Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 80 na Majeruhii 133
Wapigaji epukeni kudonoa pesa ya msaada Kwa waathirika Hanang' mtaishia pabaya.

NB: pesa za misaada kama michango ya msiba CAG hakagui Ila ikibidi tutapiga kelele akague
Hizo alizokwisha kagua na ukajua zimepigwa, wapigaji wamefanywa nini?
 
Kubwa la upigaji
20231206_144636.jpg
 
Habari Hanang ! Habari Manyara!

Nimeshikwa na huzuni kuu, nawapa pole ndugu zetu na wakazi wote wa mkoa wa Manyara kwa kufikwa na hiyo changamoto.

Napenda mtambue sisi ndugu zenu tunahuzunika pamoja nanyi sambamba na kuwaombea mpate faraja mpya na tumaini lenye kuwaletea amani tena kama ambavyo mlitamani muishi au mlivyopenda kujiwekea malengo yenu kijamii, kiuchumi na kimazingira.

Jueni ya kuwa, wapo Watanzania wezenu wanawapenda sana na wapo bega kwa bega na nyinyi katika hiki kipindi kigumu mnachopitia.

Kauli Mbiu

"Nakupenda Manyara, nakupenda Hanang; Wewe ni rafiki yetu, wewe ni ndugu yetu."
 
Hivi ni mafuriko ya maji?
Tope lq volcano?
Landslide
Bwawa lilipasuka
Au mto ulifurika
Au ni mafuriko ya kawaidia.
Au ni nini,

Maneno yamekuwa mengi tunakoswa cha kuchukua.
 
MANYARA: IDADI YA WALIOFARIKI KWA MAFURIKO YAFIKA 63, MAJERUHI 116

Idadi ya Watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Mji wa Kateshi, Wilayani Hanang imeongezeka na kufikia 63 baada ya kupatikana miili zaidi wakati wa zoezi la uokoaji linaloendelea
Jana tumeambiwa 68 imekuwaje leo toll inashuka
 
1702016273998.png


Nilipowianisha ukubwa wa eneo naa mtu, nilidhani huyo mwenye suti nyeusi ni mtoto kumbe mtu mzima
 
Unauliza swali la kijinga na kipumbavu Kwa kuwa hujui hata maana ya serikali na majukumu yake..!!

Upangaji wa makazi unafanywa na watu binafsi au na serikali?

Ina maana wewe hujui kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuzuia watu kuweka makazi ktk maeneo hatarishi hata kabla ya maafa.?

Lakini kinachofanyika ni nini? Ni serikali kutoa vibali vya ujenzi hata katika maeneo ambayo inajua fika kuwa ni hatari Kwa maisha ya watu..!

Si hivyo tu, bali pia ni jukumu la serikali kuhakikisha inajenga miundombinu ya kuzuia mafuriko...

Lakini hebu nenda na angalia kwenye miji yetu mingi. Mambo yako hovyo hovyo sana, watu wanajijengea nyumba hovyo, hakuna mifereji ya kupitisha maji mengi...

Ukitaka kujua hatari inayokuja, nenda ktk mji wa Mwanza uone namna watu wanavyojijengea hovyo na kwenye maeneo hatarishi huku mamlaka za serikali zinazohusika na mipango miji zikiangalia tu...

Kwa hiyo, ni kweli Kwa kiasi kikubwa serikali inastahili kulaumiwa Kwa uzembe na kushindwa kuwajibika hata kutokea Kwa maafa haya..!!
Huko mimi nimewahi kufika, hawakujenga mabondeni wala kwenye njia ya maji ni eneo salama kabisa, na sasa hivi njia ya maji imehamishwa na hayo maafa yametokea kwenye njia isiyo ya maji, lakini ni vile unawaza kimatamanio zaidi.
 
Huko mimi nimewahi kufika, hawakujenga mabondeni wala kwenye njia ya maji ni eneo salama kabisa, na sasa hivi njia ya maji imehamishwa na hayo maafa yametokea kwenye njia isiyo ya maji, lakini ni vile unawaza kimatamanio zaidi.
Wewe umewahi kufika tu lakini mimi huko ndo nyumbani kwetu...

Kama ni sehemu salama imekuwaje watu wamelambwa,na maporomoko (landslide) hayo.?

By the way, hoja yangu kwa ndugu niliyemkwoti ilikuwa ni yeye pengine "kutojua kabisa jukumu la serikali"..

Ndiyo maana nikatoa maelezo marefu kidogo kumkumbusha. Na ishu siyo Hanang - Katesh tu. Ni maeneo mengi ya miji na vijiji Tanzania watu wanaishi kwenye maeneo hatarishi kupindukia na bado mamlaka za kiserikali zinazohusika zikiangalia tu pengine mpaka waje wafe watu kama huko Hanang...

Nikatoa mfano wa Jiji la Mwanza (maana ndo naishi huku Kwa sasa). Kwamba, Kuna watu wanajenga nyumba tena za udongo wa kawaida kabisa kwenye vilele vya miinuko ya milima...

Serikali ipo na inatoa mpaka vibali vya ujenzi na inapeleka huduma zingine za kijamii kama maji na umeme huko..

Swali la kujiuliza ni hili;

Kwamba ina maana Tanzania tuna uhaba wa ardhi salama, ya kawaida na tambarare kiasi cha watu wa kawaida kujenga makazi kwenye maeneo hatari kama milima, mabonde nk nk? Au ni serikali kukosa mipango thabiti tu?

Ni wazi kuwa iko shida serikalini..
 
Back
Top Bottom