Mapato sherehe ya Mavuno Jimbo Katoliki Dar ni Tsh. Bil. 4.5

Mapato sherehe ya Mavuno Jimbo Katoliki Dar ni Tsh. Bil. 4.5

Ni kweli kanisa katoliki linatumia Sadaka kujenga shule nyingi sana zenye majina makubwa

Mfano St francis mbeya

Marian bagamoyo

St joseph dar es salaam

Swali kubwa ni JE KWENYE HIZO SHULE ZA KATOLIKI WATOTO WA WAUMINI WALIOTOA SADAKA KUZIJENGA HUWA WANASOMESHWA BURE ? WANAPEWA DISCOUNT YA ADA AMA WANALIPA SAWA SAWA NA WATOTO WA DINI ZINGINE..

MFANO WAISLAM WANAOSOMA ST FRANCIS WANALIPA ADA KIASI TOFAUTI NA WAKATOLIKI WANAOSOMA ST FRANCIS AMA WOTE ADA NI SAWA ?
Huduma Bora ni Gharama,
Hakuna ubaguzi kwenye ada wote sawa
 
Juu hapo ulikiri kuwa michango ni lazima mtu asipo changa kwenye jumuiya hapakaliki. Sio wewe uliesema?

Hizo tabia za kususia misiba kisa mtu haji kwenye jumuiya mnayo sana. Naziona sana Kwa majirani zamgu
Tafadhali nionyeshe wapi mimi nilipoandika maneno hayo?

Halafu sahihisha siyo kususia msiba haususwi kinachofanyika ni ”marehemu muhusika hafanyiwi ibada” ila vingine vyote vinafanyika na kama nilishindwa kumkiri Mungu nikiwa na pumzi aliyonipa ninyi Kanisa ni nani hata mkusanyike mje kuilazimisha maiti yangu imkiri?

Wakatoliki sisi siyo wanafiki,imani sahihi ni ile nianze nayo mimi nikifa ninyi mnaobaki muitimilize kwa kuniombea heri siyo muanze nayo nyie mimi niitimize nikiwa mfu huko ni kupoteza wakati.
 
Hongera wana Jimbo, hongera kanisa moja la mitume.

Kumbuka haya ni mapato ya sherehe ya mavuno tu, na ni kwa jimbo moja tu.

View attachment 2833300
Ukijumlisha vyanzo vingine vya mapato mfano:
1. Tegemeza jimbo
2. Miito mitakatifu
3. Sadaka za kawaida
4 mchango wa pili
5. Bahasha za Noeli/Pasaka
6.
7.
8.
9.

Kisha kadiria kwa Nchi nzima. Nadhlimani utakubaliana na mimi ukubwa wa hii taasisi.

Ni tofauti kabisa na "ndugu zetu wa upande wa pili". Heko kanisa, heko watoaji.

PS
Sijajua matumizi ya hizo pesa maana kama kuna ujenzi basi itaanzishwa account ya kuchangia.
Wajinga ndio......
Na waliochanga wataendelea kuwa maskini, limbukeni, fukara na kuendelea kutapeliwa kiroho!🤣😂😅
 
Wajinga ndio......
Na waliochanga wataendelea kuwa maskini, limbukeni, fukara na kuendelea kutapeliwa kiroho!🤣😂😅
Usijifariji bro,maskini utaendelea kuwa wewe wanaotoa hawawezi kuwa maskini.nakuonyesha kitu hapo chini kitizame kisha jitafakari yupi maskini wewe au wanaojitoa kwa kazi ya Mungu?

Hii tulifanya harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mapadre inatakiwa 200mill sasa unaweza ukahisi watu kama hawa wapo wangapi na zitapatikana bei gani?
IMG_20231205_120643.jpg
 
Maendeleo ya hii taasisi yapo wazi. Na sasa linajengwa kanisa la kimataifa huko Gezaulole. Na nguvu ni zao pekee. Huku wakiwa na taasisi zao za Elimu anzia awali mpaka chuo kikuu, mahospital n.k. Hivyo uwekezaji wao hauna mashska kabisa mkuu.
Kabisa na mapato yanawekwa wazi tofauti na wenzetu
 
Tafadhali nionyeshe wapi mimi nilipoandika maneno hayo?

Halafu sahihisha siyo kususia msiba haususwi kinachofanyika ni ”marehemu muhusika hafanyiwi ibada” ila vingine vyote vinafanyika na kama nilishindwa kumkiri Mungu nikiwa na pumzi aliyonipa ninyi Kanisa ni nani hata mje kuilazimisha maiti yangu imkiri?

Wakatoliki sisi siyo wanafiki,imani nianze nayo mimi nikifa ninyi mnaobaki muitimilize siyo muanze nayo nyie mimi niitimize nikiwa mfu huko ni kupoteza wakati.
Mbona mnaombea wafu, mnauhakika wanawasikia..?
 
Back
Top Bottom