Unauliza swali la kijinga na kipumbavu Kwa kuwa hujui hata maana ya serikali na majukumu yake..!!
Upangaji wa makazi unafanywa na watu binafsi au na serikali?
Ina maana wewe hujui kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuzuia watu kuweka makazi ktk maeneo hatarishi hata kabla ya maafa.?
Lakini kinachofanyika ni nini? Ni serikali kutoa vibali vya ujenzi hata katika maeneo ambayo inajua fika kuwa ni hatari Kwa maisha ya watu..!
Si hivyo tu, bali pia ni jukumu la serikali kuhakikisha inajenga miundombinu ya kuzuia mafuriko...
Lakini hebu nenda na angalia kwenye miji yetu mingi. Mambo yako hovyo hovyo sana, watu wanajijengea nyumba hovyo, hakuna mifereji ya kupitisha maji mengi...
Ukitaka kujua hatari inayokuja, nenda ktk mji wa Mwanza uone namna watu wanavyojijengea hovyo na kwenye maeneo hatarishi huku mamlaka za serikali zinazohusika na mipango miji zikiangalia tu...
Kwa hiyo, ni kweli Kwa kiasi kikubwa serikali inastahili kulaumiwa Kwa uzembe na kushindwa kuwajibika hata kutokea Kwa maafa haya..!!