Kuliko unavyoendekeza mihemko ya kihisia. Alafu kama ni MTU mzima ndio haileti picha nzuri, mihemko Kwa Watu wazima ni aibu na mara nyingi huwadhalilisha.

Kama hukuelewa ungeuliza
Au unaambiwa kuna Laana ya Wazazi, lakini unakuja kuona wapo wanasiowaheshimu wazazi wao lakini wanaishi Kwa furaha na Maisha ya mafanikio, muda huohuo kuna wanaowaheshimu wazazi wao lakini wanateseka. Mwisho unahitimisha ni UONGO hakuna kitu kama hicho.

Heshima ni pamoja na kusaidia wazazi
 
Kufanikiwa ni matokeo ya kutumia akili juu ya kiwango cha kawaida na si vinginevyo. Sio laana, sio baraka.
Akili inakufanya ujue jinsi dunia ya mali inavyokwenda.
Acha uongo kufanikiwa kwa asilimia kubwa kwanza ni bahati then ndo yaje hayo mambo ya akili hakuna asiyetaka kufanikiwa kimaisha ila wanaofanikiwa mbona sio wote.
 
Au unaambiwa kuna Laana ya Wazazi, lakini unakuja kuona wapo wanasiowaheshimu wazazi wao lakini wanaishi Kwa furaha na Maisha ya mafanikio, muda huohuo kuna wanaowaheshimu wazazi wao lakini wanateseka. Mwisho unahitimisha ni UONGO hakuna kitu kama hicho.

Heshima ni pamoja na kusaidia wazazi

Sio kweli.
Kusaidia Ipo kipengele cha upendo.

Unapomsaidia mzazi wako sio kwamba unamheshimu Bali unampenda.
Heshima inahusu Mamlaka, utawala, Oda, maonyo, maadili,..

Upendo unahusu kujali, kuhudumia, kufariji, n.k.

Tofautisha hayo mambo.

Kuna Jambo moja hautanielewa kama utatumia mihemko kusoma ninayondikaga.
 
Acha uongo kufanikiwa kwa asilimia kubwa kwanza ni bahati then ndo yaje hayo mambo ya akili hakuna asiyetaka kufanikiwa kimaisha ila wanaofanikiwa mbona sio wote.
Bahati ni nini? Bahati ni kitu ambacho hakipo. Inaaminika tu kuwa ipo lkn haipo. Hayo ni maneno ya jamii kuelezea mambo yaliyo juu ya uwezo wao.
 
Zaka tafsiri yake ni fungu la kumi linalotelewa kwaajili ya makuhani, wachungaji, maaskofu na viongozi wengine wa Dini.
Kwa mujibu wa Dini ya kiyahudi na kiebrania.

Sadaka ndio hutolewa kwaajili ya msaada tuu kadiri ya mapenzi ya MTU.

Binadamu huna chochote utakachofanya kwaajili ya Mungu.
Kusema unatoa shukrani Kwa Mungu haina maana yoyote Kwa huyo MUNGU MUUMBAJI WA YOTE. Labda miungu yenye vikao na wanadamu

Hujui maana ya shukrani wewe sisi waislam tunafundishwa kushukuru kwa kila jambo jema, na shukrani yako kwa mungu haimsaidii kitu zaidi ni kuonyesha unyenyekevu na umuhimu wa jambo alilokupa.
 
Anaandika Robert Heriel.

Leo tutajadili ishu ya UONGO dhidi ya UKWELI.
Katika Mantiki/Logic Ipo Hivi;
Ukweli + Ukweli = Ukweli
Ukweli + Uongo = Uongo
Uongo + Uongo = Uongo
Uongo + Uongo = Uongo

Mara nyingi ukweli hujulikana zaidi kwenye matokeo/mwisho wa Jambo au muda.
Ukweli huwaga hauna Pande mbili. Yaani ukweli hautegemei mtazamo au Maoni ya MTU. Ukweli NI ukweli.

