Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 80 na Majeruhii 133
Nchi haipo kwenye maomboleze
Tv,media wanapiga misingeli amapiano tu+ misomisondo tu
Watu hawana habari na huko hanang

Any way poleni

Ova
 
Kuna watu humu hawajawahi kukumbwa na mafuriko, wanadhani ni wale tu waliojenga mabondeni kiholela. Majanga hayachagui masikini na tajiri, hayachagui mitaa ya wenye hela na wasio na hela, hutokea popote pale hata milimani, tambarare, baharini, nchi kavu, angani. Kwa hiyo tuwaombee sana watu wa hanang, misaada ya hali na mali inahitajika kwao. Hayo siyo majanga ya kujitakia.
Hawajui, mafuriko hayana cha bondeni Wala Nini, kama hayo ya Manyara ni yanatokea juu ya mlima yanashuka na mawe na miti, haijalishi umejenga kwenye muinuko au bondeni
 
Mafuriko yamesomba Kijiji, nyumba zimepotea na maisha ya watu, watu hawajui pa kulala, watoto wamelala njaa, asubuhi unawaambia rais kasema pole!!
Nimekumbuka yule aliyewaambia wenye njaa " nendeni muote Moto mshibe"
 
Kilichotokea ni landslide, siyo mafuriko (flooding), wala siyo mudflow.

Mudflow inasababishwa na kufurika kwa maji na kisha yale maji kuwa na uwezo wa kuondosha udongo wa juu na kuufanya tope.

Landslide and mudslide ni movement ya ardhi inayoweza kusababishwa na mvua kubwa ambapo layer moja ya ardhi hutembea juu ya layer nyingine kwa sababu contact inakuwa saturated na maji.

Kwa kawaida madhara ya landslide huwa ni makubwa kuliko mudflow kutokana ukubwa wa mzigo unaosababishwa na landslide.

Hawa got it right.

At least 47 people killed and 85 injured by landslides in Tanzania

The Guardian, UK.
 
Landslide:
Kujongea kwa kipande kikubwa cha ardhi kutoka juu kuelekea chini hii inahusisha kutokea kwa ufa (fracture) pia uwepo wa maji kama kichocheo Cha mmeguko.
View attachment 2833246
Madflow:
Kujongea kwa tope zito kutoka juu mlima kwenda chini hii inatokana na ardhi kushiba maji ya kutosha.
Picha za mlima Hanang umeziona au umetumia video za Katesh kusema ni mudflow?
 
Jamaa katoa ushauri mzuri, wewe sijui mambo ya udini umetoa wapi, unataka uonekani wa tofauti.
Mungu awaangazie watu wa Hanang Tanzania.
Umeisoma post yake ukaimailiza?

Au na wewe ni watu mnaowaza kwa hisia, miladi ayo akipost kwa huzuni unakua na huzuni, akicheka unacheka pia, akilia unalia pia.??
 
Mnachanganya mambo nyie, hao ni askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wakiwa ndani ya yunifomu zao zinazofanana na za askari wa FFU, tumewashauri sana wabadishe yunifomu zao zisifanane na za FFU lakini bado wanaendelea kuzivaa, ona sasa wanavyochanganya watu wanadhani ni FFU
Acha upumbavu , hao ni FFU .
We huoni mavazi hizo black beret na bullet proof vests ?
Zimamoto na black beret au bullet proof vests wapi na wapi ?
Na zimamoto nguo zao kijani yake ni tofauti na kijani ya FFU hata ukiziangalia huwa zipo tofauti ,na wanavaa beret nyekundu
 
Tukio lililotokea Hanang kwa nchi za wenzetu ni kubwa lakini kwetu ni dogo haliwezi kuizidi mechi ya mpira! Jana Jumatatu asubuhi vituo vya TV karibu vingi vilikuwa na uchambuzi wa mpira, haiingii akilini, ukifungua Tv haukuti taarifa zozote kuhusu maafa hayo zaidi ya muziki wa Bongo fleva na muvi! Mambo yanaenda kimyakimya kwani hata TBC1 inaonesha sura za viongozi tu wanapokuwepo kwenye eneo, wakiondoka nao wanaondoka!
Tz Kuna makanjanja hakuna wanahabari
 
Tukio lililotokea Hanang kwa nchi za wenzetu ni kubwa lakini kwetu ni dogo haliwezi kuizidi mechi ya mpira! Jana Jumatatu asubuhi vituo vya TV karibu vingi vilikuwa na uchambuzi wa mpira, haiingii akilini, ukifungua Tv haukuti taarifa zozote kuhusu maafa hayo zaidi ya muziki wa Bongo fleva na muvi! Mambo yanaenda kimyakimya kwani hata TBC1 inaonesha sura za viongozi tu wanapokuwepo kwenye eneo, wakiondoka nao wanaondoka!

