Haiwezekani kiongozi wa umma anapata ajali halafu wananchi hawapewi taarifa , hii nchi inao wenyewe ambao ni sisi wananchi , hapa ni lazima Spika Ndugai na wenzake watoe maelezo ya kutosha ili waeleweke , au la tuambiwe ajali ya Nditiye ni ya kuanguka bafuni ambako si rahisi watu kuona , lakini vinginevyo hakuna ajali yoyote ya barabarani ambayo ni ya siri .
Juzi Katibu Tawala wa Arusha amefariki kwa ajali lakini tumeonyeshwa hadi gari alilopata nalo ajali lilivyoharibika , na tukaelezwa alikuwa anatoka wapi na kuelekea wapi , huyu mnayetaka kuficha ajali yake ametenda kosa gani ?
Rais wa Tanzania Dr Magufuli aliwahi kusema kwamba Watanzania siyo Wajinga sana .
Tuambiwe ukweli ili tuelewe