Maoni: Kama una miaka 25+ na humiliki kipande chochote cha ardhi (hata 2*2) kuna uwezekano mkubwa kufa masikini

WOTE TUKIMILIKI ARDHI MBINGU ATAMILIKI NANI?
Yesu akija atakuja kubomoa kile ulichojenga ili akupe kipya alichokujengea huko mbinguni.
Fanya faster mkuu, miliki ardhi, mchina anatoka shang'ai anamiliki kijijini huko ibadakuli wewe unatoka dar unashindwa kumiliki hata kiasarawe mzenga huko porini ambapo unaenda kwa daladala kwenda na kurudi.

tujiitahidi wakuu, inawezekana kabla ya miaka 25
 
Hivi nikinunua hiko kipande na sina hela ya kujenga si bure tu[emoji13][emoji13]mwisho wasiku kionekane kimetelekezwa kiuzwe tena[emoji13][emoji13].
Unakizungushia ukuta kama sheria inavyosema unakiaacha, kitakuwa kinapanda thamani chenyewe automatic.

Lakini mtoto wa kike hata usiponunua ardhi sawa tu;hahaha we si unakuta kila kitu umeandaliwa
 
huu utukutu na ukorofi mkuu.
Miongoni mwa watu watakaochomwa moto ni wale waliokataa kumiliki vitu vya dunia hii wakisubiri vya mbinguni.
Hata Yesu aliwahi kusema '' Miliki hadi nitakapokuja'' '' Occupy until I come''.

Hata babu wa Imani Ibra alinunua kipande cha ardhi kwa fedha
 
Unaweza usimiliki ardhi na ukafa bonge la tajiri, nan kakwambia ukimiliki ardhi hutokufa maskini? watu wanamashamba na majumba wanakufa wanakuja kugombea mali mafala wengine tu ambao hata hukuwa nao close.. leo mali za Erasto Msuya mpaka mkuu wa wilaya anaingilia..
 
Kwani uwanja wa taifa umeuhesabia?
 
Kama ardhi ni asset kwangu ni bora nipambane kuipata ya kutosha jiulize kama ardhi ingekuwa njia ya kutoka kimaisha naamini vijijini vingi Tanzania wakazi wake wangekuwa na matajiri sana kuliko mijini na miundombinu ingekuwa bora kuliko tunavyo ona hivi sasa hata uarabuni ambapo ardhi yao ni kame sana (jangwa) lakini wanaweza wasaidia au kupata na kuwapa wenye mawazo ya kufanyia ubunifu au kazi ili kuzalisha kwa manufaa ya wote lakini sisi wa subsahara desert huwa tuna ubinafsi kwa maana usipo pata kwa urithi pambana kwa juhudi zako tofauti na hapo wewe ni sawa na yatima tuu !!!!!
 
Huna ardhi wewe[emoji23]
 
Nimejaribu kujadili kwa mujibu wa maoni yako kuwa,kama una 25+ yrs na humiliki ardhi unaweza kufa masikini. Na katika maelezo yangu nimejaribu kueleza ni jinsi gani kwa hapa Tz ardhi haiakisi utajiri lkn pia utajiri ni suala mtambuka, unaweza kuwa na hiyo ardhi then huwezi kukidhi hata mahitaji ya chakula! Kwa maana nyepesi utabaki kuwa masikini tu. Kama unashauri watu wajitahidi kumiliki ardhi hilo ni jambo jingine mkuu.
 
Unakizungushia ukuta kama sheria inavyosema unakiaacha, kitakuwa kinapanda thamani chenyewe automatic.

Lakini mtoto wa kike hata usiponunua ardhi sawa tu;hahaha we si unakuta kila kitu umeandaliwa
Ngoja nimsisitize mchumba anunue ardhi[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
 

Mawazo ya kimasikini haya.

..............Maishani kila mtu na muda wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…