Maria Sarungi ashindwa kuja kumzika baba yake kwa kuhofia usalama wake

Maria Sarungi ashindwa kuja kumzika baba yake kwa kuhofia usalama wake

Mkuu nawe usipotezwe kirahisi, serikali gani yenye habari na haka kamaria?!!! Wakimtaka si yupo Kenya tu hapa wanampigia tukio Moja la kimataifa basi, anajistukia tu baada ya Kila porojo yake kufeli. Ile movie yake ya kutekwa ilivyobuma vibaya ndo anazidi kuona aibu.
kenya sio lumumba mkyundu wewe
 
Ukiwa na mtoto kama Maria ni utukufu mkubwa japokuwa amekulia kwenye maisha mazuri lakini angalau anashare machungu na sisi masikini.pole saaana dada endelea kutumia elimu yako vizur.na sisi tunakuombea ata Mungu anaona ibada yako.
Kwa jicho la kawaida unaona anashare maumivu na wewe, funguwa jicho la tatu uone wired funds zinazoingia kwenye account yake kutoka kwa mabeberu.
 
Sio kama kwasababu mtu ni mkubwa sana na kwamba anajua kuwa yeye atazikwa tu.

Hebu fikiria hii scenario, umepanda ndege na mabodigadi wako unapita juu ya Bahari mara ndege inapata hitilafu inatumbukia Baharini kama ilivyokuwa Malaysian Airlines.

Hata huo mwili wa kuzikwa inakuwa haupo.

Pole sana Dada Maria Sarungi Mungu anaona yote.
 
A
Sawa, kama baba yake alikuwa mtu mwema kwa Samia mbona huyo Samia hakuguswa na kifo chake? Shida ya Samia anataka kila mtu amuite mama. Yeye kila kitu utasikia ni hisani kutoka kwa mama. Upumbavu mtupu!
Tatzo nkwamba aliye asisi "kwa hisani ya..." alipongezwa na kutukuzwa keamba anastahili vitu vyote kuitwa kwa hisani yake.

Hivyo tutarajie maraisi wote kuwa na hulka ya namna hiyo. Kwakuwa ndo swaga wanazo zihusudu wapiga kura wao.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Godbless Lema amemfariji Maria Sarungi kupitia ukurasa wake wa X kutokana na Maria kushindwa kufika katika msiba wa baba yake

“Nimekusikiliza ukiongea kwa njia ya mtandao wakati wa salamu za rambi rambi ukiwa mbali na halaiki iliyokuja kumuaga baba yako Prof Sarungi hapa Karimjee Hall. Naelewa maumivu yako sana tu , usalama wako ni muhimu na hauwezi kuupuuza. Nafsi yako itakuwa inaumia sana. Jipe Moyo Mkuu sana kwani hatuna muda mrefu sana kufika ktk hatua muhimu ya mabadiliko.” - Godbless Lema

Yapi maoni yako

Pole Yake!
 
Pole sana kwake inasikitisha mno
Lakini maisha ni mapambano !
Hata mtu akiogopa na akawa muoga namna gani bado matatizo ya kila aina yatamjia tu na ni lazima akabiliane nayo !
Mtu kushindwa kuhudhuria msiba au mazishi ya mzazi kwa kuhofia Usalama wa mhusika hata Mungu na hata wale wanayoiamini mizimu itakuwa wameelewa ni kwanini hajahudhuria na watakuwa upande wake !!
 
Siyo kweli kosa kubwa alilofanya Maria Sarungi ni kutochangia hata mia msiba wa baba yake mzazi hata kama haji kwa mujibu wa ndugu zake

Hata kama haji angechangia basi mchango gharama za mazishi hakuchangia hata mia
Wewe ni mwenyekiti wa michango ya rambi rambi? Na rambi rambi zina ukomo kwamba lazima zitolewe kabla ya mazishi..kesho akitoa utasemaje..? Acha kudandia misiba ya watu, ni Maria peke yake ameshindwa kuja? Mbona kaka na dada yake nao wameshindwa kuja..! Acha kuzungumzia mambo ya ndani ya familia za watu!
 
Kukosoa katika baadhi ya Nchi za Afrika inatafsiriwa ni kukosa heshima kwa mamlaka !
Nimeiona Clip moja ya Kagame akijinasibu kwamba yeye ni bora mtu aje na bunduki amuue lakini hayuko tayari kupiga magoti kwa yeyote yule mahali popote pale !

Kwahiyo my take ni kwamba “ mkuki ni kwa nguruwe tu lakini kwa binaadamu ni mchungu 😳 !
🤣🤣😂
 
Siyo kweli kosa kubwa alilofanya Maria Sarungi ni kutochangia hata mia msiba wa baba yake mzazi hata kama haji kwa mujibu wa ndugu zake

Hata kama haji angechangia basi mchango gharama za mazishi hakuchangia hata mia
Unadhani hiyo ni familia masikini kama ya kwako kwamba inategemea michango ya watu kuendesha misiba?

Acha akili za kimasikini
 
Back
Top Bottom