Ngoja nikupe mifano ya UKWELI
i. Moto unaunguza - KWELI
Hii hahitaji mjadala, Watu wote na viumbe wote hujua Moto unaunguza. Yaani hata kichaa anajua ukweli huo.

ii. Mapenzi yanaumiza - KWELI
Watu wote Duniani na viumbe vyote Duniani vinajua mapenzi yanaumiza.

Yafuatayo ni mambo ya UONGO AMBAYO watu wengi hujua NI ukweli.

1. Laana na Baraka - UONGO
Unaambiwa ukifanya hivi utalaaniwa au ukifanya hivi utabarikiwa. Huo ni Uongo.
Nitakupa mfano, Kwenye dini unafundishwa Fanya kazi Kwa nguvu na bidii ili ubarikiwe. Lakini unakuja kugundua wapo wanaofanya kazi hawafanikiwi, na wapo wasiofanya kazi wanafanikiwa. Mantiki ya Jambo hili ni Uongo.

Au unaambiwa kuna Laana ya Wazazi, lakini unakuja kuona wapo wanasiowaheshimu wazazi wao lakini wanaishi Kwa furaha na Maisha ya mafanikio, muda huohuo kuna wanaowaheshimu wazazi wao lakini wanateseka. Mwisho unahitimisha ni UONGO hakuna kitu kama hicho.

Ukweli NI huu; kila MTU au kiumbe kimeshaupangiwa nini kitafanya katika Maisha yake. Chochote ukifanyacho kipo katika Akili ya mtunzi aliyekubuni.

2. Kumwabudu Mungu ndio kufanikiwa - UONGO
Wapo wasiomuabudu Mungu na wamefanikiwa.

3. Yesu alikufa ili kutukomboa - UONGO
Dhana ya kusema bila ya Yesu Watu hawawezi kumuona Mungu ni UONGO kwasababu wapo ambao tayari walikuona huyo MUNGU hata Kabla ya Yesu kufa. Kimantiki hiyo stori ni ya uongo Kwa sababu tayari inapande mbili.

4. Kifo kililetwa na dhambi ya kula tunda pale Edeni - UONGO
Kwa sababu wapo viumbe ambao hawakula lile tunda na wanakufa. Wanyama, ndege na samaki, na mimea inakufa licha ya kuwa haikula lile tunda.
Kifo NI mfumo wa Maisha Kwa mwanadamu. Hakina mahusiano na masuala ya maadili.

5. Kutoa zaka unapata thawabu kutoka Kwa Mungu - UONGO
Ni uongo Kwa sababu wapo ambao hawatoi zaka lakini wamefanikiwa. Viongozi wa dini wasiseme Uongo katika hili, muulize kiongozi wako mbona kuna Watu hawatoi zaka na wanamaisha mazuri kuliko wanaotoa?

Kwa kifupi zaka ni malipo unayompa mchungaji au Sheikhe au kiongozi yeyote wa Kiroho mara baada ya kupokea Huduma Fulani. Kama huna Huduma yoyote uipatayo kwenye mambo ya Kiroho hautakiwi kutoa zaka.
Ukienda kanisani au msikitini lazima utoe zaka kwani unaenda kupata Huduma hizo.

Ngoja ninywe maji kisha narudi kupendele.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Yesu ni Mungu,
Wakati huohuo Yesu ni mwana wa Mungu
=>UONGO
 
Sio kweli.
Kusaidia Ipo kipengele cha upendo.

Unapomsaidia mzazi wako sio kwamba unamheshimu Bali unampenda.
Heshima inahusu Mamlaka, utawala, Oda, maonyo, maadili,..

Upendo unahusu kujali, kuhudumia, kufariji, n.k.

Tofautisha hayo mambo.

Kuna Jambo moja hautanielewa kama utatumia mihemko kusoma ninayondikaga.
Ukikipenda kitu ni rahisi sana kukiheshimu, huwez sema unampenda mtu alafu umheshimu umeshaona wapi mfano mwanamke akikupenda atakushimu na atakua tayari kujitoa Kwa ajili yako, ukiwapenda wazazi wako utawaheshimu na kujitoa Kwa ajili yao
 
Back
Top Bottom