MODS, ISOMEKE MANYARA BADALA YA HANANG.
Wewe mwenyewe mleta mada ni tatizo.

Ni kwanini unataka heading isomeke "Manyara" badala ya "Hanang'" wakati tukio limetokea Hanang' na siyo Manyara yote?
 
MANYARA: Idadi ya Watu waliopoteza maisha kutokana na Mafuriko yaliyosababishwa na Mvua zilizonyesha kuanzia Desemba 2 huko Hananga imefikia 47 na Majeruhi 85

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Mvua hizo zimeathiri Miundombinu ikiwemo kuvunja baadhi ya Nyumba, kukata Mawasiliano ya Barabara na Umeme.

============

===========

Watu watano wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa wilayani Hanang mkoani Manyara baada ya mvua iliyonyesha usiku wa Desemba 2, 2023 kusababisha mafuriko.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Desemba 3, 2023 amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na madhara katika mali za watu.

Fuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi na tovuti kwa taarifa zaidi

--

UPDATE: WALIOFARIKI DUNIA WAFIKIA 17

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amesema Watu 17 wamefariki dunia katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kufuatia mafuriko yaliyoambatana na mawe makubwa na miti kuingia katika makazi ya Watu ambapo imepelekea nyumba kadhaa kuanguka.

“Leo asubuhi tumepata changamoto hapa Hanang toka jana usiku zilikuwa zikinyesha mvua za kawaida lakini maji yakawa yameporomoka kutoka Mlima Hanang yakiwa na mawe na miti kuja katika Mji wa Kateshi yakiwa na nguvu, ambapo mpaka sasa tumepata vifo vya Watu 17 pamoja na majeruhi ambapo maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Tumaini lakini pia uharibifu wa miundombinu ya barabara kati ya Sindiga na Babati yamesimama kwa muda ila TANROADs na TARURA wapo hapa kuhakikisha mawasiliano yanarejea”

“Pia niwaombe Wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati jitihada za uokoaji zikiendelea”

====

HANANG, Manyara: At least 20 people have been confirmed dead and several others missing following heavy rains that triggered flash floods in northeastern town of Hanang in Manyara region on Sunday.

Manyara Regional Commissioner, Queen Sendiga, confirmed the incident, saying 70 people have suffered minor and serious injuries. The leader described the incident as “fatality and a tragedy” in the region.

Sendiga said the rescue teams were swiftly deployed to the affected areas to provide support and aid in the search for the missing.

==============
WALIOFARIKI WAFIKIA 49
MAAFA HANANG | Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, wilayani Hanang imeongezeka na kufikia watu 49 baada ya kupatikana miili miwili wakati wa zoezi la uokoaji linaloendelea.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga aliyotoa asubuhi ya leo Disemba 4, 2023 inasema idadi ya majeruhi bado ni 85.

Ameongeza kuwa shule za msingi Katesh, Hanang na Dumanang zitatumika katika kuhifadhi waathirika wa mafuriko hayo, na kuwataka wananchi kuhama mara moja maeneo ya hatari ili kujikinga na madhara mengine yanayoweza kutokea.

MANYARA: IDADI YA WALIOFARIKI KWA MAFURIKO YAFIKA 63, MAJERUHI 116

Idadi ya Watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, Wilayani Hanang imeongezeka na kufikia 63 baada ya kupatikana miili zaidi wakati wa zoezi la uokoaji linaloendelea

Waziri Mkuu Kassim Majalia amesema maporomoko ya udongo yamechangia athari kuwa kubwa.

Pia soma; Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang
watu 63 waliokufa ni watu wachache sana katika idadi ya watu milioni 60 na zaidi waliopo tanzania kikubwa nchi hapa imedhalilika kwa miundo mbinu mibovu, pesa zipo ila matumizi mabaya na bado majanga mengine yanakuja na yatawaangamiza wengi tu mpaka tutakapokuwa waaminifu kwenye matumizi ya pesa za wananchi kupitia serikali viongozi wengi akili zao zimezubaa mno.
 
Back
Top Bottom