Mamilioni ya pesa anayotaka Jackline Mengi kwa ajili ya malezi ya watoto wake haya hapa!

Mamilioni ya pesa anayotaka Jackline Mengi kwa ajili ya malezi ya watoto wake haya hapa!

Huyu aache kusumbua watu.. Iko siku watoto wake watamhoji wakiujua ukweli..
 
Dogo anatembeza sumu ya mende kunguni kiroboto door to door [emoji23][emoji23][emoji23] wakati mzee wake aliacha B1
Wee acha tu mkuu, kuna jirani yangu kule kijijini miaka ya 1995 anaendesha range, maana mjini alikua vizuri sana, na ana ghorofa hapo manzese adi leo lipo...
Alifariki 1996 mwaka 2003 nmeenda kijijini nkamkuta mama ake kachoka nkamnunulia sukari kilo 2 alishukuru adi machozi yakanitoka, nkajiuliza ule utajiri ulienda wapi? Mwanae aliekua anatupakiza na kutuzungusha kitaa kawa tapeli mjini, Nkabaki nawaza tu labda utajiri wa tunguli ulikua lkn baada ya kukua zaidi nikagundua mengi zaidi ya tunguli tunapitia humu duniani
Utajiri wakati mwingine ni mateso kwa kizazi chako ulichokiacha duniani
 
Mwenye mali ndio anaamua kuhusu mali zake ale na nani? Watoto hawana nguvu kwa mwenye mali
Sheria inataka maamuzi hayo ayafanye akiwa na akili timamu na sio wakati ‘dishi’ limeyumba, pia maamuzi yako yasivunje sheria zingine zinazoongoza ugawaji wa mali.
 
Bila mengi kuzaa na jack.

Mali zake zilikuwa zinahama kwenye blood line yake miaka isiyozidi 20 mbele.

Kuzaa na jack mengi hajakosea kabisa. Maana watoto wake wa mwanzo walikuwa hawataki kuoa wala kuzaa na wameshafika miaka 50 wote. Sasa wakifariki mali zingeenda kwa nani?
Hili ndio jibu..!

Hao kina Abduel na Regina sijui walifungwa wapi na nini /Nani... ..Wana shida sehemu ...

haKuna hata mwenye ndoa Wala mtoto.. wawaache wadogo zao waendeleze ukoo.. ..

Mzee Naye alikosea angegawa Kama zawadi kabla hajafa.. ..
 
Hiyo 90M kwa mwaka ni takribani USD 38500 si pesa ya kutisha kwa kustarehe kwa watoto 2 + mama yao + beki tatu kwa wenye pesa zao.

Sisi tusio nazo ndio tunaona pesa nyingi.

Tukaze matako kutafuta pesa nasi mwaka mmoja tuwe na matumizi ya luxury zaidi ya 90M kwa mwaka.
Tatizo sio udogo au ukubwa wa pesa tatizo ni value of money kwamba je iyo pesa inaenda mahali stahiki? Mchango wa jack katika mafanikio ya Mzee Mengi haujafikia uhalali wa kukunja mkwanja mkubwa ivyo ingekua ni yule mke wake aliefariki tungesema sawa maana walihustle pamoja kuanzia chini
 
Kama baba yao yupo yes. Sasa anawaomba watu ambao si wazazi wa hao watoto. Yeye kama mzazi ana uwezo wa kutoa hizo pesa? Tuanzie hapo kwanza.
Sheria ya child support ifanyiwe marekebisho mzazi anaekaa na mtoto ndio anatakiwa kutimiza gharama zote za matunzo kama uwezo hana au anataka watoto waishi maisha ya luxury ambayo hawezi kumudu basi ampeleke mtoto kwa mzazi mwenzake au mlezi aliepewa jukumu la matunzo ya mtoto kuliko kusumbuana sumbuana
 
hapo kwanza nicheke starehe kwa mwaka ni mafao ya mfanyakazi aliyefanya kazi miaka 40
 
Sio wachaga tuu washamba woteee uzeen ndo wanaona pa kuanzia kula starehe na makahaba
Mzee mengi hata kipindi akiwa maji ya moto alikua kiwembe wakina madam ritta hawa ashapiga sana mashine enzi izo wakiwa bado mabinti wabichi tu labda ukiwembe alienda nao mpaka uzeeni
 
Hili ndio jibu..!

Hao kina Abduel na Regina sijui walifungwa wapi na nini /Nani... ..Wana shida sehemu ...

haKuna hata mwenye ndoa Wala mtoto.. wawaache wadogo zao waendeleze ukoo.. ..

Mzee Naye alikosea angegawa Kama zawadi kabla hajafa.. ..
Shida ni kwamba mama yao anataka kuwachonganisha hao watoto na ndugu zake. Alifoji wosia wa tamaa na kutaka kujimilikisha IPP yote mwenyewe. Huo ni upuuzi na sijui aliingizwa mjini na matapeli gani..

Jackie angeamua tu kusiwe na purukushani bado angeendelea kuishi vizuri na by the year watoto wanafika 18 wangepewa shares huko IPP na maisha yangeendelea. Sasa haya anayoendelea kuyafanya ashukuru tu ile familia ni wapole, angekutana na vichaa angenyooshwa vizuri tu
 
Ukiwa na mali ukafunga NDOA na slay queen umeenda na maji!!

Ukishafunga tu NDOA hesabu nusu ya Mali imeenda ukimzalisha tu mali ZOTE zimeenda na maji!!
 
Wapo wadada wanaoomba Jack ashindee ili nao waanzishe kesi za namna hii, wakifika mahakamani wanasemaa mheshimiwa rejea kesi ya Jack na watoto wa Mengi.

uchaggani ukijifanya mjuaji wanakutenda zaidi. ila ukikaa ukatulia na kujamiiana nao vizuri basi watakupokea na kujumuika nawe
 
Kuoa uzeeni ni kuleta balaa nyumbani
Nashangaa wengi wanakuunga mkno. Wako mamilioni waliooa uzeeni na wakaishi vizuri. Na kuna mamilioni walioa ujanani, na wakaishia pabaya. Tusichukuwe matukio machache kuandika hitimisho. Ni kuonyesha ufupi wa akili.
 
Washua mkisha zeeka msioe hawa wanawake wachanga hususani hawa wanao angalia panapo fuka moshi mtasababisha uzao wenu uteseke na kusumbuana na kurogana saana. Mkisha zeeka wazee wetu tafuteni wa bibi wenzenu.
Mbona kuna ndoa nyingi za vijana zenye ugomvi wa mirathi? Usiwe kama yule kipofu aliyepata uwezo wa kuona kwa sekunde moja, akaona mwezi. Bada ya kurudi katika hali ya upofu akawa kila akimbiwa kitu chenye sifa fulani huwa anafananisha na mwezi.
 
Back
Top Bottom