Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Chuo kikuu cha Ardhi kimetoa Taarifa kwa umma kikieleza kuwa Mapacha wawili wanaofanana ambao walifanya mahojiano na kituo Cha Wasafi FM 06/03/2024 kuwa Mapacha hao watachunguzwa kutokana na kusema kuwa mmoja kati yao amewahi kumfanyia mwenzake mtihani wakati wakisoma shahada ya kwanza katika chuo hicho.

Katika mahojiano hayo Mapacha hao walisikika wakisema mmoja kati yao amewahi kumfanyia mwenzake mtihani wa Hydrolojia ambao ulikuwa n mtihani wa marudio (Supplementary) kwa kutumia kitambulisho Cha pacha mwingine.
Wala hawafanani,mmoja sura yake pana kuliko mwenzake.
 
Walimaliza 2021 sio mbali mkuu.

Hao mabinti walikosea, hii kitu itawapotezea muda.
Kwa nature ya nchi zetu, akitokea mwanasiasa hapo kati akalivalia njuga ili apate umaarufu hawatoboi hao.
Wangejitahidi sana basi wasikitaje chuo wala mtihani, sasa wao hadi mtihani wameutaja, muda wa kuufanya wameutaja.

Acha tusubiri.
Halafu pia wameharibu credibility ya chuo.
 
Hivi unakiri vipi kwenye kweye TV inayotazamwa na watu wengi hivyo jambo linaloweza kukuingiza matatani? Haya sasa mambo yameharibika!

Chuo Kikuu Ardhi kimepata taarifa kupitia Wasafi FM, chaneli ya YouTube ya mahojiano kati ya waandishi wa habari na mapacha wawili wanaofanana. Mahojiano hayo yalirushwa siku ya Jumatano, tarehe 6 Machi, 2024 kwenye kipindi cha Jana na Leo.

Kwenye mahojiano hayo, mapacha hao walisikika kupitia chombo hicho cha habari kuwa walisoma “Chuo cha Ardhi” na kufanya mtihani wa Hydrolojia. Katika mtihani huo, mmoja wa mapacha hao alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) kwa kutumia kitambulisho cha pacha mwingine.

Chuo Kikuu Ardhi tunchunguza ukweli wa taarifa hizo na baada ya uchunguzi kukamilika, umma utajulishwa matokeo ya uchunguzi huo

Imetolewa na:
Prof. Evaristo Liwa
Makamu Mkuu – Chuo Kikuu Ardhi
7 Machi, 2024

View attachment 2927199

Pia soma: Chuo cha Ardhi kinapaswa kuchukua hatua dhidi ya mabinti mapacha waliokiri kufanyiana mitihani
Baba levo haijui Supplementary
 
Mbwembwe tu hizi kuwapoza wananchi lakini hizo degree wataendelea kuwa nazo.

Unafikiri wataweza kuthibitisha kama kweli?..

Mfano hao mabinti wakisema walikuwa wanafurahisha baraza..?

Subiri uone.
 
Chuo kitawezaje kuthibitisha hili?
Hao wanaweza kukataa tu kirahisi kwamba walikuwa wameongopa kutafuta umaarufu.
Ila hawana akili na wasafi FM pia hawana mhariri wa vipindi ni uhuni na utoto tu.
Ona Sasa wanaenda kuwaharibia maisha hao wajinga. Wawape Ajira hapo wasafi wakifutiwa degree zao.
 
Back
Top Bottom