Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo

Wala hakuna kesi hapo, na chuo hakitakiwi kuthibitisha jambo lolote, wahusika wameshakiri wenyewe, kinachofuatia hapo ni kuwafutia hayo matokeo yao.

Ujinga unaenda kuwaharibia future hao watoto, kama matokeo yakifutwa maana yake hata vyeti walivyopewa kwa kufaulu masomo havitakuwa valid tena, na kwasababu hiyo, hata kazini kama walipata kazi kwa qualification zao, wataenda kupoteza ajira zao/yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Waandish hawafai hapo wao wako zao pemben wanasoma mchezo
 
Hao ni mapacha ambao wanafanana sura sidhani kama miandiko yao inafanana pia. Wakitaka kutrace kwa mwandiko kama haifanani watakamatika tu.
Ni ngumu sana,kwani mwandiko mtu si anaweza badili .Any kisheria ni haiwezekani kudhibitisha,labda kama msimamizi siku ya mtihani angeshtuka na kumkamata huyo Kulwa/Dotto. Otherwise hakuna case.
 
Ni ngumu sana,kwani mwandiko mtu si anaweza badili .Any kisheria ni haiwezekani kudhibitisha,labda kama msimamizi siku ya mtihani angeshtuka na kumkamata huyo Kulwa/Dotto. Otherwise hakuna case.
Kwenye uchunguzi mwandiko unaweza kuchunguzwa kujua ni wa nani kwa hiyo hapo wajiandae kisaikolojia😂😂😂😂
 
Akihojiwa kwenye kipindi ,Pacha aliyekuwa anaisoma Chuo Kikuu Cha Udom pamoja na Mwwnzie wameingia matatani baada ya kuropoka kwamba alimfanyia Mwwnzie Mtihani wa marudio wa somo.la Hydrology baada ya kufeli Kwa kutumia kitambulisho Cha pacha mwenzake bila kutambulika.

Chuo Kikuu Cha Udom kusema baada ya kusikia mahojiano hayo kimeanzisha Uchunguzi wake kisha kitatoa taarifa rasmi ya hatua za kuchukua.
---
Kufuatia mahojiano na pacha waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu Ardhi wakieleza jinsi walivyoweza kufanyiana mtihani, uongozi wa chuo hicho umesema unafanya uchunguzi wa jambo hilo.

Katika mahojiano hayo ya Wasafi FM yaliyofanyika Machi 6 mwaka huu, pacha mmoja alikiri kumfanyia pacha mwenzake mtihani wa marudio (supplementary) wa Hydrolojia kwa kutumia kitambulisho cha mwenzake baada ya kufeli mtihani huo.

“Tulikuwa chuo sasa unajua chuo tunasoma kozi ambayo kuna masomo ambayo tunaendana kwahiyo sasa kuna somo moja ambalo linaitwa Hydrology tukawa tunaingia class moja lakini bahati mbaya mwenzangu akapata supp mimi nikawa nimetoboa, sasa nikamwambia hapo kwenye supp tulia nitafanya mimi [..] akanipa kitambulisho chake nikamaliza akatoboa supp na hawakuwahi kujua,” mmoja wa pacha alieleza.

Aidha, uongozi wa chuo hicho umesema baada ya kufanya utafiti na kubaini ukweli wa taarifa hizo, umma utajulishwa juu ya matokeo ya uchunguzi huo.

My Take
Pale Mjinga mmja anaporopoka upumbavu akidhani sifa kumbe amefanya kosa ambalo linaweza kumsababishia kufutiwa degree yake na kufikishwa kizimbani Kwa makosa ya udanganyifu.

Kuna watu wanaojiita Wasomi ila Wana ujinga mwingi kichwani kama Hawa pacha.
 
Akihojiwa kwenye kipindi ,Pacha aliyekuwa anaisoma Chuo Kikuu Cha Udom pamoja na Mwwnzie wameingia matatani baada ya kuropoka kwamba alimfanyia Mwwnzie Mtihani wa marudio wa somo.la Hydrology baada ya kufeli Kwa kutumia kitambulisho Cha pacha mwenzake bila kutambulika...
Kama hawana ushahidi watawezaje kubaini

Unfortunately hao mapacha wapo wanafanya ubunifu wa mavazi
 
Back
Top Bottom