Mambo gani huwa unafanya ukiwa na msongo wa mawazo ama mtu akikukera?

Mambo gani huwa unafanya ukiwa na msongo wa mawazo ama mtu akikukera?

Pepsi big ya bariidiii inatosha.
Kisha natembea tembea hapo home sikai chini mahali pamoja muda mrefu.
Naenda narudi naenda narudi hadi saa 8 usiku toka jioni.
Sitaki maswali au kelele yeyote.
Sipokei simu labda nihisi ya jambo muhimu sana.
Naingia JF natoka, naingia natoka. Na refresh page kila mara nione New Posts.

Hahaha eti hutaki maswali 😂
 
1.kula ( nikiwa na stress nakula sana mkuu )
2.Japo ya kitoto ila huwa inanisaidia sana,. Huwa nachukua karatasi na peni naandika kila kitu kinachonisumbua na kunikera yaani like namuhadithia mtu hivi,. Nikimaliza nachana chana basi😂😂😂
Utanongeka sasa jirani 😹😹
 
Kwasababu ya maoni ya wadau? Ni kweli kuna muda sisi wachangiaji tunazingua sana mtu akija na tatizo lake....lakini naona siku hizi tunajitahidi
Naam, kwa kiasi chake imepungua ila bado si sana.
Unaweza kuta maoni ya mtu haya kuhusu wewe ila uwasilishajiwake ukawa mbaya kwako.
Hapo tayari Isha kuondolea furaha
 
Back
Top Bottom