Kweli kabisa mkuu, watawala hata watanzania wapo kwaajili ya kulinda Utawala wao na hawana muda na Mahanga ya raia. Subiria ufike uchaguzi , uone Magari ya polisi yananunuliwa au silaha za kijeshi kisa tu kuwaogofya raia. Kule Zanzibar JWTZ wanajaza Kama wote , ila kwenye majanga Kama haya JWTZ inakuwa kigugumizi. Very stupid government.
 

Sidhani Kama ana huo muda , na sidhani ana wazo la kutoka huo msaada ulioandika. Zaidi ya kudhibiti taarifa ya watu waliofariki sidhani Kama Kuna jipya.
 

Kwa picha zilizo Kuja, mwanzoni kulikuwa na raia wamejibanza hapo juu ya bati kutokana na matope kujaa Chini, Sasa hao policcm wakaenda kuwafukuza.
 

Nadhani kwenye mambo ya majanga bado tupo nyuma sana, kuanzia ajali ya Precision Air na hii ya Hanang. Tunahitaji kukiboresha kitengo Cha maafa na idara ya polisi zimamoto na uokoaji
 
Mlima hanang unashusha mafuriko ya matope, katesh inafunikwa.

Inahisiwa kwamba crater ya juu ya mlima imezidiwa na maji na kupasuka.

Video hapa chini ni karibu na stendi ya katesh.
View attachment 2832069

Aisee hii ilitokea pia Same miaka kadhaa nyuma. Poleni sana wana Hanang’ Mungu awakinge na majanga zaidi pia atoe moyo wa huruma kwa wengine kuwapatia msaada wa kibinadamu.
 
Mkuu huwa Wana zuiliwa wasipigi picha, mm nilishuhudia mafuriko ya Moro mwaka huu mkurugenzi akiwa msando, alizuia waandishi wa habari wasipige picha za drone eneo la kihonda IPO tokea mafuriko

Kweli kabisa. Nimeiona hata vyombo vya habari vimepigwa biti.
 
Serikali ina kosa gani?!
Unauliza swali la kijinga na kipumbavu Kwa kuwa hujui hata maana ya serikali na majukumu yake..!!

Upangaji wa makazi unafanywa na watu binafsi au na serikali?

Ina maana wewe hujui kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuzuia watu kuweka makazi ktk maeneo hatarishi hata kabla ya maafa.?

Lakini kinachofanyika ni nini? Ni serikali kutoa vibali vya ujenzi hata katika maeneo ambayo inajua fika kuwa ni hatari Kwa maisha ya watu..!

Si hivyo tu, bali pia ni jukumu la serikali kuhakikisha inajenga miundombinu ya kuzuia mafuriko...

Lakini hebu nenda na angalia kwenye miji yetu mingi. Mambo yako hovyo hovyo sana, watu wanajijengea nyumba hovyo, hakuna mifereji ya kupitisha maji mengi...

Ukitaka kujua hatari inayokuja, nenda ktk mji wa Mwanza uone namna watu wanavyojijengea hovyo na kwenye maeneo hatarishi huku mamlaka za serikali zinazohusika na mipango miji zikiangalia tu...

Kwa hiyo, ni kweli Kwa kiasi kikubwa serikali inastahili kulaumiwa Kwa uzembe na kushindwa kuwajibika hata kutokea Kwa maafa haya..!!
 
Mungu awanusuru waja wake.

Serikali ya hovyo na mipango yake ya hovyo hovyo hugharimu maisha ya watanzania kila msimu wa mvua
Kwa hiyo huko ujerumani uchina na California ambako mafuriko hutokea wote ni wa HOVYO, ndio maana tunasemaga upinzani ni takataka hawana akili.
 
‼️Naweka kumbukumbu‼️
Machi 2023 Serikali kupitia kamati ya maafa ilipeleka msaada Malawi kufuatia maafa ya kimbunga Freddy


Msaada ulikuwa:
👉🏽Tani 1000 za unga wa mahindi (Tani 90 kutokea Dodoma na Tani 60 Iringa kuingia Malawi kila siku)
👉🏽Mablanket 6000, na mahema yasiyopungua 50
👉🏽gari la wagonjwa(Ambulance)
👉🏽karakana ya magari inayotembea(mobile workshop
👉🏽 malori makubwa ishirini yenye uzito wa tani 30
👉🏽 malori 10 yenye uzito wa tani zaidi ya kumi na nane(18)
👉🏽 Helikopta mbili
Katesh vipi mmeona hata ambulance huko?
@TZWaziriMkuu mpo?


#TutaelewanaTu lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…