Maoni Yangu: Kauli hii ya Rais Samia imekaa kibabe sana! Je, ni hasira?

Maoni Yangu: Kauli hii ya Rais Samia imekaa kibabe sana! Je, ni hasira?

Wamemfikisha hapo , she should fire them . Mbona simple ?! Nasema something is wrong ? Some one is controlling her . Au she is on depression
Kayataka mwenyewe kuwasikiliza hao na nina imani walimwambia usihofu wabongo watapiga kelele mwanzoni then wataacha na maisha yataendelea sasa hili dubwasha la bandari linawaka moto kila iitwapo leo hata dalili za kuzimika hazipo😁
 
"Hakuna mtu mwenye ubavu na misuli kuigawa nchi hii, kuiuza au kuharibu amani yake iliyodumu kwa miaka mingi".

Simply ni kuwa ata yeye anatambua hakuna wa kuiharibu hii nchi akiwemo yeye mwenyewe kwa hiyo Hilo jambo la bandari limesikika na litashughulikiwa kama wananchi na maoni ya walio wengi yanavyoelekeza kwa kuwa nchi ya wananchi wenye amani Yao na Umoja wao Kuna nguvu nyuma yake inailinda hii nchi.

Kwa hiyo haya yeye hawezi kupuuzia Hilo.

Linalokwenda kutokea sasa ni mojawapo kati ya haya mawili.

Kuachana na mkataba na DP World.

Ama la kurekebisha kwa mujibu ya maoni ya wananchi na wadau walio wengi.

Tunataka uwekezaji wenye Tija.
 
Licha kudai kukaa kimya na kuendelea kukaa kimya kuhusu sakata la Bandari lakini bado akazungumza, hakukaa kimya kama alivyodai ina first statement...
Ndio Iko hivyo kuna sehemu alisema Baba ASKOFU nimekusikiliza vizuri, ASKOFU alimpa makavu mengi sana ambayo hakutarajia hasa pale kwenye tukikemea kama tulivyofanya sasa msiseme tunachanganya dini na siasa.
 
samia huwezi shindana na taasisi kama TEC. Endelea kujifanya kibri na kushupaza shingo.

Hao wana mizizi mirefu utaumia.
TEC ni Vatican, Vatican wako na MAKUNDI kama "Jesuits" na "MAFIA," na mengine mengi. Dola ya Roma ndio hadi sasa inatawala dunia.

ilianza Babeli ikaja Uajemi, kisha Uyunani na sasa ni Roma. hadi arudipo Yesu kwa mara ya pili (na ni hivi karibuni).

YESU NI BWANA&MWOKOZI
 
Rais Samia ndiye mkuu wa majeshi yote nchini na kwakawaida jeshini huwa hakuna kumbembelezana wala lugha laini ya kufurahisha kwahiyo alichokizungumza ndivyo inatakiwa kuwa Kwa mtu ambaye ni amiri jeshi mkuu
Ni amiri jeshi mkuu kwa majeshi, siyo kwa raia........sidhani kama una uelewa wa hili.
 
Atanyooka tu yeye ni mmoja na jopo lake la wachumia tumbo, hatashinda akili za watu million 40 awe tu makini.
Najua roho inamuuma sana juu ya hili la bandari.
 
Rais Samia ndiye mkuu wa majeshi yote nchini na kwakawaida jeshini huwa hakuna kumbembelezana wala lugha laini ya kufurahisha kwahiyo alichokizungumza ndivyo inatakiwa kuwa Kwa mtu ambaye ni amiri jeshi mkuu
Sitafanya lolote kwenye DP world agreement! Sitajibu nitanyamaza tu ila DP world watakabidhiwa bandari zote! Hakuna mwenye ubavu wa kuniambia cha kufanya mimi nimeamua! Sheria zitabadilishwa na Bandari watapewa hakuna mwenye ubavu wa kuleta fyoko! Ndio lugha ya nani kama mama hii! kama hamjui kusoma kati ya mistari.
 
Back
Top Bottom