Maoni: Kama una miaka 25+ na humiliki kipande chochote cha ardhi (hata 2*2) kuna uwezekano mkubwa kufa masikini

ardhi unayonunua kwa pesa alafu serikali inakupangisha usipoendeleza inapokonya bora kutwanga raha tuu!
 
kwenye maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa kila kitu na wakati wake! Mfano hai rafiki yangu X alinunua kiwanja 2016 mpka leo kipo vile vile wakat rafiko yangu Y kanunua mwaka huu na tayar kaanza ujenzi! tuache hizo mentality! mtu anaweza kufanikiwa katika umri wowote cha msingi kupambana
 
Handeni nina hela 5.
Lakini siwezi kusema nina Mali.
Maana ardhi kule haina thamani kwa miaka ya sasa labda baadae.
hata VX ukiwa hujui ni nini haina ishu saana.
ndio maana almasi mwadui walikuwa wanachezea usoro na bao leo inatafutwa mji mzima ni mashimo.

chekecha kichwa huko handeni mbwana.... acha hizo😎😎😎
 
unanunua kiwaja 5milioni kisemvule huko halafu unatumia miaka 20kujenga.. Sasa hiyo 5milioni kwanini usiingie nayo mtaani ukapambana mwanzo mwisho kwa miaka 20 halafu baada ya hapo umuhamishe mtu mikocheni/kawe beach/ununio/ au hata Goba basi.

Akili za kukimbilia kuzika hela ardhini kwa kujidanganya unamiliki asset basi Watanzania wengi sana wangekuwa matajiri, Wahindi wapo mjini miaka nenda rudi wanatafuta hela na ukizisachi account zao unakutana na mamilioni yenye uwezo wa kununua nyumba popote pale na walivyowajanja bado hawajenga hapa wananunua nyumba Canada/London na wengine sikuhizi wananunua apartments Dubai wanapangisha..

Tuache akili za kijamaa tunaishi dunia ya mabepari na ubepari. Eti unamiliki asset ambayo umetumia miaka 20 kuitafuta wakati mwenzako anamiliki investments ambazo faida yake inamuweka kwenye hekalu ambalo anaweza kujenga in 2month.
Tuache maisha ya kurithi,uoga na akili za kijamaa aisee, tujikite kwenye kupambana na kuongeza mapato yako maradufu ili watoto wasije kurithi nyumba baadala yake warithi biashara na usimamizi wake hili ndilo lenye msaada kwao,, Kariakoo pale vijana wengi wameachiwa urithi wa vibanda ambavyo wameishia kuviuza kwa wakinga/waarabu/wachaga na mwisho wa siku waliowengi wamebaki masikini maana hawakuwa na akili wala elimu ya kumiliki na kuzungusha hela..
 
Mbinguni kuna makao mazuri sana x2


Anayekajua haka kawimbo tuimbe wote


[emoji23][emoji23][emoji1492]‍♂️[emoji1492]‍♂️[emoji16][emoji16]
 
Naunga mkono hoja yako Mkuu,viwanja havijawahi kuisha ndio maana hata Posta kila leo mabati yanazungushwa ujenzi unaendelea. Ukiwa na pesa hata gorofa ni kiwanja unavunja unaset plan zako maisha yanaendelea. Shida yetu wengi tunatafsiri utajiri kama umiliki. Utajiri ni mfumo unaojengwa kwa ajili ya kuwekeza na kumaintain assets zako kwa malengo ya kuingiza faida kwa muda mrefu ujao. Ni kuhakikisha kesho inakukuta na kukuacha uko well off.
 
"Nchi za kimasikini"[emoji23][emoji23][emoji23]Hivi unadhan kijana wa kiarabu wa 24-30 priority yake ni ardhi??au kijana wa Denmark awaze ardhi ya 10m??ebu kua serious kidogo mkuu,nkienda apo Kisarawe napata kiwanja cha 100k-300k kikubwa tu!!
Mbona huna sasa?
 
Ukiwa na kiwanja kinakuzuia kuwa na pesa?
 
Kiwanja ulichonunua mil5 Kisemvule kinakuzuia kutafuta hela?
 

Nani amekwambia kuwa na ardhi ndio utajiri?
 
Kiwanja ulichonunua mil5 Kisemvule kinakuzuia kutafuta hela?

hiyo mil 5 huoni kama ndio kianzio kwa maana ya mtaji?.
Ukishakinunua kikawepo utaanza kudunduliza ujenge kwa muda wa miaka kadhaa na hizo hela na muda ungetumia kwenye mihanjo mingine ambayo ingekufikisha mbali.
 
Ngoja siku kodi ya ardhi ikiwa kubwa mtayakimbia hayo mashamba yenu
 
Katiba ya nchi imekaa kimya hapa
 
sina mpango wa kununua kiwanja

sina mpango wa kujenga

nime assume kodi ni 1M per month

nime assume pia nitaishi miaka 100 (ukitoa niliyonayo sasa)

nimepata kuwa nahitaji bank niwe na 36 Billion.

by now bank kuna 152 Billion na bado zinaendelea kuongezeka

Bado unaniambia ninunue kiwanja? Chanini? nifanyie nini?

Alisikika mtu akijisemea moyoni hayo.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…