Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia

Habari wakuu, nimeona taarifa kadhaa kwenye mtandao hasa kwenye page ya HabariLeo ya kwamba TRA wameshaita vijana kazini. Hii inaukweli wowote? Na kama ni kweli wanawezaje kuita kimya kimya bila kutoa pdf?

======

#HABARINJEMA: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia Suluhu Hassan kuajiri vijana 1,000 zaidi ya idadi ya awali.

TRA ilipewa kibali cha kuajiri vijana 1,100 hata hivyo Rais Samia aliongeza idadi ili kuotoa msukumo mpya wa ukusanyaji mapato.

Kaimu Katibu Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Samwel Tanguye ameiambia Daily News Digital kuwa idadi ya watumishi wengine wa TRA wataajiriwa hivi karibuni. TRA sasa inafikisha idadi ya watumishi 5000.

Alisema katika ajira za TRA vijana takribani 66,000 walituma maombi na baada ya kuchujwa kulingana na vigezo vijana 13,800 waliitwa kwenye usaili na 8,586 ndio waliofika kwenye usaili uliofanyika Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar.

Imeandaliwa na Idd Mwema
Hizi ajira zilitangazwa tangu mwezi August 2021 hadi sasa vijana hatujaitwa kwenye interview wala hakijulikani kinachoendelea.

Kila tukiuliza tunaambiwa Mh. waziri wa nishati ,January makamba hajatoa kibali cha ajira. Sasa kwanini nafasi zilitangazwa na watu wakaomba?

Tunaomba mamlaka zinazuhusika kuifuatilia jambo hili na inawezekana EWURA iliajiri kimya kimya bila interview kufanyika kwa kuwachukua Watoto wa vigogo na kuwapa ajira.

Kila tukifuatia HR wa Ewura kupitia simu namba 0783-335-800 Anajibu majibu ya ajabu kwa kusema hakuna ajira wakati alitoa tangazo la ajira.
Rais samia tunakuomba angalia Ewura kwa jicho la karibu malalamiko ni mengi mno.
 

Attachments

Back
Top Bottom